Jamani tujaribu kuwa wawazi katka mahusiano!

Mercy Clara

Member
Mar 11, 2010
16
0
Hivi mwanaume anapoamua kwenda kumchumbia mtu mwingine huku akiwa na msichana mwingine ambaye anamwonyeshea mapenzi kama kwamba ndiye mtarajiwa kumbe anamng'ong'a kisogo na kujifanya mkali kama ndiye baba mwenye nyumba kumbe loh. Ni hivi kulikuwa na mtu kaka na kaka mmoja ana girl friend wake kwa muda mrefu na kila mtu alikuwa huru kwa mwenzake na hata mmoja wapo akiwa na shida husaidiana sababu wote ni wafanyakazi. Juzi kati mwanaume alimfuata dada wa watu na kumwomba hela fulani eti ana shida sana ya haraka anaomba amuazime then atamrudishia, dada wa watu bila kujua lile wala lile akampa. Baada ya siku kama moja kupita ndio akapata udaku kutoka kwa watu wanaompenda eti huyo mwanaume ametoa mahali sehemu kuna mtu anataka kumwoa, dada akashtuka kiasi ila coz she's strong woman akaamua kulifuatilia na kuja kugundu kuwa ni kweli sasa basi kumbe ile hela aliyomuazima yule jamaa ilikuwa ndio ya kuongezea kwenda kulipa mahali kwa mwanamke mwenzake bila yeye kujua. Mbaya zaidi huyo anajidai kidume anaomba msamaha na kudai bado anahitaji mchango wake zaidi. Sasa huyo ni uchizi au? Inaboa sanaaaaaaaaa!
Mbona sielewi sielewi hapo? Embu nisaidieni wana wa JF!
 
nani alimuambia kwenye mapenzi kuna kukopeshana, huwa tunapeana tu!....alimuuliza huyo mkaka juu ya hizo tuhuma na alipewa hadithi gani?......mwanaume unatakiwa ukae nae **** moja, ukikaa nae yote mawili mambo ndio kama haya.
 
Yaani hiyo ni kweli kabisa na alithibitisha hayo baada ya kufanya upelelezi wa kina. Yeah ni kweli wanawake tunatakiwa kukaa mguu moja ndani wa pili nje!
 
thats so selfish of that kaguy.inaelekea huyo jamaa alikuwa anamtumia tu dada watu na hampendi wala nini.mshauri huyo mdada asimsamehe aachane nae atapata mwingine atakaye thamini penzi lake.
 
Alimuuliza kabisa na kujifanya usisikilize ya watu, matokeo yake akawa anawapigia simu marafiki zake na kuwatukana eti kwa nini mmemwambia!
 
Kila kukicha mambo yanaongezeka ..ila huyu mwanaume ana roho mbaya na ngumu kama Israel mtoa roho.Huyo dada amwambie tu ameshamsamehe na dada wa watu aendelee na 50 zake hakuna penzi hapo zaidi ya utaperi
 
yeah kweli kabisa huo ni utapeli mkubwa mnoooooooo
Hivi hawa watu wataacha lini hizo tabia zao?
 
Mbona hii wala si ngeni??? Watu wanakuwa na watu mpaka siku ya arusi na hawajui!!

Swala la kuwa muwazi kwenye mahusiano inategemea dhamira ya wapenzi wenyewe. Kama unadhamiria awe ndio mwenzi si rahisi kumfanyia ujinga huu but kama ni mapozeo na kipotezea muda you dont have to.
 
Yeah ni kweli wanawake tunatakiwa kukaa mguu moja ndani wa pili nje!
Ndo maana mapenzi ya dhati siku hizi hakuna ama ni wachache sana wenye kuendeleza utamaduni huo. Sijui tunaelekea wapi? Mwenyezi tunusuru.

Aliyebahatika kuoa/kuolewa atulie na ndoa yake jamani,mbona nyama ni ileile buchani? Kama mpishi hajui mapishi tujaribu kuingia pamoja jikoni tuelekezane na hatimae tutapata kitu tunachokitaka.
 
Mbona hii wala si ngeni??? Watu wanakuwa na watu mpaka siku ya arusi na hawajui!!

Swala la kuwa muwazi kwenye mahusiano inategemea dhamira ya wapenzi wenyewe. Kama unadhamiria awe ndio mwenzi si rahisi kumfanyia ujinga huu but kama ni mapozeo na kipotezea muda you dont have to.[/QUOTE]

Huo ndo ukweli wenyewe. Mambo ya kutumiana yapo sana. Na mbaya zaidi ni vigumu kujua kama unatumia hadi inakuwa too late. Hata hivyo inabidi tuwe makini tunapokuwa kwenye mahusiano kabla ya ndoa. Kwa nini watu wanajiachia kiasi hicho? Hata kwenye ndoa, inabidi mtu ujiamini wewe mwenyewe tu. Mwenzio unaweza kumwamini lakini usijiingize mzima mzima. Inauma sana kufanyiwa michezo michafu kwenye mahusiano.

Ndo maana mapenzi ya dhati siku hizi hakuna ama ni wachache sana wenye kuendeleza utamaduni huo. Sijui tunaelekea wapi? Mwenyezi tunusuru.

Aliyebahatika kuoa/kuolewa atulie na ndoa yake jamani,mbona nyama ni ileile buchani? Kama mpishi hajui mapishi tujaribu kuingia pamoja jikoni tuelekezane na hatimae tutapata kitu tunachokitaka.

Watulie/tutulie lakini kila abiria achunge mzigo wake. Always listen to your heart. Ukihisi jambo chafu linatendeka, hata ukiwa ndotoni basi lifanyie kazi. Hakuna njia ya mkato.
 
Kila kukicha mambo yanaongezeka ..ila huyu mwanaume ana roho mbaya na ngumu kama Israel mtoa roho.Huyo dada amwambie tu ameshamsamehe na dada wa watu aendelee na 50 zake hakuna penzi hapo zaidi ya utaperi

very true FirstLady1 the guy is shameless, yaani wanaume wengine wanakuaga na akili za kishetani,sijui vipi aisee. M2 anakuaminisha kuwa anakupenda, at the end of the day anakugeuka inauma sana. kuweni na huruma wanaume lol!!
 
Ni kweli hili suala ni baya sana na linadhihirisha kuwa watu wanawaumiza wenzao kwa kiasi ambacho ni kigumu kuamini. Huyu jamaa hastahili msamaha wa aina yoyote. Hata hivyo ni muhimu kujadili hili suala kwa mtazamo wa jumla (tukiangalia pande zote mbili). Tunalaumu wanaume kwa kosa hili alotenda huyu bwana ila kuna wanaume wengi sana ambao pia wametelekezwa na wake/wachumba au marafiki zao.
 
Ni hivi kulikuwa na mtu kaka na kaka mmoja ana girl friend wake kwa muda mrefu na kila mtu alikuwa huru kwa mwenzake na hata mmoja wapo akiwa na shida husaidiana sababu wote ni wafanyakazi.

Nimependa hgeading ya hii thread. Kwenye hiyo story inaonekana wote wawili hawakuwa wawazi kwenye hayo mahusiano. Kuwa GF au BF, sio sawa na uchumba. So ni vema kama mpo kwenye mahusiaono ya namna hiyo mkaelezana mapema kabisa matumaini na matarajio ya kila mmoja. Huyo dada inaelekea alivyoona 'anapendwa' hakujali kumuuliza huyo kaka tena hayo 'mapenzi' yataishia wapi. Laiti angeliumuuliza na wakazungumza pengine anagejua mapema zaidi kuwa huyo kaka hakusudii kumwoa.
 
Kweli mkuu, ukimya nao ni tatizo. Ila wakina dada wengine wanaogopa kuonekana wanalazimisha ndoa. Hata hivyo ni muhimu kuvunja ukimya na kuongelea hatima ya ushiano walau mara moja kwa mwezi! Hata hivyo diplomasia (ya kuzaliwa nayo) inahitajika sana. Inabidi watu wawe mbayu wayu wakati wote!
 
Back
Top Bottom