Jamani hivi huwa naeleweka?

vukani

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
245
165

Naamini wengi hamtanielewa kwa sababu hamjui leo ninataka kuandika nini. Hata wewe unayesoma hapa huenda ukasoma mwanzo mpaka mwisho lakini ukatoka kapa kwa kuwa najua utakua ni mmoja wa vilaza wa kusoma makala za kufikirika au kusadikika.

Nimekuwa nikijiuliza, hivi ni kwani nini watu huwa hawanielewi, nimekuwa nikijaribu kuandika kwa lugha nyepesi sana lakini sieleweki. Je uwezo wangu ni mdogo katika kueleza jambo likaeleweka au wale ninaowaandikia wana uelewa finyu wa kuelewa kile ninachomaanisha katika maandishi yangu.

Inashangaza sana kuona hata wale wanazuoni ninaowaamini nao pia wamekuwa ni wagumu kunielwa. Japokuwa ninatumia lugha nyepesi lakini bado wanashindwa kunielewa. Pamoja na kwamba leo hii nimejitahjidi sana kuandika kwa lugha nyepesi tena nimejitahidi kufafanua na kutoa mifano kadhaa, bado naona kuna ugumu watu kuelewea ujumbe wangu.

Wako wapi wanazuoni wenye ujuzi wa kusoma maandiko ya wengine na kuyatolea ufafanuzi hadi watu waelewe pasi na shaka?, wako wapi malenga wetu na wajuvi wa lugha wasaidie kutafsiri maandiko haya?

Hata wewe unayesoma hapa sasa hivi yawezekana usinielewe ninataka kuandika nini, lakini nakuomba usome maandiko haya kwa makini naamini utanielewa hapo baadae kuwa namaanisha nini.

Ni mara nyingi nimekuwa nikiandika juu ya kile niandikacho na nimekuwa nikiandika kwa lugha nyepesi sana lakini nasikitika kuwa wasomaji wengi hawanielewi kabisa. Labda leo niombe ushauri kwenu kuwa ni lugha gani nyepesi ambayo itakuwa ni rahisi kwenu kunielewa? Nikisema niandike Kiingereza naamini sitaeleweka maana nakijua kiingereza changu ni cha kuombea maji tu, nikisema niandike kipare lugha ya mama yangu ndio wee nitachemsha kabisa, na kichaga nacho lugha ya baba, lahaula, nitawachekesha walionuna.

Mwe, mwenzenu nina kazi mimi, hata sijui nilitaka kuandika nini leo.

Hebu nikumbusheni, nilikuwa nataka kuandika nini vile?

Hata hivyo naamini mmenielewa japo kidogo, na asiyeelewa basi akaombe msaada pale TAASISI YA KUKUZA KISWAHILI CHUO KIKUU (TUKI)
 
tatizo lako unarudiarudia threads zako hadi mtu anashindwa aichangie ipi na aiache ipi .so kama kidhungudhungu vile!
 
mbona unasomeka vizuri tuu kaka labda kueleweka ndio tatizo. si kwa maandishi, bali inaoneka kama vile unajiuliza wewe mwenyewe tu kichwani hayo maswali yako badala ya kutuuliza sisi.

Umekua ukiijiuliza kipi? mbona ujasema tukakielewa au ndio tu-guess, like i said unaeleweka sana yeah labda ujielize wewe je unajielewa unataka kusema nini kwani wengine hatutaota unachotaka kusema bila ya kutuelezea.
 
Mkuu Mpaka uwe Senkd ndiyo ujue kama unaeleweka? au teh teh teh
 
Naamini wengi hamtanielewa kwa sababu hamjui leo ninataka kuandika nini. Hata wewe unayesoma hapa huenda ukasoma mwanzo mpaka mwisho lakini ukatoka kapa kwa kuwa najua utakua ni mmoja wa vilaza wa kusoma makala za kufikirika au kusadikika.

Nimekuwa nikijiuliza, hivi ni kwani nini watu huwa hawanielewi, nimekuwa nikijaribu kuandika kwa lugha nyepesi sana lakini sieleweki. Je uwezo wangu ni mdogo katika kueleza jambo likaeleweka au wale ninaowaandikia wana uelewa finyu wa kuelewa kile ninachomaanisha katika maandishi yangu.

Inashangaza sana kuona hata wale wanazuoni ninaowaamini nao pia wamekuwa ni wagumu kunielwa. Japokuwa ninatumia lugha nyepesi lakini bado wanashindwa kunielewa. Pamoja na kwamba leo hii nimejitahjidi sana kuandika kwa lugha nyepesi tena nimejitahidi kufafanua na kutoa mifano kadhaa, bado naona kuna ugumu watu kuelewea ujumbe wangu.

Wako wapi wanazuoni wenye ujuzi wa kusoma maandiko ya wengine na kuyatolea ufafanuzi hadi watu waelewe pasi na shaka?, wako wapi malenga wetu na wajuvi wa lugha wasaidie kutafsiri maandiko haya?

Hata wewe unayesoma hapa sasa hivi yawezekana usinielewe ninataka kuandika nini, lakini nakuomba usome maandiko haya kwa makini naamini utanielewa hapo baadae kuwa namaanisha nini.

Ni mara nyingi nimekuwa nikiandika juu ya kile niandikacho na nimekuwa nikiandika kwa lugha nyepesi sana lakini nasikitika kuwa wasomaji wengi hawanielewi kabisa. Labda leo niombe ushauri kwenu kuwa ni lugha gani nyepesi ambayo itakuwa ni rahisi kwenu kunielewa? Nikisema niandike Kiingereza naamini sitaeleweka maana nakijua kiingereza changu ni cha kuombea maji tu, nikisema niandike kipare lugha ya mama yangu ndio wee nitachemsha kabisa, na kichaga nacho lugha ya baba, lahaula, nitawachekesha walionuna.

Mwe, mwenzenu nina kazi mimi, hata sijui nilitaka kuandika nini leo.

Hebu nikumbusheni, nilikuwa nataka kuandika nini vile?

Hata hivyo naamini mmenielewa japo kidogo, na asiyeelewa basi akaombe msaada pale TAASISI YA KUKUZA KISWAHILI CHUO KIKUU (TUKI)

Kama ulivyotangulia kusema,naona hata hili wameshindwa kukuelewa,lakini mimi nimekuelewa ulichotaka kusema.Ya kwamba pindi uandikapo watu hawakuelewi kama ambavyo na leo wameshindwa kukuelewa ingawa haujui ni kwanini hawakuelewi.
 
to be honest ndg. Vukani... huwa haueleweki!! inawezekana ni ufinyu either wa wanazuoni, au wa kwako mwenyewe
 
Vukani,

Umeandika posts tisa tu halafu unadai maandiko yako hayaeleweki?
Nadhaki kichwa kinakuuma. Jaribu kumeza HEDEX.
 
kama mimi sijakuwelewa? inawezekana mada zako huwa hazieleweki.
 
Tatizo lako unataka kuongeza idadi ya your posts ndo maana yakikupanda unawasha computer!
 
We andika tu, usichoke kwani naamini ipo siku utaeleweka.
Ila kama huwa unaandika ukiwa umekunywa au umevuta kidogo, nakushauri usiandike hadi stimu ziishe kabisa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom