Jamani where is Mramba?

Chief mangi

Member
Feb 7, 2012
5
0
Jamani huyu babu aliyezeekea madarakani yuko wapi mbona simsikii? Hakuamini macho wala masikio uchaguzi uliopita 2015 tunamkaribisha tena Rombo kwa ugombea.
 

Joseph

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
3,520
1,225
Kuna siku nilimuona mjini akiwa anaingia katika moja ya ofisi pale wizara ya mambo ya ndani,ila kachoka sana siku hizi.
 

FredKavishe

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,090
1,195
Ujumbe kwa kijana yoyote atakayesimama Rombo 2015 au selasini kama atarudi kugombea.

Ni wakati wa kuifungua rombo sasa barabara tumeshajengewa nzuri kenya tunaiona kwa dakika chache tu.
Ushauri wangu kwa wagombea
1.Tujenge soko kubwa Rombo bidhaa zote zije chukuliwa pale ambazo wakenya wanahitaji kuanzia mahindi,sukari na vingine tukijenga hili soko tuzibe pia miaya ya njia zote za panya zinapoleka mazao yetu ya chakula kenya.
Tukifanikisha kujenga hili soko kubwa tutafaidikaje:
1.Tunatengeneza ajira kwa vijana wengi na wakina mama
2.Kuongoza kipato cha kodi
3.Kupanua uchumi wa rombo

2.Tufufue zao la kahawa lirudi kama enzi zake
Zao la kahawa sasa limekufa kwenye mashamba mengi tilifufue lilete tija tena tunaweza jenga na kiwanda kidogo cha kutengeneza kahawa yetu tutawezaje kufufua kahawa
1.Kupanda miche mipya
2.Kufanya kilimo cha kisasa zaidi

3.Wale wakina mama na wazee wanaopandisha ndizi siku za masoko labda ya mamsela na sehemu nyingine waundiwe utaratibu mzuri wasiwe wanalanguliwa bei zao na wanunuaji wa ndizi wanaoenda na mafuso rombo.

4.Lazima mbao zinazotoka kwenye msitu wa rongai zinufaishe wana rombo kwanza

5.Tujenge sehemu nzuri za utalii recreation centers
Hizi sehemu ziko chache sasa rombo tuwe wa kwanza kujenga hizo center tuweze kuvutia watalii wa ndani mfano kipindi hiki zaidi ya wachaga laki 3-8 wanarudi makwao kama kutakua na center nzuri ya kubembea kwa watoto na wengine kutulia tunaweza kupata mapato mazuri sana.

6.Tuboreshe sera za kilimo zetu pale rombo zitunufaishe wana rombo kwanza

Hizo ni sera chache sana shime kijana atakaweza kugombea azifanyie kazi sasa unaweza kuomba pesa za soko serikali kuu iskupe.

Well kama wewe kijana au selasini una uchungu kweli na wana rombo ushauri wangu huu ukitaka hii ifanikiwe ule mkopo wa milioni 90 wa gari wote utupe jimboni nunua mchanga na cement anza kufyatua matofali ukumaliza itisha kikao na wana rombo.

Siamini kama kuna wana rombo wenye itakia mema rombo watashindwa kutoa japo 1000 kwa mwezi ukipata watu 20000 una zaidi ya milioni 20 kwanini malengo ya soko yasifanikiwe na kujenga recreation center yasifanikiwe.

Tunahitaji wabunge watakao jali wananchi wao kwanza kabla ya family zao

Fred kavishe
 

DALA

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
1,238
2,000
I resently met him at a petrol station pale Gapco ya Leaders club alikuwa amepanda Rav4 Nyekundu akiendeshwa na mama mmoja hivi kwa vyovyote alikuwa mke wake! He is out safe and sound!

Wewe endelea kumsubiri Rombo!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom