Jamani nifanye vipi nisimchukie?

Ongeza muda wa kusoma katika lesson preparation zako pia mengine jitahidi kumwachia Mungu na kumshukuru kwa kila jambo, huwezi kujua Mungu amekuepushia nini kwa huyo mwanamke.
Ahsante nashkuru sana ila pia rafiki zake huwa wananipigia simu nahisi nao wananiongezea chuki tu
 
HAHAHAHA DA NGOJA NIFANYE KAZI KWANZA
 
Ahsante nashkuru sana ila pia rafiki zake huwa wananipigia simu nahisi nao wananiongezea chuki tu
Tena hao watakufanya uzidi kuzunguka kwenye duara hilo, unahitaji kuvunja huo mnyororo, wakipiga kuwa makini kuwauliza wanataka nini? Ukiwa makini sana mtu anajitafakari kabla hajapiga simu.
 
Pole unapaswa kutendwa kama mara tatu then utakuwa perfect, chukulia hio kuwa ni test number 1, subir test nyingine 2. Then oa utakuwa vizuri tu.
Huwa najiuliza kuhusu hawa watu wanao ishi pamoja mpaka wana zeeka sijui huwa wana tumia mbinu gani kuishi na wanawake... Wazo la kuoa lime yeyuka kwa speed sana
 
Ninakumbuka once upo the time, nilimpenda kaka mmoja, sikudhani kama nitaweza kuishi bila yeye. Alipoamua kusitisha mahusiano nilisikia kabisa maumivu fizikia ya moyo sio hisia tu. Sasa hivi tunaongea kama watu tunaofahamiana na huwa ninacheka hivi huyu alinifanya niumie huyu.
 
Huwa najiuliza kuhusu hawa watu wanao ishi pamoja mpaka wana zeeka sijui huwa wana tumia mbinu gani kuishi na wanawake... Wazo la kuoa lime yeyuka kwa speed sana
Ukikutana na mtu sahihi mapenzi si kifungo, matatizo ni pale unapokutana na mtu ambae hamwendani ni mtihani wa maisha.
 
Mimi niliwahi kuamua kua kila nikijihisi nina hasira naenda kupiga gita na ni lazima nikapige.
Gita lilipo na ninapoishi ni mbali, halafu sijui vizuri hivyo hua naona "Dah natembea mpaka huku kisa gita ambalo siliwezi vizuri?" Njiani hua napima ishu zilizosababisha kilichotokea na hua naona nakua sawa.
Ugumu wa kulifuata na kulitumia gita umenifanya niwe mwangalifu katika maamuzi ili nisije kujikuta nimekasirika ghafla na kutakiwa kulifuata gita.
 
Tena hao watakufanya uzidi kuzunguka kwenye duara hilo, unahitaji kuvunja huo mnyororo, wakipiga kuwa makini kuwauliza wanataka nini? Ukiwa makini sana mtu anajitafakari kabla hajapiga simu.
Ni kweli kuna vimaneno huwa wanavileta mara ooh mtu wako likizo kaenda kwa mshikaji.. Natakiwa kweli kuwa mbali nao
 
I like this mkuu.
 
("Huwa tunasema "Chuoni njoo na akili zako tuu Tabia zote utazikuta chuoni")anonymous... "Tatizo mi bado nilipokosea kakosa sitambui? Mpaka kafunga virago na kaamua kuondoka sitambui...ila kinachoniuma maneno neno maneno[emoji36] [emoji445] "
_______________________________
Song-Ukimuona
 
Mwanaume kuumizwa na mwanamke ni uzembe. Haya maua yamejaa tele... hili likinyauka unachuma lile.

Ndo ujinga huu wa watu kujifanya wasafi. Mwanaume unapaswa uwe na mademu watatu angalau... Huyu akileta fyoko unakuwa tayari una back up.
Unaongea kirahisi rahisi kama wewe unao hao watatu.
 
Haaa haaaa mkuu hiyo style yako nimeipenda sana... Vip bado tu hujajua kupiga gita??
 
Ukikutana na mtu sahihi mapenzi si kifungo, matatizo ni pale unapokutana na mtu ambae hamwendani ni mtihani wa maisha.
Sasa huyo sahihi sijui ntamjuaje maana hata huyu mwanzo alinipenda sana.. Nlikuwa nashangaa kwanini watu wengine hawataki kuoa.. Sasa nahisi na mimi naelekea huko huko
 
Haaa haaaa mkuu hiyo style yako nimeipenda sana... Vip bado tu hujajua kupiga gita??
Hadi leo sijui na sidhani kama nitajua kwakua kulifuata ni mpaka nikasirike na nimekua sikasiriki so nipo nipo tu hata chords nishazisahau.
 
Hadi leo sijui na sidhani kama nitajua kwakua kulifuata ni mpaka nikasirike na nimekua sikasiriki so nipo nipo tu hata chords nishazisahau.
Chanzo cha hasira zako ni nini??
 
Haya matatizo bwana ni rahisi mtu kukwambia piga chini lakini ni wewe na moyo wako ndiyo unajua unaumia vipi. Time is the best healer.
asee kweli kabisa muda pekee ndio mponyaji. Haya mambo yanaumiza saana asikuambie mtu, ni rahisi kushauri usiombe yakukute. Mimi yalinikumba january 2014 nilikuchua mwaka kupona, ila mpaka leo moyo haujafunguka kupenda
 
Hili ndo Tatizo la kuanza mapenzi mwaka wa 3 chuo ,piga chini huyo demu asikuumize kichwa pia mademu walioko chuo wengi mizinguo sana tafuta WA mtaani tena mwenye shughuli zake achana na videmu vya chuo chuo bhana vitakupa stress tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…