Jamani kina dada mna nini jamani kuwataka shemeji zenu?

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,188
4,100
Wazima ,bila kupoteza muda ngoja niende kwenye mada

Na nyie kina dada acheni kusimulia mambo mazuri mnayofanyiwa na wapenzi wenu ona sasa yaliyomkuta ndugu wa rafiki yangu.

Iko hivi, rafiki yangu kanipa mkasa ambao umenigusa sana! Ana ndugu yake ambae aliku na mpenzi wake. Mapenzi kama yote, mahaba ya kihindi akawa anamsimulia rafiki yake kuhusu vinono anavyopewa na babe pia akawa anampa aongee naye kwa simu.

Hakujua kua yule rafiki alikua anatamani nayeye apate vile vitu alivyokua anapewa yeye. Basi akawa anajidai anamsapoti rafiki yake kumbe anatafuta namna ya kumpata shemeji yake.

Basi siku moja yule dada akaomba waende nae kwa shemeji yake bila wasiwasi akakubaliwa wakaenda wote walipofika kwa shemeji bi dada hakufanya kosa alihakikisha anachukua namba ya shemeji yake na ndio mchezo ulipoanzia.

Akaanza kuwasiliana na shemeji mapaka akapindua meza tena kwa kishindo kikuu! Ndugu wa rafiki yangu anakuja kushtuka anasikia rafiki yake anataka kuolewa na anaolewa na mpenzi wake.

Ushauri kama una rafiki yako usimwambie mazuri ya shemeji yake msimulie mabaya tu na kamwe usiwaweke karibu utaumia tu siku moja.
 
Umepata kichaka cha kujificha.. Ni mara ngapi mnachepuka na marafiki hata ndugu wa wapenzi/ wake zenu hata bila ya wao kusema chochote na wengine huna sifa yoyote anakuvumilia tu.. Duuh JF upotoshaji mtupu
 
Ss huoni kama hata mwanaume hana msimamo?! Ujasiri wa kumuoa rafiki ya aliekua mpenzi wako unautoa wapi kama sio dishi limeyumba
Bahati mbaya wanaume tuna madishi mawili (la juu & chini)
Bora liyumbe la juu utaokota makopo, likiyumba la chini analiwa hata kuku na mayai yake.

Haya mambo kwa sasa yamekua ya kawaida, kikubwa tumwombe Mungu atupe mioyo ya kutubu kweli na mwisho mwema.
 
hata kama ni wewe poa tuu...ila pole.....hata hayo mabaya utakayomwambia kwa mwenzio mazuri....MWANAUME ni yule yule....ALFA na OMEGA...
 
pole kwa yalomfika, pia pole kwa mleta uzi coz nawe umeplay part yako kwenye hili
 
wanaume wengine wanatafutaga tu kulogwa wawe machizi

hako kadada nako kanajikubalisha kabisa kanaolewa na mume wa rfk ake (kanguchiro kbsa)

mimi ningekua huyo mdada muibiwa mume

Ningeliaaaaa weeee Ningeliiaaaaaa weeee Ningeliiiaaaaa weeee kama FAIZA wa sugu

halafu nikimaliza kulia napenga makamasi pyeeeee then kesho yake

naenda zangu china kufata ma wiving ya wateja wangu.
 
Ahahahaha dah kama pesa ya china hakuna anaenda wapi
 
Bahati mbaya wanaume tuna madishi mawili (la juu & chini)
Bora liyumbe la juu utaokota makopo, likiyumba la chini analiwa hata kuku na mayai yake.

Haya mambo kwa sasa yamekua ya kawaida, kikubwa tumwombe Mungu atupe mioyo ya kutubu kweli na mwisho mwema.
huku Kolomije bado sio mambo ya kawaida. Labda yaletwe na hawa wanyama wa Burigi Chato
 
Back
Top Bottom