Arumeru: Mwanamke achomwa maji ya moto na mumewe

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,022
Reaction score
6,858
Mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Upendo Shabani, mwenye umri wa miaka 38, mkazi wa kitongoji cha Engorika, kata ya Kiutu, wilayani Arumeru, mkoani Arusha, anadaiwa kuchomwa maji ya moto na mumewe, Gibson Alfred, na kusababisha majeraha ya vidonda sehemu mbalimbali za mwili wake, ikiwemo kifuani.

Tukio hilo limetokea Septemba 19, 2026, majira ya saa tano usiku, ambapo Gibson Alfred anadaiwa kuchemsha maji kwa kutumia hita na baada ya maji hayo kuchemka kabisa, alimuagia mkewe kifuani na sehemu mbalimbali za mwili wake.

Akizungumza Upendo Shabani, ambaye ni mama wa watoto wanne, amesema kuwa si mara ya kwanza kwa mumewe kumpiga, akieleza kuwa amekuwa akivumilia vipigo vya mara kwa mara kutokana na watoto walionao.

Soma Pia: Mke adaiwa kumuua mumewe kwa sindano yenye sumu

Mwenyekiti wa eneo hilo, Bw. Praygod, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuiomba Serikali kuongeza nguvu katika kuhakikisha Gibson Alfred anakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
 
View attachment 3678372
Chanzo ni nini?
 
Back
Top Bottom