Jamani hivi huwa naeleweka?

sasa kama sisi vilaza ya nini unaendelea kutuandikia????????????
 
Naamini wengi hamtanielewa kwa sababu hamjui leo ninataka kuandika nini. Hata wewe unayesoma hapa huenda ukasoma mwanzo mpaka mwisho lakini ukatoka kapa kwa kuwa najua utakua ni mmoja wa vilaza wa kusoma makala za kufikirika au kusadikika.

Nimekuwa nikijiuliza, hivi ni kwani nini watu huwa hawanielewi, nimekuwa nikijaribu kuandika kwa lugha nyepesi sana lakini sieleweki. Je uwezo wangu ni mdogo katika kueleza jambo likaeleweka au wale ninaowaandikia wana uelewa finyu wa kuelewa kile ninachomaanisha katika maandishi yangu.

Inashangaza sana kuona hata wale wanazuoni ninaowaamini nao pia wamekuwa ni wagumu kunielwa. Japokuwa ninatumia lugha nyepesi lakini bado wanashindwa kunielewa. Pamoja na kwamba leo hii nimejitahjidi sana kuandika kwa lugha nyepesi tena nimejitahidi kufafanua na kutoa mifano kadhaa, bado naona kuna ugumu watu kuelewea ujumbe wangu.

Wako wapi wanazuoni wenye ujuzi wa kusoma maandiko ya wengine na kuyatolea ufafanuzi hadi watu waelewe pasi na shaka?, wako wapi malenga wetu na wajuvi wa lugha wasaidie kutafsiri maandiko haya?

Hata wewe unayesoma hapa sasa hivi yawezekana usinielewe ninataka kuandika nini, lakini nakuomba usome maandiko haya kwa makini naamini utanielewa hapo baadae kuwa namaanisha nini.

Ni mara nyingi nimekuwa nikiandika juu ya kile niandikacho na nimekuwa nikiandika kwa lugha nyepesi sana lakini nasikitika kuwa wasomaji wengi hawanielewi kabisa. Labda leo niombe ushauri kwenu kuwa ni lugha gani nyepesi ambayo itakuwa ni rahisi kwenu kunielewa? Nikisema niandike Kiingereza naamini sitaeleweka maana nakijua kiingereza changu ni cha kuombea maji tu, nikisema niandike kipare lugha ya mama yangu ndio wee nitachemsha kabisa, na kichaga nacho lugha ya baba, lahaula, nitawachekesha walionuna.

Mwe, mwenzenu nina kazi mimi, hata sijui nilitaka kuandika nini leo.

Hebu nikumbusheni, nilikuwa nataka kuandika nini vile?

Hata hivyo naamini mmenielewa japo kidogo, na asiyeelewa basi akaombe msaada pale TAASISI YA KUKUZA KISWAHILI CHUO KIKUU (TUKI)
Aaah,hapa leo nimekuelewa vizuri kabisa kuwa ulichokuwa unakifanya sio kuandika lugha ngumu wala laini bali ni mbinu zako za kitoto za kujipatia wingi wa threds ulizo tuma(kujiongezea points)
 
vukani Junior Member
red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png

green.png

green_right.png
Join Date: Wed Dec 2009
Posts: 9
Thanks: 0
Thanked 3 Times in 1 Post
Tatizo lipo hapo kwenye red , wewe bado bwana mdogo sana hapa jamvini, endelea kuandika 'ukikua' tutakuelewa tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom