Jamani hivi huyu baba ana upendo namimi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani hivi huyu baba ana upendo namimi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Loly, Aug 22, 2011.

1. Loly

Loly JF-Expert Member

#1
Aug 22, 2011
Joined: Mar 10, 2011
Messages: 485
Likes Received: 54
Trophy Points: 45
Wapendwa wana Jamii Forum naombeni msaada wenu kuhusu huyu baba yangu mzazi.
Kwa kifupi mimi ni mtoto wa nje ya ndoa ninatambulika kwenye familia na kwenye ukoo ninashirikishwa kwenye kila kitu kwenye majukumu ya hela na mambo mengine.

Baba yangu huyu hakuwa na uwezo siku za nyuma alikuwa ananisumbua sana kuniombaomba hela na nilikua nampa japo nikishingo upande maana hajanilea toka aliponitelekeza nikiwa mtoto kwa mama yangu hadi nimemaliza shule nimekuwa mtu mzima nafanya kazi ndipo alipo nitokea nakujionyesha ananipenda nikawa namjali kwa chochote nilichonacho. Sasa hivi baba huyu kapiga bingo ana hela kama uchafu cha ajabu hana time na mimi.

Anawasaidia watoto wake wengine mitaji na mambo mengine mengi mazuri kasoro mimi, kanitenga kama mtu baki jamani na hajawahi kunifanyia chochote kama mzazi kwenye maisha yangu. Nimelelewa na mzazi mmoja toka utotoni sijui ladha ya baba ikoje ila nilivyokua ndio kaanza kujipendekeza kwangu na wala sio kwa upendo ni kwa ajili ya shida zake.

Hivi majuzi bila aibu aliniambia nimsaidie kumtafutia mtoto wake sehemu nzuri ya kufanyia biashara anataka kumpa mtaji bila hata kujiuliza huyu nimeshamtendea lipi kwenye maisha yake.

Jamani huyu ni baba anaestahili kuonyeshwa upendo kweli? Maana sijawahi kufikiria au kuzania kuwa siku huyu baba yangu mzazi akiwa na hela atanidharau hivi.

Jamani wana jamii naombeni mchango wenu.

2. First Born

First Born JF-Expert Member

#2
Aug 22, 2011
Joined: Jul 11, 2011
Messages: 5,315
Likes Received: 96
Trophy Points: 145
hapo we jipinde tu mamaangu upige bingo la kufa mtu kumzidi yeye atrudi tena, na akifanya hivyo usiwe na huruma nae kabisa

3. The Boss

The Boss JF-Expert Member

#3
Aug 22, 2011
Joined: Aug 18, 2009
Messages: 37,822
Likes Received: 22,467
Trophy Points: 280
pole mno...
maumivu yako ni makubwa mno.....

cha kufanya ni kuwa shut down from your life
wote,yeye na watoto wake........

kuwa na uso wa mbuzi,usiwaonee haya,
hata ukisigia anaugua au amekufa.wewe kaaa nao mbali.badili namba ya simu,ikibidi uhame wasijue unapokaa

life is too short to let others stressing you up.....

4. Loly

Loly JF-Expert Member

#4
Aug 22, 2011
Joined: Mar 10, 2011
Messages: 485
Likes Received: 54
Trophy Points: 45

ahsante sana first born maana nina mauchungu

5. Loly

Loly JF-Expert Member

#5
Aug 22, 2011
Joined: Mar 10, 2011
Messages: 485
Likes Received: 54
Trophy Points: 45

Thanks so much The Boos hapo umeniambia kitu chamaana ukweli nina machungu mbaya

Vt

6. The Boss

The Boss JF-Expert Member

#6
Aug 22, 2011
Joined: Aug 18, 2009
Messages: 37,822
Likes Received: 22,467
Trophy Points: 280

ondoa machungu kwa kukaa nao mbali.....
watu wengine sio watu kabisa....shut them from your life

7. D

Domo Zege JF-Expert Member

#7
Aug 22, 2011
Joined: Sep 18, 2010
Messages: 687
Likes Received: 38
Trophy Points: 45
Ili ujue msimamo wake muombe fedha za mtaji au jifanye unashida inayohitaji fedha then angalia response yake.Ukiona anakupotezea ww mpotezee kabisaa.Tafuta fedha yako na usahau kama una baba focus na maza yako aliyekulea toka utotoni,anayejua shida zako zote

8. mikatabafeki

mikatabafeki JF-Expert Member

#8
Aug 22, 2011
Joined: Dec 29, 2010
Messages: 12,837
Likes Received: 2,101
Trophy Points: 280
dont f....u...ck wit a ni....gga who dont give a f.......u...ck endelea na maisha yako ndgu

9. Dumelang

Dumelang JF-Expert Member

#9
Aug 22, 2011
Joined: Aug 11, 2011
Messages: 2,190
Likes Received: 1,543
Trophy Points: 280
Ubaya haulipwi kwa ubaya na mzazi ni mzazi tu...hivyo sitakubaliana na dhana ya kumpotezea au kuishi mbali nao : that isn't a solution.
Kama una shida mwombe pesa uhakiki je atakunyima? kama akitosa usiuzunike yasahau then tafuta kwa jasho lako kwani pia ni bora kujua akunyimae samaki anakupa uwezo wa kujifunza kuvua. ridhika na kidogo unachopata ndo chako, kisha truggle for better future of urs..lastly mpende baba zaidi ya awali.

10. Dark City

Dark City JF-Expert Member

#10
Aug 22, 2011
Joined: Oct 18, 2008
Messages: 16,277
Likes Received: 241
Trophy Points: 160
Loly,

Huyo siyo baba mwenye upendo wa kweli kwako bali na baba tu kwako wakati ule anapokuhitaji.

Kama alivyosema Domo Zege, jipange umpe test ya mwisho ili akishidwa uachane naye na watoto wake. Na sidhani kama unatakiwa kuhangaika naye kwa vile hakuwahi kukuona kama mtu wa maana. Anajali mali zako na siyo wewe kama mtoto wake..

Achana naye...Bora uwe na marafiki wa nje kuliko ndugu asiye na manufaa kwako!!

11. k

kisukari JF-Expert Member

#11
Aug 23, 2011
Joined: Jul 16, 2010
Messages: 3,764
Likes Received: 1,052
Trophy Points: 280
trust me,inauma.mimi na dada zangu tumelelewa na mama tu,baba yetu hakuwa na upendo wowote kwetu,sasa tumeshakuwa huwa anajaribu kuwa karibu na sisi.najikuta roho yangu haipo safi juu yake,kama huyo wako,akitutafuta basi ana shida fulani.kama alivyosema mdau mmoja hapo juu,jaribu na wewe kumuomba hela uone ata react vipi,unastahili kwani na wewe ni baba yako.kama unaweza kumuuliza kistaarab,muulize baba nimekukosea nini?umuelezee how you feel

12. First Born

First Born JF-Expert Member

#12
Aug 23, 2011
Joined: Jul 11, 2011
Messages: 5,315
Likes Received: 96
Trophy Points: 145
hapo ndo la msingi, ukicheka na aliekununia utaonekana kichaa!

13. m

mageuzi1992 JF-Expert Member

#13
Aug 23, 2011
Joined: Apr 9, 2010
Messages: 2,512
Likes Received: 6
Trophy Points: 0
Mungu atakuongezea palipopungua usitie shaka

14. nyumba kubwa

nyumba kubwa JF-Expert Member

#14
Aug 23, 2011
Joined: Oct 8, 2010
Messages: 10,280
Likes Received: 1,720
Trophy Points: 280
Mimi sijaelewa kidogo. Wewe nadhani ni mtu mzima kwa maana umeshapita umri wa utegemezi. Kwa nini unataka baba yako akupe ela? Kwa sababu na wewe ulimpa au kwa kuwa una shida kweli kweli? Mh. mimi hata sijawahi kuwaza kupata mtaji toka kwa baba japo have different story kwani mimi sikutelekezwa.

