Jamani mapenzi na chama wapi na wapi?

Jamani mapenzi na chama wapi na wapi?

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
1,353
Reaction score
2,851
Hii imemtokea rafiki yangu kipenzi, Jana aliniomba nimsindikize Lenana Hotel jioni akisema kuwa kuna binti kampenda sana sasa anataka amweleze intention yake ya kumuoa, mimi nikamsindikiza, kufika Lenana Hotel baada ya dakika kama 20 binti akafika, ukimwangalia kwa haraka haraka atakuwa na umri wa miaka 21-25 hivi, basi, tukasalimiana pale, mazungumzo ya kuchumbiana yakaanza, kilichonistua zaidi ni hili, katika kuulizana maswali ya hapa na pale mfano, unafanya kazi gani, umri wako, kwenu mpo wangapi, wazazi wako wapo, unasali dhehebu gani, nk. ndipo yule binti akauliza wewe ni chama gani? duuu!! ikabidi nimuwahi kwa kumuuliza swali, chama una maana gani? akasema, Chama cha siasa, Bahati nzuri yule rafiki yangu akasema hana chama ila ni mshabiki wa vyama tu! binti akasema yeye alitaka kufahamu tu!!

Sasa nauliza, hivi siku hizi mkichumbiana ni lazima hili swali umuulize mwenzio? na nafasi ya hili swali katika mahusiano ni ipi?
 
hahahaha binti ana akili sana lazima ujue mumeo ni chama gani maana ukianza kuleta sera za CCM wakati yeye ni CDM hapatakalika
 
Kuna umuhimu ili kufahamu upstairs mwenzio yukoje, si unawaona wenye chama wenzio walivyo kama wamemwazima mtu akili zao? Wao jambo lililo na manufaa kwa wananchi wao ndio wako against nalo
 
Hahahahah dah binti alikua anahofia asije kulamba magwanda,maana ni washari sana!
 
Hii imemtokea rafiki yangu kipenzi, Jana aliniomba nimsindikize Lenana Hotel jioni akisema kuwa kuna binti kampenda sana sasa anataka amweleze intention yake ya kumuoa, mimi nikamsindikiza, kufika Lenana Hotel baada ya dakika kama 20 binti akafika, ukimwangalia kwa haraka haraka atakuwa na umri wa miaka 21-25 hivi, basi, tukasalimiana pale, mazungumzo ya kuchumbiana yakaanza, kilichonistua zaidi ni hili, katika kuulizana maswali ya hapa na pale mfano, unafanya kazi gani, umri wako, kwenu mpo wangapi, wazazi wako wapo, unasali dhehebu gani, nk. ndipo yule binti akauliza wewe ni chama gani? duuu!! ikabidi nimuwahi kwa kumuuliza swali, chama una maana gani? akasema, Chama cha siasa, Bahati nzuri yule rafiki yangu akasema hana chama ila ni mshabiki wa vyama tu! binti akasema yeye alitaka kufahamu tu!!

Sasa nauliza, hivi siku hizi mkichumbiana ni lazima hili swali umuulize mwenzio? na nafasi ya hili swali katika mahusiano ni ipi?

acha uongo mkuu, ina maana ulikaa nao meza moja wakati wakit.ongozana?
 
Haa yan umeshangaa chama? Watu wanaulizana hadi timu za mpira eboh !!
 
Hilo swali la chama halijanishangaza,kilichonishangaza ni wewe kuwanyima wenzio uhuru wa kutongozana!!
 
acha uongo mkuu, ina maana ulikaa nao meza moja wakati wakit.ongozana?

Sio kutongozana mkuu, kuchumbiana, jamaa aliniambia nimsindikize, sasa wakati wanazungumza mimi nilikuwa na kinywaji changu najifanya kama vile sisikilizi kinachoendelea kumbe huku sikio moja liko pale kwao, na kumbuka katika issue ya kuchumbiana unaweza kumchukua rafiki au ndugu yako wa karibu ambaye hana tamaa akakusindikiza, hapa ni kuongeza nguvu tu mkuu.
 
....................................................................
 
Sio kutongozana mkuu, kuchumbiana, jamaa aliniambia nimsindikize, sasa wakati wanazungumza mimi nilikuwa na kinywaji changu najifanya kama vile sisikilizi kinachoendelea kumbe huku sikio moja liko pale kwao, na kumbuka katika issue ya kuchumbiana unaweza kumchukua rafiki au ndugu yako wa karibu ambaye hana tamaa akakusindikiza, hapa ni kuongeza nguvu tu mkuu.

Labda kwasababu ni mtoto wa miaka 21 mtu mzima kama mie uanze kunichumbia huku rafiki yako amekaa meza hiyo hiyo eti anakunywa kinywaji na kujifanya hatusikiliza wakati masikio hayana mlango kusema ameufunga asitusikie, aisee isingewezekana
 
shida ya huyo dada ni kuwa GONGO kwenye familia yao ni kharam,,,so alikuwa ana wasiwasi asije nyweshwa GONGO!!!!
 
Sio kutongozana mkuu, kuchumbiana, jamaa aliniambia nimsindikize, sasa wakati wanazungumza mimi nilikuwa na kinywaji changu najifanya kama vile sisikilizi kinachoendelea kumbe huku sikio moja liko pale kwao, na kumbuka katika issue ya kuchumbiana unaweza kumchukua rafiki au ndugu yako wa karibu ambaye hana tamaa akakusindikiza, hapa ni kuongeza nguvu tu mkuu.

kuchumbiana wakati hata umri hakuwa anaujua wala anafanya kazi gani, huo ulikuwa mtongozano
 
Sijaona kosa lako kukaa nao kalibu, kwani kipindi hiki watu wanachumbia na kutongozana mbele ya wazazi sembuse we,lafiki tu. Achana na washamba wanao tongezeana kwenye majumba mabovu.
 
Hapo walitoka out tu hakuna cha kuchumbiana hapo.

Maswali kama hayo mbona ya kawaida kabisa? Ni lazima muendane kwa kila kitu hata mavazi, chakula, elimu, sehemu za starehe nk. Sasa kama yeye ni njagu atakubali awe na mtu wa chama cha upinzani? Au kama atakubali ujue yuko kazini huyo. Kila akiamka anapeleka ripoti ofisini yaliyojiri kwenye chama fulani.
 
Back
Top Bottom