Jamani tuambieni kuhusu pasaka

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
17,336
21,435
amani iwe kwenu

Nina imani kila mwenye imani ya kikristo ameshakwenda kanisani na kukamilisha ibada yake maalumu ya siku ya pasaka

Na sasa ni muda maalumu wa kurudi nyumbani kungonja maandalizi ya mahanjumati na wengine wakianza na kilauri mapema kujichangamsha

Nakumbuka kipindi chetu cha udogo kuna jirani yetu mmoja alikuwa akirudi tu kanisani, huweka muziki kwenye redio yake kubwa aliyoipata huko sheli sheli walipokwenda kulinda amani ,wakati huo sisi muda huu tukiosha gari tayari kwa maandalizi ya jioni kwenda kutembezwa ndani ya land rover 109 ,hali ya uchumi kipindi kile ilikuwa nzuri sana.

Vipi leo hii jamani mbuzi wamechinjwa ,kreti za soda na bia zimenunuliwa mbona sisikii zile harufu za kipindi kile au watu wanakwenda kula mahotelini!

tuchangie pasaka yetu tunavyoisherekea kipindi hiki!
 
OK subiri utakaribishwa baadae kwasasa uchumi wa kifamilia umeyumba kidogo.
 
Ninakumbuka Tanzania ile ya awamu ya kwanza, Christmas mdingi lazima achukue likizo na wote tulikutana, pilau tulikuwa na watoto wote wa mtaani na soda juu. Iddi pia tuliletewa sinia la pilau limefunikwa na kawa na kibakuli cha visheti. Those were the days.
 
Hivi sasa gawapi mashii kila kitu kimekwenda!
 
Dah hivi sasa watoto wangu pia wamesema baba usiangake tukodishie cd tuangalie maana tunamjua dereva wa lori,enzi zetu saa hii tunajitayarisha kwenda kupanda punda!
 
Ofcourse mylove navile unavopenda nimeandaa special for you Smart911 wangu
Unajua sana kupika love... Achilia uzuri ulionao, hata jikoni upo vizuri sana... Pilau lipo safi, kachumari nzuri. Juice safi, kuku mtamu balaah...

Na napenda ulivyonivalia... Yani baada ya maankuli, nije nikukule na wewe...

Mh tena kuna watu wanakula nyama za watu!
 
Unajua sana kupika love... Achilia uzuri ulionao, hata jikoni upo vizuri sana... Pilau lipo safi, kachumari nzuri. Juice safi, kuku mtamu balaah...

Na napenda ulivyonivalia... Yani baada ya maankuli, nije nikukule na wewe...

Asante mylove Smart911
Mimi nipo kwa ajili yako tu Smart911 wangu
Muda na saa yoyote ukinihitaji nichukue mzima mzima
 
Back
Top Bottom