Jamani tumekufa!!!!!!

Halafu hawa EWURA kazi yao si ku-regulate bei zisipande au wapo tu kama katuni vile pamoja na kupandisha huduma za umeme, bado huduma hizo ni mbovu kupindukia
 
Huu ni mpango maalum wa serikali kuhakikisha Baba_Enock anapunguza 18% ya matumizi yake katika baa kwa mwezi! I'll miss you my dear bottle come January 2011 - and Jose too!
 
Serikali kupitia EWURA imeridhia ongezeko la 18% ya bei ya umeme kuanzia January mwakani. Hilo ni pigo kwa mtumiaji na tayari ongezeko hili litakuwa na athari katika uchumi wetu. Wahanga wakubwa ni watumiaji wa majumbani ambao wenyewe hawana wa kumtwisha zigo hilo mtu yoyote tofauti na viwanda ambavyo vinaweza kufidia kwa kupandisha bei ya bidhaa zake.
WanaJF mnalionaje hili?

Source. TBC1
hii nchi ya tabaka la juu bana, weeeeeeee wacha tuuuuuuuuuuuuu, ila ndio tunakula na kunywa faida ya machaguo yetu ya mwezi Oktoba
 
nalaani kitendo hiki na hili ni zao letu wenyewe... we voted for this government so tujilaumu wenyewe

je kwa wale wataalam, viwango vipya vikoje ukilinganisha na nchi jirani kama kenya, uganda au zambia?
 
Jamani hizo bilions atakazolipwa lowasa na wenzake ni lazima tukamuliwe!!!!!!!!!!habari ndio hiyo!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
HIVI TANZANIA KUNA SIKU TUTASIKIA HUDUMA AU BIDHAA FULANI IMESHUKA BEI?KENYA KUPANDA NA KUSHUKA HUFANYIKA KUZINGATIA HALI HALISI!HAPA BONGO INAPANDA TUU MWAKA 2005 dumu la mafuta ya kula lilikua sh 18000 leo sh 50 000 wala hakuna anayejali wala kuandamana na hali hii

Hapa hakuna Serikali kuna Majambazi!
 
mnalalamika nini nyie? kwetu uswahilini tunatumia umeme kila kitu unanunua umeme wa buku unamaliza mwezi full kuchakachua, anayehitaji huduma anipm, vigezo na masharti kuzingatiwa!
 
kichwa cha habari hakifungamani na maudhui ya post yako
Ni kweli. ni lazima utakuwa umejiuliza tumekufa nini? Umekufa kupanda kwa bei ya umeme wewe unit moja ulikuwa unanunua Tsh 129 sasa unanunua 153 unadhani ni mchezo mkuu? Vile vile ni lazima uandike kitu ambacho kitawavutia watu kusoma post yako otherwise mtu atakuwa akiiona tu anaacha na kusoma post nyingine.
Post nazo ni kipimo mkuu?
 
Hahaha @samora10. Sniper wa nini ndugu wakati mafuta tumejipaka wenyewe!
 
Chadema yaandaa maandamano kupinga bei mpya ya umeme Wednesday, 22 December 2010 20:07

Hussein Issa na Eveline Kijumbe
Mwananchi

CHAMA Cha Demokrasia (Chadema), kimeandaa maandamano makubwa nchi nzima kupinga bei mpya ya umeme iliyotangazwa Desemba 20 mwaka huu na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura).

"Tutawaunganisha wanachama wetu wote wa mikoani tujumuike pamoja katika maandamano hayo ili kudai haki zetu za msingi, "alisema Mkurugenzi wa Oganization na Mafunzo wa Chadema, Singo Kigaira.

Kigaira aliwataka wafuasi wa chama hicho, wanachama na wananchi kuacha woga akieleza kuwa kila kitu kinahitaji mipango na katika maandamano hayo, kiongozi wa mipango hiyo ni Chadema.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Habari wa Chadema, Erasto Tumbo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa chama hicho kimeamua kuandaa maandamano hayo baada ya kutambua kuwa bei hiyo mpya ya umeme inamwumiza mwananchi wa kawaida.

"Maandamano hayo tutayafanya mwezi Januari na tutaomba wananchi watuunge mkono kwa sababu hii ni haki ya msingi. Hakuna sababu ya kuonewa hapa. Junuari tutatangaza siku maalumu ya maandamano hayo,"alisema Tumbo.

Aliendelea "Katika hali ya kawaida kabisa, mtu anakuwa na matumizi ya Sh1000 kwa siku, leo hii unampandishia umeme kwa asilimia 18.5, unadhani maisha yatakuwa rahisi kweli?"

Kwa mujibu Tumbo, Serikali ingeweza kutumia njia nyingine mbadala kuboresha upatikanaji wa umeme nchini bila kuwapandishia wananchi bei ambao kimsingi ni mzigo kwao.

Alisema moja kati ya njia hizo ni kufunga mitambo ya kisasa ya kuzalisha umeme ndani ya bahari ili kundokana na tatizo la upungufu wa maji ya kuzalisha nishati hiyo.

Tumbo alisema baadhi ya nchi duniani, zinazalisha umeme kwa kutumia maji ya bahari jambo ambalo lingeweza pia kufanyika Tanzania kama viongozi wangekuwa wabunifu.

"Pia Serikali ilipaswa kuboresha vifaa vya kutengenezea umeme wa jua ili umeme huo uzalishwe kwa wingi na sio kupandisha gharama za umeme kiholela na kutuumiza (wananchi),"alisema.

Kwa mujibu wa Tumbo, kiini cha kupanda kwa bei ya umeme ni deni kubwa la Serikali katika taasisi zake, wizara na ofisi nyingine ambazo kwa kawaida hazilipi kodi hivyo kinachotakiwa ni kuwaeleza wananchi ukweli kuhusu madeni hayo.

"Lazima tuelezwe ukweli kwamba Serikali na vigogo wake wanadaiwa shilingi ngapi kwani ndio hasa chanzo cha ongezeko la bei za umeme hapa nchini. Wananchi tumeshachoka kuburuzwa kama hatuna elimu, "alisema Tumbo.

Alisema ongezeko hilo la bei ya umeme la asilimia 18.5, linaamanisha kuwa uniti moja sasa itakuwa inauzwa kwa Sh 367.80 kiasi ambacho kitamuumiza mwananchi wa hali ya chini.

Tumbo alienda mbali zaidi na kusema anaamini kuwa Serikali imeamua kupandisha bei hiyo ya umeme ili kupata fedha za kuilipa kampuni ya Dowans inayoidai Tanesco mabilioni

Alisema haiingii akilini kuona Tanesco inapandisha bei ya umeme wakati baadhi ya Watanzania hadi sasa wanashindwa kumudu gharama za kuingiza nishati hiyo majumbani mwao.

Desemba 20 mwaka huu Ewura, iliruhusu Tanesco kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 18.5 kuanzia Januari Mosi mwakani.

Mkurugenzi wa Ewura, Haruna Masebu, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa ongezeko hilo la bei ni chini ya mapendekezo ya Tanesco kwa asilimia 16.1.

Kwa mujibu wa Masebu, Tanesco ilipendekeza umeme upande bei kwa asilimia 34.6, lakini baada ya uchambuzi wa kina, mamlaka ilikubali kuruhusu nyongeza ya asilimia 18.5 kwenye nishati hiyo.

 
Back
Top Bottom