15. Mpatanishi

Mpatanishi JF-Expert Member

#15
Aug 23, 2011
Joined: Jul 1, 2011
Messages: 1,709
Likes Received: 43
Trophy Points: 145
Temana nao tu wala ucjal maisha yapo tu,
fyt kivyako utatoka tu.
mm mwenyewe baba alikua na wake wawili, ndugu zangu kwa mama mwingine walitoka kimaisha kitambo tu then wakatutenga but sisi hatukujali tumesoma na ku fyt nikiwa na ndugu zangu wa mama mmoja/tumbo moja na Mungu si athuman nasi tumetoka kiana wenzangu wote wako mbele na wanatuma mambo me natengeneza life bongo.
Najua unaumia bt usijali kaza moyo, thread yako imenigusa sana nakumbuka enzi nasoma naumwa huku cna hata mia na braza wana mkwanja mrefu ila walinitosa kisa tu tumezaliwa mama tofauti.
Yani up to knw ctaki hata kuwasikia.
Nakuombea Mungu akujalie.

16. Tulizo

Tulizo JF-Expert Member

#16
Aug 23, 2011
Joined: Jun 13, 2011
Messages: 849
Likes Received: 21
Trophy Points: 35
Haina haja ya kusema piga chini..vita mbele.. kwa nini usumbue akili?

Naungana na mdau aliyesema ubaya haulipwi kwa ubaya. Kuna watu walishatendewa ubaya na wazazi wao lakini hawakulipa ubaya. Waliendelea kuwaheshimu kama wanavyoheshimu majirani zao..

Umeshakuwa mtu unayejitegemea. Sahau senti za baba au mali yake. Mheshimu Baba kama unavyowaheshimu wazee wengine pasipo na cha ziada.

Kama baba ameomba umsaidie kumtafutia kijana mwingine sehemu ya biashara, fanya kama unaweza, yaani kama vile mimi niku-pm na kuomba kama unajua sehemu yeyote iko free kufanya biashara.. kwa upande mwingine unamsaidia kama ungemsaidia jirani yako... kama hauwezi hakuna kusumbuka.

Cha muhimu angaika na maisha yako..usilipize kisasi.. heshima baba na ndugu kama unavyowaheshimu jirani zako waliokuzidi umri.

17. Ms Judith

Ms Judith JF-Expert Member

#17
Aug 23, 2011
Joined: Dec 24, 2010
Messages: 2,569
Likes Received: 20
Trophy Points: 135
mpendwa Loly,

kwanza naona kama tayari unalo jibu kichwani kwako kuhusu soala unalotaka ushauri na jibu lenyewe ni kuwa hupendwi na ni vyema ujiangalie mwenyewe na kuwageuzia kisogo baba yako na ndugu zako upande wa baba yako. hili linajitokeza hasa kutokana na namna unavyopokea kwa mikono miwili ushauri wa aina hiyo. ukisoma vizuri majibu yako kwa post zilizokushauri hivyo utaligundua hili ninalolisema.

pili, mi siko mbali sana na michango hiyo hapo juu.

ila nionavyo, tatizo unalo wewe na kwa kuwa umelelewa na mama pekee unaamini kuwa kwa kuwa sasa baba ana pesa na huko nyuma umekuwa ukimsaidia, basi unahitaji special treatment tofauti na ya ndugu zako wengine mliochangia baba. na pia kuna uwezekano kuwa hata mama yako akawa anakuaminisha mamabo hayo na hata kukuchochea utafakari upya upendo wa baba yako

katika jamii yetu kuna sababu nyingi sana zinazosababisha mtoto kujikuta analelewa na mzazi mmoja, kwa hiyo usimchukulie baba yako kama "mhalifu" moja kwa moja bila kuzingatia kilichosababisha ulelewe na mama peke yake. pengine hata sababu kubwa ni tabia ya mama yako, au nini kinine tena, hapo wanajuana wenyewe, labda kama walikudokeza kidogo japo hawawezi kukueleza kila kitu katika mahusoiano yao.

nijuavyo mimi, mtu asiyejiweza, mfano asiye na kazi ama biashara ya kipato cha kueleweka ndiye huwa anasaidiwa ili anyanyuke kimaisha na huenda baba yako anajitahidi kuwanyanyua ndugu zako ili nao wajitegemee hasa uizingatia kuwa pesa kachelewa kuzipata na huenda hakuwa amewaandaa vizuri kielimu kama wewe ulivyoandaliwa na ndio maana anaona basi bora ajaribu kuwapa mitaji wajaribu biashara. kwa upande wako, umesema mwenyewe kuwa una elimu na kazi na umekuwa hata ukimsaidia huyo baba yako. sasa na wewe unatakiwa kusaidiwa? aache kusaidia wasio na kazi na wasiojiweza kiuchumi, akusaidie wewe unayejiweza? au unataka akulipe pesa uliyokuwa ukimsaidia alipouwa na hali ngumu? nasikitika kusema kuwa, kwa kweli huu sio ubinadamu!

kama tatizo ni wasiwasi ulionao kuwa huenda hana mapenzi ya kweli kwako, basi chukua hatua ya kumjaribu, jifanye una matatizo kazini au tatizo jingine lolote ambalo kama mzazi litamshtua, kisha uone anavyo-react. na ukishaprove kuwa anakupenda, basi mweleze ukweli kuwa ulikuwa na mashaka na upendo wake ndio ukaamua kumjaribu na kama alikupa pesa mrudishie mwambie umethibitisha upendo wake ili naye ajue kulikuwa una mawazo gani upande wa pili. ila tahadhari ni kwambasi vyema kumjaribu mtu, kazi ya kuleta majaribu ni ya shetani, sisi tunapaswa kupambana na kuyashinda majribu, siyo kuyaleta ili kuwakwaza watu.

zaidi sana tafakari vizuri ushauri unaopewa na mama yako kumhusu baba yako, kuna mifano mingi sana ya watoto waliolelewa na mzazi mmoja kupotoshwa na huyo mzazi aliyehusika na malezi kumwelekea mzazi mwingine, so watch out my dear.

mwisho, kama ulimsaidia baba, ulifanya vyema na usichukulie kama ilikuwa investment ambayo unataka anze kuklipa na riba. tenda wema usitafute shukrani, upendo wa kweli huvumilia, hufadhili (1 Wakorintho 13:1-13). mwachie Mungu ndiye atakayekulipa kwa wema wako. sisi tunatakiwa kuwapenda hata adui zetu, sembuse kumpenda baba yako?

nakuombea amani ya Bwana ipitayo akili zote

Jina la Bwana libarikiwe

Glory to God!

18. Loly

Loly JF-Expert Member

#18
Aug 23, 2011
Joined: Mar 10, 2011
Messages: 485
Likes Received: 54
Trophy Points: 45

Miss Judith sijawahi kufundishwa na mama yangu kumdharau baba yangu hata siku moja kwanza nilikua nampenda baba sana toka nikiwa mtoto na mimi niliamini ananipenda mambo ya malezi nilijua hana hela sikumuhukumu kwatokunijali nikiwa mdogo, kinachoniumiza ni kwamba alijitokeza zaidi kwangu baada ya kujua anaweza kupata chochote kutoka kwangu sasahivi keshakamata mkwanja kanitosa na wala hataki nijue kuwa amepata hela nasikia tu tetesi kwa ndugu na jamaa namimi namuona jinsi anavyonunua magari kama pipi, na mbona kama kuwajali anawajali hata ndugu zangu wenye kazi zao nzuri tuu ili mradi ni watoto wake sio wasio iweza, kwani mimi ninatofauti gani na hao wengine? Mimi sio kwamba nina uwezo sana na isitoshe hana time na mimi ananitafuta akiwa na shida tuu kama hivyo, na wala hajawi kunieleza kuwa sasa hivi mambo safi maana mwanzo nilikua sijajua kwahiyo nikienda kumsalimia nikimwachia hela kidogo anapokea anakauka na wala haniambii kuwa hana shida ndogondogo tena kumbe keshatoka siku nyingi.
Hivi wewe unaona huyu ni mzazi mapenzi na mimi?

19. Loly

Loly JF-Expert Member

#19
Aug 23, 2011
Joined: Mar 10, 2011
Messages: 485
Likes Received: 54
Trophy Points: 45

Thanks mpatanishi kwakunielewa vizuri, nashukuru pia kwa mchango mzuri

20. Rutashubanyuma

Rutashubanyuma JF-Expert Member

#20
Aug 23, 2011
Joined: Sep 24, 2010
Messages: 158,806
Likes Received: 420,234
Trophy Points: 280
Malachi 2:15 "God seeks godly offsprings."

Kwa hiyo usipigwe na butwaa kwa hayo yaliyokukuta..........

Loading...