Jamani Human Resources Officers/Managers muwe na huruma kwa watoto wa wakulima

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
Ndugu zangu kuna kazi imetangazwa kwenye kampuni moja,watu wameapply ghafla mtu akaitwa pembeni na mtu wa karibu na HR akasema ili nipate hiyo kazi HR anataka kama kilo 8 hivi.Hivi kijana aliyetoka chuoni ambaye pesa ya fotokopi ya cheti ni ishu anatoa wapi hii pesa ukizingatia anatokea familia maskini.Kwa mpango huu kazi ni watu wenye pesa.
 
rafiki,

haya ndio mambo ya mjini, nipe kitu nikupe maisha. ulikua hujui
 
ndugu umesahau kauli mbiu yetu''UKITAKA KULA LAZIMA NA WE ULIWE KIDOGO'' Siku hizi kununua kazi ndio mpango mzima hata uwe na GPA ya 5 kama hutoi kitu hakuna kazi.changamka kama una hiyo kila 8 mpe mshikaji coz ukichelewa wajanja watawahi
 
kaka upo nchi gani? Mbona kwa tz,hiyo ni kawaida 2?hata mwezi uliopita kuna ofisi walitangaza nafac za kazi kuna hr akamwambia kijana tafuta kilo 6 upate kazi,na kweli yule kijana akawa nayo akampatia,hata kwenye interview hakwenda wiki iliyopita ameripoti kazini!inshu sio kutoa,je unayo?ndio tulipofikia.
 
Jamani mbona wanakukatisha tamaa hivyo, hao ni waliopata kazi kwa njia hiyo au wanaotoa kazi kwa njia hiyo, sio sehemu zote bwana mwambie ndugu yako aendelee kuomba sehemu nyingine atapata tu..
 
Ndo maana hatuna wataalam. Afu tunalilia kila siku TZ haina maendeleo. Any way, kila hareli waTanzania kufikia maendeleo na maisha bora
 
kweli kaziipooo.........lowasa atupe hzo kazi maana yy c ameishatuona cc ni bomulitakalo lipuka...bira aje alitegue hili bomu kabla yakulipuka.
 
Kijana changamkia hyo dili kama hauna ni PM nikamdakishe hela huyo HR fasta nilambe ajira.

"Ukitaka kula lazima na wewe uliwe"--Jakaya Kikwete

"Sina maana hiyo"--Jakaya Kikwete
 
kama una hiyo pesa ni bora akafanye biashara! kuliko kwenda kumpa mtu na usipate hiyo kazi@ zipowawa
 
Back
Top Bottom