Jambazi achomwa moto Kibiti

Jambazi achomwa moto Kibiti

Unafurahia kitendo cha raia kujichukulia sheria mkononi? Unayajua madhara yake?
Ndio maana nimekuwa mwangalifu kusema kama ni mhusika mkuu!!
Sifurahii kitendo cha raia kuchukua hatua mkononi ila PUBLIC PUNISHMENT sends a very powerful message than a verdict within the court's wall.
Hapo ni adhabu kwake pia onyo kwa wale wanaoona kuwa ukiiba yatakukuta haya, mahakamani ni adhabu kwa mtuhumiwa ila jamii haijifunzi kitu zaidi ya kusema kuwa jamaa yuko jela anakula ugali wa bure!
 
Mkuu hujawahi ibiwa/ vamiwa na jambazi/ kibaka! Hawa watu hawahitaji huruma hata kidogo, wanarudisha nyuma watu kimaendeleo na wako tayari wachukue pumzi yako kisa wanataka kitu ulichokitafuta kwa jasho lako!
Kuna mida kunakuwaga na mistaken identity au ukurupukaji wa raia wenye hasira hivyo mara chache wanaweza ua mtu ambaye sio sahihi, ila kama wanakuwa wamempata mtu sahihi, mi nasema AROSTIWE tu maana hamna namna.
Tokea vibaka waanze kuchomwa moto na raia walioamua kujichukulia sheria mkononi mitaani, je vibaka wamepungua au wameongezeka? Unadhani vibaka kuchomwa moto na raia walioamua kujichukulia sheria mkononi ndio solution ya hilo tatizo?
 
Umepimaje kuwa vibaka wameongezeka au wamepungua??
Endapo wangekuwa hawachomwi moto umepimaje kuwa wangekuwa vibaka wengi zaidi au wangepungua??
Upande wa adhabu kwangu naona ni moja ya solutions ingawa zipo solutions zingine za kuanzia ktk mizizi!
 
Kibiti watu wamekuwa na roho ngumu sana hebu tazama wanawake walivyo jasir mpaka wanachukua video

Sent from Samsung Galaxy S8 Plus using JamiiForums mobile app
 
Umepimaje kuwa vibaka wameongezeka au wamepungua??
Endapo wangekuwa hawachomwi moto umepimaje kuwa wangekuwa vibaka wengi zaidi au wangepungua??
Upande wa adhabu kwangu naona ni moja ya solutions ingawa zipo solutions zingine za kuanzia ktk mizizi!
Jaribu kusoma comment na kuielewa kabla hujaamua kuijibu,ni wapi nimesema vibaka wamepungua au wameongezeka?! Hukuona hiyo question mark niliyokua nimeiweka? au hujui question mark ina maana gani?
 
Jaribu kusoma comment na kuielewa kabla hujaamua kuijibu,ni wapi nimesema vibaka wamepungua au wameongezeka?! Hukuona hiyo question mark niliyokua nimeiweka? au hujui question mark ina maana gani?
Tokea vibaka waanze kuchomwa moto na raia walioamua kujichukulia sheria mkononi mitaani, je vibaka wamepungua au wameongezeka? Unadhani vibaka kuchomwa moto na raia walioamua kujichukulia sheria mkononi ndio solution ya hilo tatizo?
Okei, labda niseme MTU ANAPIMAJE kuwa vibaka wamepungua au wameongezeka maana naona neno 'unapimaje' umelichukulia personal sana!
 
Kama hujawahi kuvamiwa na jambazi/kibaka ni bora ukanyamaza kimya.... Kama ni kweli ni mtuhumiwa ndiyo adhabu yake anastahili...

Halafu hili tukio halijatokea KIBITI nimetokea Mbagala-Mbande, Wakurya wamefanya yao walimchinja shingo ndiyo wakaanza kumpiga moto huyo ni mwizi aliye shindikana kwa taarifa nilizo zipata
 
Wezi, wachawi na waongo wanachukiwa na jamii yote. Hata hivyo kitendo cha kutoa uhai wa mtu kinatoa thibitisho la kiwango cha uduni wa uelewa wa sheria. Na si wananchi tu, hata dola kupitia police imekuwa ikifanya hivo, tofauti ikiwa ni moto na risasi. Watu wamechoka, police wamechoka na uvunjifu wa amani, wanachukua sheria mkononi. Imani pungufu kwa mahakama zetu, ni moja ya sababu. Police hawana data base sahihi ya wahalifu, wakipelekwa mahakamani wanaachiwa. Matokeo ndio haya.
 
Back
Top Bottom