Jamani kulea mabinti ni kazi, kha!

na sisi wazazi tunachangia...

dawa ni kuwa karibu na watoto wao, wakuheshimu kama baba/mama lakini wakuone kama rafiki ambaye mnaweza keti na kutia story, ambaye akitatizwa anakufuata kukuomba ushauri /kukuuliza na unapoulizwa ujibu sio kuleta ukali

na kuzuia watoto wenu kuwa karibu na utandawazi hata kama umeenea kiasi gani, mtoto darasa la saba ana simu, tena yupo facebook anafanya nini huko? simu ya nini? kukiwa na simu ya tochi nyumbani ambayo inatumiwa na kila mtu unayoicontrol itakuwaje?

unazungumza na watoto wako wa kike na wakiume kuhusu mapenzi, madhara yake, maradhi nk?


vitoto vya siku sijui aisee,yanaingilia huku yanatokea kule.
 
kuna katoto niliona niwe mama ushauri wake katika maongezi nikamwambia ukifanya hayo mambo waweza pata mimba akaniambia wewe mimi sijawahi kulala na mwanaume yeyote bila kutumia mpira ,nilizimia mtoto wa miaka 12

haya sasa,at 12!
 
Kumbe huwa inauma Bishanga ehee...ulipokuwa unachezea watoto wa watu au ukiwa unapiga infidelity zako kaa ukijua kuwa na wewe wa kwako kuna jamaa wataanza kummendea soon...lol
umefurahiiiiiiiiii ndo mana kina Nitonye na Rejao wanakunyang'anya mabibi zako,lol,mwone kwanza!
halafu nimekumbuka ngoja nimPM SL nimfahamishe kuwe TF ndo kamuhonga PAW amlambe ban Nitty.
 
Siku hizi hamna unafuu..yani wote ni pasua kichwa.

Mwenye wa kike an hofu ya kuletewa kitumbo kilichotuna huku mwenye wa kiume ana hofu ya kuletewe "boifriend". Yani hamna kupumua mpaka wawe watu wazima na uone hayo yote yamekwepeka.

Huyo wako nenda nae taratibu maana sasa hivi ndio kile kipindi cha kukomoana na mzazi kwake...ukiongea sana kitu ambacho hajafanya basi anafanya...ukijifanya mnoko sana basi anafanya yale anayojua ukijua yatakukera sana hata kama sio anayotaka kufanya.Jitahidi kuongea na kureason nae...the more mnaelewana lugha the better.
Lizzy kwa mipweint bana utadhani alikuwa darasa moja na Oprah,ila sa ingine we nae ukali unazidi.Ahsante kwa ushauri.
 
We umeoa tayari umeshampa mimba bi harusi, mama umeolewa tayari mimba miezi 7, unataka mtoto azaliwe na tabia gani?, Watoto mnawazaa kwenye laana yenu msiwalaumu!, Vimba sana ila angalia usipasuke, ni matunda ya kazi yako!
mmmmmhhhhhh????
 
Na watoto wakike na wakiume lakini ukweli watoto wakike huwa hawasumbui sana kama mitoto ya kiume.

Yani hayo ma nunda nilio nayo kila siku naletewa mashitaka, afu mama yao anasema yamekufata :biggrin:
du! Pole mkuu!
 
Pole sana bishanga,ukali hapo hauna nafasi na wala hautasaidia,jitahidi kuwa rafiki wa karibu ili akuone km mshauri itakuwa rahisi kufuata kile unachomshauri au kumwambia,
Kwa umri huo hata umpige na kumjeruhi kamwe hutafanikiwa kumweka utakavo,

Mie nakumbuka baba alikuwa akinipenda na kuwa rafiki yangu kiasi kwamba kila alichonambia ndio nilifata mpaka mama akawa akitaka kunionya kitu anasema subiri baba yake akimwambia ndio anaelewa na hii ni kwa sababu mama alikua anaongea kwa fimbo na baba alitumia hekima na busara na nashukuru alifanikiwa kunilea vema mpaka nimekua mtu mzima.
Canta,kwa hiyo bakora sio muhimu kihivyo?
 
