Jamani nimeamua kuokoka

Jamani nimeamua kuokoka

siyo ikibidi...walio okoka hawana mambo ya nyuma ya pazia...wako wazi!!badili ID na uweke picha yako...

Tayari yuko wazi,unafikiri kuja hapa barazani na kumtangaza Kristo live sio mchezo, huoni kuwa jamaa ameshaanza kazi ya kuchapa injili hapa jamvini?

Watu wanamaliza pages kusoma huu uzi kwa sababu Yesu ametajwa hapa. Mkuu kama umeokoka kweli, usirudi nyuma, chapa lapa, mbele kwa mbele.

Injili popote, hata jf uwe unatupia tupia kiaina kama ulivyofanya leo.
 
Tayari yuko wazi,unafikiri kuja hapa barazani na kumtangaza Kristo live sio mchezo, huoni kuwa jamaa ameshaanza kazi ya kuchapa injili hapa jamvini?

Watu wanamaliza pages kusoma huu uzi kwa sababu Yesu ametajwa hapa. Mkuu kama umeokoka kweli, usirudi nyuma, chapa lapa, mbele kwa mbele.

Injili popote, hata jf uwe unatupia tupia kiaina kama ulivyofanya leo.
tunataka tumtambue pia kwa matendo yake...si kwa kile akisemacho tu!
 
Kwa hiyo kile alichosema umepokea?
nina mashaka na anacho kisema...kwa nini anasema akiwa kajificha...biblia takatifu inaonya kuhusu wanao muonea aibu...naye atawaonea aibu mbele za baba yake...
 
nina mashaka na anacho kisema...kwa nini anasema akiwa kajificha...biblia takatifu inaonya kuhusu wanao muonea aibu...naye atawaonea aibu mbele za baba yake...

Hajajificha, ila njia aliyotumia kufikisha ujumbe ni sawa na mazingira tuliyomzoea, yaani ya kutumia ID feki. Je angetangaza jambo la hatari la kweli kwa ID feki ungesema ni uongo? Cha msingi hapa, tumshauri, kama amemkataa shetani, basi asajiri upya ID yake ili yale yote yaliyokuwa na ID feki yasimfuate fuate, na huko ndiko kuzaliwa upya.

Amefanya vizuri kutangaza kwa kutumia ID yake ya zamani ili wadau wajue kwamba mwenzetu nuru imemwangazia na sasa ni kiumbe kipya ndani ya YESU KRISTO, ila kama ataendelea kutumia ID feki mpaka kesho, basi tujue tatizo lipo.
 
Kwani ulikuwa hujui.

Bado haujathibisha kuwa allah ni Mungu.

Yesu alipokufa siku 3 Dunia ialimuachia nani !? Ishmael ?
'Zitadhalilika nyuso (za makafiri) mbele ya Aliye Hai Milele ! Mwangalizi Mkuu. Na atakuwa ameharibikiwa (kafiri) mwenye kubeba dhulma.
Qur'an: 20:111
 
Last edited by a moderator:
Yesu alipokufa siku 3 Dunia ialimuachia nani !? Ishmael ?
'Zitadhalilika nyuso (za makafiri) mbele ya Aliye Hai Milele ! Mwangalizi Mkuu. Na atakuwa ameharibikiwa (kafiri) mwenye kubeba dhulma.
Qur'an: 20:111
Kwani sasa hivi dunia kamuachia nani?
 
Mwaka 2014 nilipita katika misukosuko mingi ikiwemo kukoswa koswa kuuwawa mara kadhaa.. hata hivyo ni Mungu ndie aliyekuwa akinilinda kwa makusudi yake ili nimtumikie na kuwapeleka watu wengi kwa Yesu kupitia kazi yangu.. hivyo jana tar 1/1/2015 nimeamua kumpa Bwana Yesu kuwa mokozi wa maisha yangu.. najisikia amani sana na hofu yote imekwisha..
Mungu awabariki wana JF wote,
happy new year.
Mungu akubariki sana Ndugu. Karibu katika Maisha ya Ushindi na yenye uhakika baada ya kifo.

Kwa wale wanao taka kuokoka unakaribishwa sana.
 
JE UNATAKA KUOKOKA LEO?
Nini maana ya wokovu?
Inawezekana una maswali kama haya ndani ya moyo wako. Nini maana ya kuokoka? Au wokovu maana yake nini? Na ninawezaje kuokoka nikiwa hapa duniani? au ni kwanini niokolewe? Au nitaokolewaje? Swali lingine ambalo inawezekana unalo ni hili nikiisha kuokoka nifanye nini au nitaishije nikiwa hapa duniani?


Nimekutana na watu wengi sana wanaposikia habari hii ya kuokoka, wamekuwa na maswali kama haya mioyoni mwao, na nilipokupa wewe hii nafasi ya kukoka ninajua kuwa utakuwa na maswali kama haya moyoni mwako, ndio maana nimeamua kukujulisha kwa ufupi maana ya wokovu, na ni kwa nini unatakiwa uokoke na ukiisha kuokoka unapaswa uishije nimemwomba Roho Mtakatifu anisaidie kukiachilia kwa ufupi kile alichokiweka moyoni mwangu kinacho kuhusu habari za wokovu. Tafadhali Gonga Hapa kwa habari kamili juu ya wokovu. Baada ya kuokoka unahitaji msaada wa mafundisho juu ya wokovu.


