Zinduna
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 2,378
- 3,379
Niko Jijini Dar, tangu juzi, nimekuja kula Krismas, lakini jana nikajisikia vibaya kwani mwili ulikuwa unani-Washawasha. Nikajisemea moyoni, balaa gani hili yarabila-alamina! Nkaona nende kwa Dr. Riwa ili kupata matibabu. Kufika pale akanpima akanambia nina hitilafu kwenye Kongosho kutokana na kuugua Malaria Sugu hivyo akaniandikia Klorokwini. Nikawasiliana na Da' RussianRoulette kumweleza hali yangu, na yeye akawajuza wana JF.
Watu wa kwanza kuja kuniona walikuwa Dena Amsi na Da' AshaDii, walikuwa amenibebea uji lakini ulikuwa na ma-Bujibuji, hata sikuupenda, Pia walinipa salaam kutoka kwa Da' FaizaFoxy. Mara ghafla akaja shoga angu Mwali, akanambia Nyumba Kubwa ninayoishi itakuwa na Mbu wengi sana na akanionya niache Mcharuko nitumie Chandarua chenye kutiwa dawa. Hata hivyo alikuwa amenibebea Chauro ili nitulize njaa, Nili-Smile kwa furaha wakati napokea zawadi zile.
Lakini pia wapo walionitumia salaam za pole kupitia simu yangu ya BalckBerry, mfano Shostito Cantalisa ambaye alikuwa pamoja na Bebii walinitumia salaama wakinitaka ni-Badili Tabia na kuwa Mwanajamiione wa kutunza mazingira ili kuepuka maradhi, walinishauri niwasiliane na The Boss mshauri wa mazingira na afya kwa ajili ya kupata msaada wa kitaalamu juu ya utunzaji wa mazingira na uangamizaji wa mazalia ya Mbu. Nilipowasiliana na The Boss aliniambia yuko kikazi Mkoani Katavi na akaniahidi kumtuma Rejao ambaye yuko Moshi kwenye matambiko atakapo rudi awasiliane na mimi.
Daudi Mchambuzi hakubaki nyuma alinitumia salaam akinitaka niwasiliane na Saint Ivuga au Mti Mkavu kwani wao ni wataalamu wa tiba mbadala, kwani wanaweza kunipa ushauri. MAMMAMIA naye hakubaki nyuma alikuja kuniona na alikuwa na kadi za Get Well Soon kutoka kwa Sabry001, Da' Lizzy, Da'Aminata9 na Preta.
Napenda kuwashukuru wote mlioguswa na longo longo yangu na ningependa kuwatakia Sikukuu njema ya Krismas na Mwaka Mpya……………………………..
Wenu katika ujenzi wa JF