Jamani hii kitu ni ndege ama nini

Mada kama hii ililetwaga humu jamvini 2014. Mda mrefu wabongo tumelishwa sana matango na kamba iyo ni rocket
na kama unakumbuka tulivyojadiri hapa ndio serikali wakaanza mchakato wa kununua rada zile tano kwa bilion 67 moja dsm ,zanzibar, kia,mwanza ,mbeya
siyo mbaya wakatushukuru member wa hapa jf naamini kwa 100% walichukua wazo hapa
. 😎 🤣
 

Not true
 
kuna vibali vinatolewa na IATA na vile vya IASA ni tofauti kiutendaji.
Hawa wa anga la kimataifa wanahusiana na IATA ilihali wale wa anga la nchi husika wanasimamiwa na IASA mfano TCAA, FAA n.k.
 
Safi sana maana zamani tulilishwa matango pori,

Wakuu nahitaji ufafanuzi wa kina kama hamtojali kwa wale wanaojua ili nami nijue zaidi

Bado najiuliza maswali

Kama ni ndege ya kawaida kama hizi za kwetu kwa hiyo inaweza kubeba abiria?

Inaruhusiwa kuruka umbali gani ndo itue?

Je hizi za kwetu kwa zinaweza kuruka kwa kiasi hicho?

Huwa zinabeba nini hizo zinazopaa umbali huo?
 
Wazee wetu walijitahidi kujibu ili kupunguza maswali. Ufafanuzi mzuri sana huu.
 
Elimu Dunia!
 
dreamliner👇
 
Hiyo ndege inatembea mda wote huku inamwaga mafuta?
 
Umeua Mkuu. Yaani nilipoona thread karibu nicheke. Umejibu kisomi sana, watu kama nyie mnastahili heshima zenu humu JF. Ajabu atakuja yeboyebo anabishana na wewe!

Actually mtoa mada angepanda ndege akikaa dirishani anaweza pia kuona hiyo trail ndege inapopita eneo lenye super saturated air na baridi. Na nimefurahi ulivyofafanua juu ya contrails (condensation trails). Wengi wanadhani ni moshi wa ndege au rocket! Labda kwenye rocket wanamaanisha ni jet engine aircraft.
 
Kwa uelewa wangu huu mdogo, ila wanaojua zaidi watasema hii ni Ndege Kasi aina ya Concorde ambayo kwa Afrika inatua tu Cairo na Cape Town.
Concorde hakuna siku hizi hazisafiri kitambo sana zilikua zinakula sana mafuta so ikawa hasara kuzi oparate wakazipiga chini saizi zimebaki makumbusho
 
Huo ni uongo Mkuu, kama huelewi jambo ni vema ukae kimya kuliko kuleta stori za wajuba wa vijiweni

Ndege inamwaga mafuta wakati wa kutua kwa emergency tu. Na ndege zinazomwaga mafuta ni zile ambazo zilikuwa zifanye safari ya masafa marefu (long haul) lakini muda mfupi baada ya kuruka ikapata emergency inayomlazimu atue wakati bado ana mafuta mengi, na uzito wa mafuta, mizigo na abiria ni mkubwa akitua bila kupunguza uzito ataharibu landing gear. Pia wanaweza kumwaga mafuta kama emergency landing ina hatari ya moto, kwa mfano, kama landing gear imekataa kutoka na hivyo inabidi atue kwa tumbo. Atamwaga mafuta kupunguza uwezekano wa moto mkubwa. Na pia uzito mkubwa wa ndege maana yake umbali mrefu wa ku brake, kwa kuwa momentum inakuwa kubwa.

Ndege ya kwenda Mbeya kutoka Dar ikipata emergency hata eneo la Kibaha tu inaweza kurudi na kutua bila kumwaga mafuta kwa kuwa ndege huwa hawajazi mafuta kwa kusema weka full tank. Hata ndege ya kwenda South Africa inaweza kurudi na kutua bila kumwaga mafuta, kwa kuwa mafuta atakayokuwa amechukua sio mengi kiai hicho kwa safari ya masaa matatu ya kwenda Johannesburg

Hakuna pilot atamwaga mafuta baada ya kufika destination eti aliweka mafuta mengi au alipatwa na mgandamizo mkubwa njiani. Hizo n stori za vijiweni.
 
Hyo haiitwi rocket jombaa hiyo inaitwa jet, rockets ni zile ndege zinaenda mwezini huko jombaa.
 
Haya hebu mwaga madini ewe mtaalamu.
Nilishajibu

Ndege inamwaga mafuta wakati wa kutua kwa emergency tu. Na ndege zinazomwaga mafuta ni zile ambazo zilikuwa zifanye safari ya masafa marefu (long haul) lakini muda mfupi baada ya kuruka ikapata emergency inayomlazimu pilot atue wakati bado ana mafuta mengi, na uzito wa mafuta, mizigo na abiria ni mkubwa akitua bila kupunguza uzito ataharibu landing gear. Pia wanaweza kumwaga mafuta kama emergncy landing ina hatari ya moto, kwa mfano, kama landing gear imekataa kutoka na hivyo inabidi atue kwa tumbo. Atamwaga mafuta kupunguza uwezekano wa moto mkubwa. Na pia uzito mkubwa wa ndege maana yake umbali mrefu wa ku brake, kwa kuwa momentum inakuwa kubwa.

Ndege ya kwenda Mbeya kutoka Dar ikipata emergency hata eneo la Kibaha tu inaweza kurudi na kutua bila kumwaga mafuta kwa kuwa ndege huwa hawajazi mafuta kwa kusema weka full tank. Hata ndege ya kwenda South Africa inaweza kurudi na kutua bila kumwaga mafuta, kwa kuwa mafuta atakayokuwa amechukua sio mengi kiasi hicho kwa safari ya masaa matatu ya kwenda Johannesburg

Hakuna pilot atamwaga mafuta baada ya kufika destination eti aliweka mafuta mengi au alipatwa na mgandamizo mkubwa njiani. Hizo n stori za vijiweni.
 
uko sahihi mkuu physics form two hii sema wengi humu wakati sisi tunasoma wao walikua wanawinda ndege na manati kidding ha ha ha ha
 
nilijua ni vumbi kwenye barabara ya ndege angani

huko angani kuna trafiki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…