Mercy Clara
Member
- Mar 11, 2010
- 16
- 0
Hivi mwanaume anapoamua kwenda kumchumbia mtu mwingine huku akiwa na msichana mwingine ambaye anamwonyeshea mapenzi kama kwamba ndiye mtarajiwa kumbe anamng'ong'a kisogo na kujifanya mkali kama ndiye baba mwenye nyumba kumbe loh. Ni hivi kulikuwa na mtu kaka na kaka mmoja ana girl friend wake kwa muda mrefu na kila mtu alikuwa huru kwa mwenzake na hata mmoja wapo akiwa na shida husaidiana sababu wote ni wafanyakazi. Juzi kati mwanaume alimfuata dada wa watu na kumwomba hela fulani eti ana shida sana ya haraka anaomba amuazime then atamrudishia, dada wa watu bila kujua lile wala lile akampa. Baada ya siku kama moja kupita ndio akapata udaku kutoka kwa watu wanaompenda eti huyo mwanaume ametoa mahali sehemu kuna mtu anataka kumwoa, dada akashtuka kiasi ila coz she's strong woman akaamua kulifuatilia na kuja kugundu kuwa ni kweli sasa basi kumbe ile hela aliyomuazima yule jamaa ilikuwa ndio ya kuongezea kwenda kulipa mahali kwa mwanamke mwenzake bila yeye kujua. Mbaya zaidi huyo anajidai kidume anaomba msamaha na kudai bado anahitaji mchango wake zaidi. Sasa huyo ni uchizi au? Inaboa sanaaaaaaaaa!
Mbona sielewi sielewi hapo? Embu nisaidieni wana wa JF!
Mbona sielewi sielewi hapo? Embu nisaidieni wana wa JF!