Nini cha kufanya?
Inawezekana sasa una swali kama hili moyoni mwako, nifanye nini ili niokoke? Swali hili limewahi kuulizwa na watu wengi miongoni mwao ni huyu askari, alimuuliza Mtume Paulo afanye nini ili apate kuokoka, "Kisha akawaleta nje akasema, Bwana Wangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako" (Matendo 16:30-31). Ili leo hii uokolewe unapaswa Umwamini Bwana Yesu, swali umwamini kama nani? Unatakiwi umwamini kama Bwana na mwokozi wako, sikiliza, unaweza kabisa ukawa na imani kwa Yesu kama Mfalme, kama nabii, nk, lakini ukawa hauna imani kuwa Yesu ndiye mwokozi wako, pia unaweza ukawa na imani kuwa Yesu ni mwokozi, lakini ni mwokozi wa watu wengine, wewe bado haujampokea kama mwokozi wako, fahamu unatakiwa umpokee wewe kama mwokozi wako kwa kumuamini kuwa alikuja kwa ajiri yako, tunaupokea wokovu huo kwa njia hiyo ya imani. Imani maana yake ni kuwa na hakika na jambo lile unalolitalajia ambalo halijaonekana kwa macho haya ya nyama "Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana" (EBR 11:1) na imani huja kwa kusikia neno la Kristo "Basi imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo." (WARUMI 10:17).


Neno la Kristo lina sema wazi kuwa ukimwamini Bwana Yesu utaokoka, Amini leo, kuwa Yesu Kristo ndiye mwokozi wa maisha yako, utakapo amini na kuamua kukipokea hicho ulicho amini fahamu, leo hii Yesu Kristo atavunja kiambaza kile kilichokuwa kimewatenganisha au kwa lugha nzuri kifo, kifo hicho ninachokizungumzia ni kile cha rohoni, amini atakuja kwako sikia anavyo sema "Tazama nasimama mlangoni nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango,nitaingia kwake,nami nitakula pamoja naye,na yeye pamoja nami." (UFU 3:20)


Ukiamini au ukiwa na uakika wa maneno haya na unaamua kuufungua mlango yaani kukubari kumluhusu aingie ndani yako fahamu ataingia,na utakuwa na ushirika naye kabisaa, Je! Upo tayari Kuokoka leo hii? Kama upo tayari basi fanya hivi, tafuta pahali patulivu kisha ikiwezekana piga magoti, tafakari kisha sali sala ya toba ifuatayo kwa sauti


SALA YA TOBA
"Ee Mungu wangu ulie Mtakatifu. Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu. Ninatubu kweli. Naomba damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi yangu na mwili wangu. Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho wako – uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Ahsante kwa kunisamehe na kwa kuniokoa. Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina."


Ikiwa umesoma sala hii kwa kukusudia kabisa na kwa imani, basi wewe umeokoka na dhambi zako zimesamehewa na kusahauliwa na Mungu sawasawa na alivyoandika katika neno lake. Damu ya Yesu iko juu yako sasa. Hongera kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako.


Maisha baada ya kuokoka...
Ndugu yangu baada ya kuokoka tu, kuna swali na amini liko ndani ya moyo wako, unajiuliza, sasa leo hii nimeokoka nifanyenini sasa? Ni kweli ikiwa umeokoka kuna mambo muhimu ambayo unatakiwa uanze kuyafanya, yapo mambo mengi sana,lakini ebu nikupe haya mambo ya msingi ambayo unapaswa kuyafanya.
 
(alipokuwa anakata roho pale msalabani akatamka )..........Baba mikononi mwako naiweka roho yangu ! :A S wink:
Haujajibu swali.

1. Yesu kamuachia nani hii dunia?
2. Zaidi ya hapo, leo umeikana Quran na kukubaliana na Biblia kuwa Yesu alikufa Msalabani.
3. Vilevile, leo umekubalia kuwa Yesu ana Baba na kuipinga Quran yako inayosema kuwa Yesu hana Baba.

KARIBU KWA YESU NDUGU, maana sasa umesha elewa kuwa Yesu alikufa, na anaye Baba na ndie Mukulu wa Wakulu wote.
 
Haujajibu swali.

1. Yesu kamuachia nani hii dunia?
2. Zaidi ya hapo, leo umeikana Quran na kukubaliana na Biblia kuwa Yesu alikufa Msalabani.
3. Vilevile, leo umekubalia kuwa Yesu ana Baba na kuipinga Quran yako inayosema kuwa Yesu hana Baba.

KARIBU KWA YESU NDUGU, maana sasa umesha elewa kuwa Yesu alikufa, na anaye Baba na ndie Mukulu wa Wakulu wote.

Ameeeeen!!
 
Ongera kwa kuokoka.Upendo wa YESU na neema yake iihifadhi moyo wako mpaka kuja kwake YESU
 
stress zimeisha ndugu tangu jana... maana hakuna hukumu ya dhambi kwa hao waaminio karibu na wewe.

H
Mmh...
Davie na luse....wapya.! Ngojeni tuone .labda ndo mwanzo wa kuanzisha dhehebu jipya....
.
 
You have made a very wise decision.

Kuchagua njia ya kwenda mbinguni kwenye uzima wa milele, na kuepuka kwenda jehanum kwenye lile ziwa la moto.

Congratulations to you.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom