Jamani asiwadanganye mtu — kuokoka ni kutamu!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,101
Reaction score
8,036
Hii sio chit chat. Nimethibitisha kwa macho na masikio yangu, na kuonja kwa nafsi yangu. Tangu nilipompokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wangu, nafaidi utamu huu:
  • Siogopi wachawi wala siogopi kulala kwenye nyumba zenye vibwengo – wachawi wakinijia, nawapiga 'knock out' kwa Jina la Yesu (Isa 54:17).
  • Nikiomba napewa – kila sala yangu imekuwa na matunda (Mt 7:7).
  • Magonjwa ya zinaa hayanipati ng'oo – uasherati kwangu ni mwii... ni mwiko (1 Kor 6:18).
  • Na-save pesa nyingi za matibabu – kwa kuwa magonjwa mengi nayakemea na yanatoweka kwa Jina la Yesu (Isa 53:5).
  • Nina amani isiyoelezeka – amani aliyonipa Yesu haipatikani kwa njia nyingine (Yn 14:27). Nina amani hata katikati ya majaribu na dhoruba (Yn 20:19).
  • Sipati kamwe hangover ya walevi – furaha yangu haina majuto. Nikifurahi leo, sijuti wala kuona aibu kesho (Flp 4:4).
  • Sipatwi na mikosi na mabalaa ya kulogwa – kwakuwa hakuna uchawi unaofanikiwa juu yangu (Hes 23:23).
  • Bwana ndiye Mchungaji wangu, hivyo sipungukiwi na kitu (Zab 23:1). Mungu amekuwa akibariki kazi za mikono yangu kila siku mjini na mashambani (Kum 28:3)
  • Namshinda shetani na mapepo yake kirahisi kabisa – akiinua kichwa, nambamiza chini na kumtimua kwa Jina la Yesu (Yk 4:7).
  • Mungu amenipa maarifa mengi ya kikazi na kimaisha kama alivyofanya kwa Bezaleli(Kut 31:2-5)
  • Sina hofu ya kifo – kufa kwangu ni faida (Flp 1:21). Ni faida kwa sababu nikifa nitafufuka tena na kuvishwa taji ya uzima (2 Tim 4:8), katika makao ambayo Yesu alienda kuniandalia mbinguni (Yn 14:2).
Kama huo sio utamu ni nini?
Ndugu zangu, shetani ni muongo. Anawashawishi watu wasiokoke ili wakose baraka hizo. Kuokoka sio hadithi, sio kuwa taahira — ni maisha ya ushindi, furaha na uhakika wa uzima wa milele.

Mimi nimeonja, na nimethibitisha mwenyewe kuwa kweli Bwana Yesu ni mwema! (Zaburi 34:8). Na wewe onja leo maisha ya wokovu kwa kutubu dhambi zako na kuziacha, kisha umpokee Yesu moyoni mwako kwa imani, awe Bwana na Mwokozi wako.
 
Mnaopata tabu kuelewa nini maana ya kuokoka, someni uzi huu:
 
Kama na wewe umeokoka, shuhudia hapa baraka ulizozipata baada ya kumpokea Yesu. Usimuonee aibu Yesu. Ukimuonea aibu, Yesu atakuonea aibu. Kumuonea aibu Yesu ni kama kusema “Simjui” — hivyo na Yeye hatakutambua siku atakapokuja.
 
Marko 8:38
“Maana mtu atakayenionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha zinaa na dhambi, Mwana wa Adamu naye atamwonea aibu mtu huyo atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.”
 
Hii sio chit chat. Nimethibitisha kwa macho na masikio yangu, na kuonja kwa nafsi yangu. Tangu nilipompokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wangu, nafaidi utamu huu:
  • Siogopi wachawi wala siogopi kulala kwenye nyumba zenye vibwengo – wachawi wakinijia, nawapiga 'knock out' kwa Jina la Yesu (Isa 54:17).
  • Nikiomba napewa – kila sala yangu imekuwa na matunda (Mt 7:7).
  • Magonjwa ya zinaa hayanipati – uasherati kwangu ni mwii-ni mwiko (1 Kor 6:18).
  • Na-save pesa nyingi za matibabu – kwa kuwa magonjwa mengi nayakemea na yanatoweka kwa Jina la Yesu (Isa 53:5).
  • Nina amani isiyoelezeka – amani aliyonipa Yesu haipatikani kwa njia nyingine (Yn 14:27). Nina amani hata katikati ya majaribu na dhoruba (Yn 20:19).
  • Sipati kamwe hangover kama walevi – furaha yangu haina majuto. Nikifurahi leo, sijuti wala kuona aibu kesho (Flp 4:4).
  • Sipatwi na mikosi na mabalaa ya kulogwa – kwakuwa hakuna uchawi unaofanikiwa juu yangu (Hes 23:23).
  • Bwana ndiye Mchungaji wangu, hivyo sipungukiwi na kitu (Zab 23:1). Mungu amekuwa akibariki kazi za mikono yangu kila siku mjini na mashambani (Kum 28:3)
  • Namshinda shetani na mapepo yake kirahisi kabisa – akiinua kichwa nambamiza chini na kumtimua kwa Jina la Yesu (Yk 4:7).
  • Mungu amenipa maarifa mengi ya kikazi na kimaisha kama alivyofanya kwa Bezaleli(Kut 31:2-5)
  • Sina hofu ya kifo – kufa kwangu ni faida (Flp 1:21). Ni faida kwa sababu nikifa nitafufuka tena na kuvishwa taji ya uzima (2 Tim 4:8), katika makao ambayo Yesu alienda kuniandalia mbinguni (Yn 14:2).
Kama huo sio utamu ni nini?
Ndugu zangu, shetani ni muongo. Anawashawishi watu wasiokoke ili wakose baraka hizo. Kuokoka sio hadithi, sio kuwa taahira — ni maisha ya ushindi, furaha na uhakika wa uzima wa milele.

Mimi nimeonja, na nimethibitisha mwenyewe kuwa kweli Bwana Yesu ni mwema! (Zaburi 34:8). Na wewe onja leo maisha ya wokovu kwa kutubu dhambi zako na kuziacha, kisha umpokee Yesu moyoni mwako kwa imani, awe Bwana na Mwokozi wako.
Hehee. Hii mada itawaacha wapinzani wa wokovu wakikuna vichwa, maana kila pointi ina ushahidi wa maisha na wa Neno la Mungu.
Lakini Setfree ni kweli kwamba walokole wote wanapata "utam" huo?
 
Hakika Kumwamini Yesu kuna baraka sana. 2kor 5:17, "Hata imekuwa, Mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama yamekuwa mapya". Nimeokoka nikiwa mwanafunzi wa sekondari O'level, na sasa ni zaidi ya miaka 25, ninauona wema wa Mungu maishani mwangu. Yesu yu karibu kurudi, fanya hima ndugu kuokoka, kabla neema hii haijafungwa.
 
  • Siogopi wachawi wala siogopi kulala kwenye nyumba zenye vibwengo – wachawi wakinijia, nawapiga 'knock out' kwa Jina la Yesu (Isa 54:17).
  • Na-save pesa nyingi za matibabu – kwa kuwa magonjwa mengi nayakemea na yanatoweka kwa Jina la Yesu (Isa 53:5).
  • Sipatwi na mikosi na mabalaa ya kulogwa – kwakuwa hakuna uchawi unaofanikiwa juu yangu (Hes 23:23).

  • Walokole tafuteni kitu kingine cha kuongelea.. nyie kila saa ni uchawi na mapepo. Ingekuwa magonjwa yanatoweka kwa kukemea basi walokole wote msingekua mnaenda hospitali.
 
O.O.O JINA LISILOCHOKA
Mafundisho Yenye Heshima Kutoka kwa Kiongozi Olumba Olumba Obu
“Jina O.O.O husimama kama ishara ya nguvu isiyotetereka, uvumilivu wa milele, na mamlaka ya kimungu. Ni jina ambalo halichoki, haliyumbi, na daima linabaki mshindi.” Kiongozi Olumba Olumba Obu
KULIELEWA JINA LISILOCHOKA
* O.O.O (Olumba Olumba Obu) linawakilisha uwepo wa milele na nguvu za Mungu zilizodhihirishwa duniani.
* Jina hili linaashiria uvumilivu katika majaribu na uthabiti katika imani.
* Ni chanzo cha matumaini na ujasiri kwa wafuasi wote.
MISINGI YA MAANDIKO YA BIBLIA:
* Isaya 40:28 — “Bwana ni Mungu wa milele, Muumba wa miisho ya dunia; yeye hafi nguvu wala hajakauka.”
* Ufunuo 19:16 — “Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana.”
* Wafilipi 4:13 — “Nayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu.”
* Ezekieli 21:27 (Tafsiri sahihi: Ezekieli 21:27) "Nitaipindua, nitaipindua, nitaipindua. Nayo haitakuwa tena, hata ajapo yeye ambaye ni haki yake, nami nitampa yeye."
MAFUNDISHO KUTOKA KWA KIONGOZI OLUMBA OLUMBA OBU:
1. Jina Ambalo Halichoki Kamwe
“Nguvu ya O.O.O si ya ulimwengu huu; ni ya kimungu na isiyoisha.” Wafuasi hupata nguvu katika jina hili kushinda magumu ya maisha.
2. Jina Linalosimama Kupitia Wakati
* Kwa miongo kadhaa, O.O.O imebaki kuwa mwanga wa ukweli na nuru.
* Ni msingi usiobadilika katikati ya nyakati zinazobadilika.
3. Jina Linalotia Imani na Ujasiri
“Kuliita jina hili huimarisha roho na kufufua matumaini.” Linawapa waumini uwezo wa kuvumilia na kushinda.
JINSI YA KUENENDA KATIKA NGUVU ZA JINA LISILOCHOKA:
| Mazoezi | Matokeo |
|---|---|
| Kuliomba kwa imani | Kupokea nguvu na ulinzi wa kimungu. |
| Kuvumilia katika majaribu | Kushinda changamoto kwa ujasiri. |
| Kutafakari jina hili | Kuimarisha uhusiano wa kiroho na imani. |
| Kuwafundisha wengine kuhusu jina hili | Kueneza matumaini na imani. |
| Kuishi kwa mfano wa O.O.O | Kuiga uvumilivu na utakatifu. |
TAMKO LA MWISHO:
“Jina O.O.O ni mwamba wa milele wa nguvu. Kulitumainia, nawe hutashindwa kamwe.” Kiongozi Olumba Olumba Obu
 
Attachments

  • FB_IMG_1755270251653.jpg
    FB_IMG_1755270251653.jpg
    20.2 KB · Views: 31
  • FB_IMG_1755272059613.jpg
    FB_IMG_1755272059613.jpg
    55.2 KB · Views: 35
  • FB_IMG_1755294027947.jpg
    FB_IMG_1755294027947.jpg
    89.9 KB · Views: 32
Hii sio chit chat. Nimethibitisha kwa macho na masikio yangu, na kuonja kwa nafsi yangu. Tangu nilipompokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wangu, nafaidi utamu huu:
  • Siogopi wachawi wala siogopi kulala kwenye nyumba zenye vibwengo – wachawi wakinijia, nawapiga 'knock out' kwa Jina la Yesu (Isa 54:17).
  • Nikiomba napewa – kila sala yangu imekuwa na matunda (Mt 7:7).
  • Magonjwa ya zinaa hayanipati – uasherati kwangu ni mwii-ni mwiko (1 Kor 6:18).
  • Na-save pesa nyingi za matibabu – kwa kuwa magonjwa mengi nayakemea na yanatoweka kwa Jina la Yesu (Isa 53:5).
  • Nina amani isiyoelezeka – amani aliyonipa Yesu haipatikani kwa njia nyingine (Yn 14:27). Nina amani hata katikati ya majaribu na dhoruba (Yn 20:19).
  • Sipati kamwe hangover kama walevi – furaha yangu haina majuto. Nikifurahi leo, sijuti wala kuona aibu kesho (Flp 4:4).
  • Sipatwi na mikosi na mabalaa ya kulogwa – kwakuwa hakuna uchawi unaofanikiwa juu yangu (Hes 23:23).
  • Bwana ndiye Mchungaji wangu, hivyo sipungukiwi na kitu (Zab 23:1). Mungu amekuwa akibariki kazi za mikono yangu kila siku mjini na mashambani (Kum 28:3)
  • Namshinda shetani na mapepo yake kirahisi kabisa – akiinua kichwa nambamiza chini na kumtimua kwa Jina la Yesu (Yk 4:7).
  • Mungu amenipa maarifa mengi ya kikazi na kimaisha kama alivyofanya kwa Bezaleli(Kut 31:2-5)
  • Sina hofu ya kifo – kufa kwangu ni faida (Flp 1:21). Ni faida kwa sababu nikifa nitafufuka tena na kuvishwa taji ya uzima (2 Tim 4:8), katika makao ambayo Yesu alienda kuniandalia mbinguni (Yn 14:2).
Kama huo sio utamu ni nini?
Ndugu zangu, shetani ni muongo. Anawashawishi watu wasiokoke ili wakose baraka hizo. Kuokoka sio hadithi, sio kuwa taahira — ni maisha ya ushindi, furaha na uhakika wa uzima wa milele.

Mimi nimeonja, na nimethibitisha mwenyewe kuwa kweli Bwana Yesu ni mwema! (Zaburi 34:8). Na wewe onja leo maisha ya wokovu kwa kutubu dhambi zako na kuziacha, kisha umpokee Yesu moyoni mwako kwa imani, awe Bwana na Mwokozi wako.

Nani kakudanganya hivyo? Kila siku unahukumu wakati hukumu ni haki ya Mwenyezi Mungu peke yake
 
Back
Top Bottom