lonalove
Member
- Sep 17, 2016
- 27
- 66
Habari zenu wana JF, ni Mara yangu ya kwanza kupost hapa japo ni mfuatiliaji wa mda mrefu wa maada mbali mbali hapa jukwaani.
Ndugu zangu Mimi ni mhitimu wa shahada ya Elimu ya masomo ya sanaa kutoka chuo kimoja mkoani Morogoro .nimehitimu masomo yangu 2015 .Nilichagua kusoma Shahada ya elimu kwa makusudi kabisa nikitegemea kuwa nikimaliza tu nitapata ajira na kuweza kupata kipato cha kujikimu na kusaidia wazazi wangu na wadogo zangu pia ,ukizingatia kuwa hali ya uchumi wa familia sio nzuri. Mategemeo yangu yalikuwa kwamba nikimaliza elimu yangu nitapata kazi kama ilivyokuwa kwa waliotutangulia ambao tuko fani moja.
Lakini kumbe nilichokitegemea sicho ,mwaka na miezi sasa imepita bila matumain yoyote..nimejaribu kutafuta hata tempo za kufundisha nako ni shida tuko wengi tunaohitaji .
Nimebaki tu nasikiliza matamko ya wizara ya elimu nikitumaini labda kuna siku watatuhitaji lakini naona kama niko kwenye fani iliyotengwa.
Toka nimalize chuo nimebaki tu nyumbani nikiwa mzigo badala ya msaada kwenye familia ,imekuwa vigumu hata kupata hela ya matumizi yangu madogomadogo.
Najua tupo wengi wenye hali hii ,ninachoomba wizara ya elimu na serikali kwa ujumla isitusahau na sisi tuliosoma Shahada ya Elimu masomo ya sanaa hali zetu ni mbaya sana.