Jamani polisi nisaidieni na tapeli huyu

Jamani polisi nisaidieni na tapeli huyu

Mwisaki

Senior Member
Joined
Mar 9, 2014
Posts
168
Reaction score
56
Mimi ni mkaazi wa DAR nipo katka kutafuta maisha tu hii leo nimetapeliwa kiasi cha 500,000 hivi kupitia nambar 0657346184 na 0754594923 anatambulika kama KESHEN NYAKUNGA hupatikana sana iringa na moro, jina lake la utapeli hutumia "afande nasoro"huyu mtu ana sare za jesh la polisi kuanzia buti mpaka kofia anacho kifanya ni kujenga urafiki na wazazi wako wakati we mwenyewe hujui ndivyo alivyo tumia kututapeli kwa kusema nimemtafutia mwanao nafasi ya jeshi mf,jwtz,magereza au polisi hivyo huchkua nakala za vyeti na kuanza mchakato wa utapeli bila wewe kujua. kutokana na umasikini wetu hapo pross huanza kupitia kwa wazazi na mtoto. ikumbukwe anatumia sare za polisi alhali si polisi ktka kufanikisha malengo yake mimi yamenikuta kwani anaingia mpaka ofisi husika pindi anapo kamilisha mambo yake na kutumia vyeo bandia wakati wa kuwasiliana na namba zake ziho zinaita mpaka sasa na anaongea na mtu ambaye namba zake ni ngeni mimi namba zangu ni 0 naombeni
 
Pole mkuu, laki tano, yaani mshahara wa graduate kwa mwezi. Lakini hebu fafanua hiyo laki tano umemtumia mwenyewe au wamempa wazazi wako?
 
Daaah, shortcut zinawaumiza wengi!!

Pole sana mkuu inaelekea jamaa ni gwiji katika tasnia hii ya utapeli katika kuwatafutia watu nafasi za jeshi,.

Tshs 500,000/- si haba!!
 
Pole mkuu, laki tano, yaani mshahara wa graduate kwa mwezi. Lakini hebu fafanua hiyo laki tano umemtumia mwenyewe au wamempa wazazi wako?

nimemtumia mwenyewe kwani wazee hawana uwezo huo ishu ilikuwa nipate kazi
 
mnapenda sana shortcut ndo mana ni rahisi kupigwa kitakomwa na boya kama huyo...wa tz hatupendi kufanya reasoning kabisa juu ya mambo mbali mbali tuyafanyayo.
 
Pole,huna kazi umetuma 500,000/=ukipata kazi mkuu si utatumia fedha nyingi sana kupata vyeo.
 
Kwanza unakesi ya kutoa rushwa kwenye taasi za ulinzi ili upate ajira je ungefanikiwa ungezirudisha hela zako kama sio kuja kuwa mla rushwa mkubwa? Ndio ukome.
 
jamani jenga picha ndo umedhulumiwa wewe jamani naombeni msada wnu bandugu
 
jamani jenga picha ndo umedhulumiwa wewe jamani naombeni msada wnu bandugu
hIYO SIO DHULUMA NI UMEPIGWA MAANA HATA WEWE ULIKUSUDIA KUDHULUMU HAKI ZA WATU WENGINE IN CASE DEAL LINGEKUBALI, KESI HIYO HUWA TUNAKUBALI MATOKEO NA KUAMBULIWA KUPATA FUNZO WHICH IS GOOD FOR FUTURE
Hapo kuna kesi tatu na zaidi za kujibu, kwanza wewe kujihusisha na rushwa alafu na huyo jamaa kujipatia kipato kwa njia ya udanganyifu plus kujifanya mtumishi wa serikali wakati si kweli. Kwa maana nyingine kwa kuwa mlishirikiana nae kupita njia za panya ili mdogo wako apate ajira maana yake wote kwa pamoja mmetenda kosa (assuming jamaa angekuwa ni askari kweli na mdogo wako angepata nafasi). Kwa maana hiyo kama mchakato ulikuwa si wa haki (rushwa) inabidi uachane na kumshitaki huyo jamaa kwa kuwa mwisho wa siku atakubana mbavu mahakamani na wewe ulishasema ilikuwa rushwa ili amchague mdogo wako. Ingekuwa jamaa amejifanya anauza shamba alafu akakuuzia shamba fake la mtu mwingine hapo sawa (kesi kama yako huwa haipelekwi polisi huwa mnamtafuta kwa juhudi zako na kama ni mjanja wa mjini una m-tight kwa taratibu nyingine kabisa lazima atatoa)
UKIONA MTU HUMJUI ALAFU ANAJIFANYA MWEMA KAA NAE MBALI MKUU HAKUNA SHORT CUT KATIKA MAISHA
 
Kwanza unakesi ya kutoa rushwa kwenye taasi za ulinzi ili upate ajira je ungefanikiwa ungezirudisha hela zako kama sio kuja kuwa mla rushwa mkubwa? Ndio ukome.

kaka kutapeliwa hakuna mwenyewe mi nnauchungu we unanidhihaki poa bhana
 
jamani jenga picha ndo umedhulumiwa wewe jamani naombeni msada wnu bandugu

upi sasa,
1:tukuchangie?
2:tukataarifu polisi?
3:tukusaidie kumtafuta?
4:tumpigie simu tumchimbe mkwara arudishe fedha.
NB: Wanasema mjini shule ila wewe bado huja qualify
 
Leo mmewaamkia matapeli......
We mwenyewe ndio mwenye kosa tapeli hana kosa hata kidogo yeye anatumia udhaifu wako zaidi, once ukijifunza ku contain tamaa zako na pupa unaweza hata kuoa tapeli haki
 
Sasa kama unaweza pata laki 5, ulichonga upate I polisi au JWTZ hii ina maana tayari unakipato?.hapa dot haziconnet otherwise wazee wako ndio wametoa hiyo hela


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
ucje tena ukatoa hela b4 hujapata kaz. Pole tatfta kaz ingne kk
 
Back
Top Bottom