Jamani nimetapeliwa

Mbona umeibiwa kirahisi sana, mnapaswa kushirikisha watu wa karibu unapoona jambo ambalo halipo sawa. Sio kufanya maamuzi kimya kimya.
 
Kwa jinsi utapeli ulivyotamalaki usishangae hao wadada watatu unaowasema ndiyo wamemtapeli huo jamaa yako kwa kusingizia kwamba wametapeliwa na hivyo kujifanya kuomba msaada kwake!
 
unapungukiwa sifa za kuwa member wa JF,unapeliwaje kishamba pa1 na kupata exposure humu JF
 
Kwa jinsi utapeli ulivyotamalaki usishangae hao wadada watatu unaowasema ndiyo wamemtapeli huo jamaa yako kwa kusingizia kwamba wametapeliwa na hivyo kujifanya kuomba msaada kwake!
Nakuhakikishia walitapeliwa, na wao sio wa kwanza.
Hali ni mbaya sana kwa sasa.
 
Kamanda yaani ukishasikia mtu anakwambia mambo ya UN ujue ni utapeli . UN haifanyi kazi hivyo na pia issue ya mizigo hutanguliwa na documents za mzigo na si vinginevyo . Nakupongeza kwa ujasiri wa kusema ukweli na kukubali kukosea .Next time ukipata issue kama hiyo tafuta ushauri kwa mamlaka husika .
hapo ndo sikuwa makini nilitakiwa nijiridhishe kwanza haswa kwa mtu ambaye simjui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama unaishi dunia ya 3 wewe bado ni mgeni wakila kitu maana huko dunia ya 1utapeli huu n levek ya chini sana
Dunia ya sasa unatapeliwa kijinga hivyo?

U need a time to learn about this world unaonekana umgeni wa dunia ya sasa hata washauri huna..
 
Mwanangu Kangungo,

Alipata dili la kupiga mpunga mrefu ndani ya 24 hours akafanya siri..

Na yeye Akazuliwa gharama za kufaulisha mzigo kedekede kama mtoa mada hapa.

Hela yenyewe ya kufaulisha mzigo alikuwa hana..

Ila kwa sbb dili lilimtoa mate, anaona kabisa ukwasi huu hapa tena within 24 hours.. 😂😂😂

Akasema usinitanie weeh..!

Akawachek wadau kadhaa fasta wamkopeshe kwa ahadi ya kuwapa riba ya maana..

Hata kama ni wewe, mtu anakuambia nikopeshe 100,000/= kesho nakurejeshea 130,000/= huwezi acha..

Akakusanya M kadhaa..!! 😂

Kesho Ilipofika Kangungo macho yalimtoka jaman..

Ninavyozungumza sasa hivi, Kangungo boom lake likitoka analifwd kulipa deni..!

Alikuja kuniambia maji yalishamfika shingoni..

Nakubaliana na ushauri wa kutofanya siri.

Pole sana Mtoa mada.
 
Matapeli yamegundua dawa ni kujifanya wazungu ilihali ni vijana wa Tz au Kenya
 
Pole mkuu mtakubaliana na mm , kwa sasa mm niliekataa...kabisa !! Kuhusu kuamin ...mawasiliano na mtu nisiyemjua !! Halafu eti akufadhili kirahic tu hiyo haipo

sent from toyota Allex
 
Yaani wabongo mkisikia mzungu basi mnajua ela ipo aseeh..

Imeisha hiyo mkuu
 

hiyo namba na simu usajili pia .....kuna mengi utawapata tz polisi watakusaidia cyber


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuna mmoja alitaka kunipiga nilichomwambia ngoja niwasiliane na Interpool hata alipoishia sijui.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…