DC una mambo! Kwema lakini mkuu?

Mie mzima kanywanyi/kalumuna!!


Unajua, wezi ni waoga sana kwani wanahisi kuwa anytime wanaweza kuibiwa kama wanavyowaibia wenzao.

Punguza tu pressure, na ujitahidi kutumia kipimo kile kile ambacho umekuwa ukitumia kuwapimia watoto wa wenzio!!

Naamini unaweza kupunguza matatizo ya stroke kwa kukubaliana na hali,

Anyway...Mwosha naye huoshwa siku yake ikifika!!...I hope haijafika bado ila una insinuate!!


Babu DC!!
 
du! Pole mkuu!
Pole Bishanga, siku hizi hakuna mtoto wa kike na wa kiume, wote wamekuwa pasua kichwa, naongea hivyo vile nawaona wadogo zangu wawili walionifuata wanavyomsumbua mama angu, anasema mpaka anaishiwa nguvu, fujo zao, club yao, pombe zao, wanawake wakubwa kwa wadogo wote wao, hawasikii la muazin wala la mnadi swala! Wakitoka nyumbani sa moja jioni bila kufika sa8 au 9 usiku hawajarudi nyumbani, huezi amini anaenifuata mgongoni ana watoto wawili kwa wanawake wawili tofauti tena wana umri sawa na dadangu wa kwanza, na wote katupiwa mama analea.....

Mama alishajichokea kuongea, siku hizi amebaki kulia na Mungu kwamba mbona anasali sana watoto wake wabadilike lakini hawabadiliki.... Endelea kumwombea binti, atabadilika, usikate tamaa bado mapema sana!
 
Pole Bishanga, siku hizi hakuna mtoto wa kike na wa kiume, wote wamekuwa pasua kichwa, naongea hivyo vile nawaona wadogo zangu wawili walionifuata wanavyomsumbua mama angu, anasema mpaka anaishiwa nguvu, fujo zao, club yao, pombe zao, wanawake wakubwa kwa wadogo wote wao, hawasikii la muazin wala la mnadi swala! Wakitoka nyumbani sa moja jioni bila kufika sa8 au 9 usiku hawajarudi nyumbani, huezi amini anaenifuata mgongoni ana watoto wawili kwa wanawake wawili tofauti tena wana umri sawa na dadangu wa kwanza, na wote katupiwa mama analea.....

Mama alishajichokea kuongea, siku hizi amebaki kulia na Mungu kwamba mbona anasali sana watoto wake wabadilike lakini hawabadiliki.... Endelea kumwombea binti, atabadilika, usikate tamaa bado mapema sana!

Nina kabinti kadogo hapa nyumbani...hebu njoo ukafunde basi.
 
Canta,kwa hiyo bakora sio muhimu kihivyo?
Kwa mtu mzima km huyo wala usijichoshe!!!
Yani ndio atazizoea na mtaanza mchezo wa kukomoana tu!
Ongea naye tu na kubali kuwa rafiki yake yani atakuwa wazi kwako kwa kila jambo nawe utakua unajua kila linalomsibu na namna ya kumsaidia kwa ushauri na kwa upendo utako mwonyesha haenda kinyume na ushari wako!

Mie nilishawahi kumpelekea baba barua ya tongozo nikiwa std 6,akanishauri na kunielewesha namna ya kutokubali na hasara za kuanza hayo mambo nikiwa mdogo na akanishauri siku nyingine nimpelekee mama,nikamwonyesha na kale kajamaa akakaelewesha makosa yake na hasara ya lile ombi lake na kwenda kumweleza na mzazi wake!!
 
Inachanganya! Ukionyesha upendo sana kwa watoto wanadeka, ukiwa mkali wanakuogopa hivyo wataficha mambo yao! Yahitaji utulivu na busara kulea hawa watoto wapya.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom