Jamani eh, sasa nimeamini, panapofuka moshi kweli panaficha moto...... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani eh, sasa nimeamini, panapofuka moshi kweli panaficha moto......

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Rutashubanyuma, Oct 20, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  Kuna rafiki yangu wa karibu anaishi nyumba za kupanga na kwa yale ambayo amenielezea hadi sasa yananithibitishia ya kuwa kwenye mapango hayo kweli kuna mambo.

  Huyu njema ana kidosho wake mrembo haswaa yaani ile ya mithili ya maandiko ya Shabaan Robert kama vile. Hawa wanandoa wanaishi wote bali yeye ni mtu wa masafa marefu kwa maana ya kuendesha malori makubwa na muda mwingi yupo nje ya pango lake.

  Sasa amejawa na hofu sana katika nyumba aishio ambayo ina makapera wengi sana na jinsi awaonavyo hasa wanaposalimiana na mke wake machale yanamcheza cheza kuwa hapa siyo bure ipo shughuli kubwa inaendelea wakati yeye yupo safarini akitafuta ugali wa familia. Hadi sasa bado hawajajaliwa kupata mtoto.

  Siku moja usiku alirudi mapema kidogo kuliko ilivyotarajiwa na aliyoyakuta yalimwongezea wasiwasi.............alikuta njemba nyingine imetuna kwenye kiti chake huko ikitwanga biryani ya nguvu na bia ikiwemo hapo pembeni kwake.

  Yaani memsapu alipomwona jamaa yake alishtuka sana na hili liliongezea ule wasi wasi wa jamaa yangu mbona hawa majirani huwa hawamtembelei akiwepo lakini akiwa hayupo ndiyo vikumbo kwake vinapata kasi sana? Na swali jingine lililomkera ni kuwa kwanini mama watoto alishtuka hivyo kama hakuna mpango wowote ule wa dhuluma dhidi yake?

  Jamaa yangu huyu ameanza hata kukonda maana ana wasiwasi sana hawa majirani zake wanaweza kuwa wanamlisha memsapu wake visivyofaa kuliwa na madhara yake sote tunayajua...

  Sasa jamaa yangu amekuja kwangu kwa ushauri wa kiutu uzima na mimi nimemweleza nina ndugu zangu kwenye Jamii Forums kwa hiyo anipe muda wa kukusanya ushauri wa kujitosheleza...............

  Sasa kazi kwenu ajitoe vipi hapa huyu ndugu yangu ambaye simanzii yake sasa ni mlima......anampenda mama watoto wake ile mbaya lakini hayupo tayari kuona njema zinamfanyia unyama huo anaouhisi na anadai machale yake siyo ya utani utani ni ya uhakika vile.............
   
 2. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ruta,
  Kwani jamaa hakuwahi kumuliza mkewe kuwa kwanini hizo njemba huwa zinakuja akiwa tu hayupo?siku hiyo ya njemba kula msosi na mamie kushtuka jamaa hakumuliza baadae kuwa ni nini kilimshtua? Je ni njemba tofautitofauti au ni aina moja huwa anaikuta?zote zinaishi around?
  Kama utafafanua hapo naweza sema kitu.
   
 3. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kama demu sio mwaminifu vile! yani mumeo hayupo wewe unaingiza njemba ingine tena ni jirani anakula na glass ya bia pembeni!?
   
 4. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Keep it up ruta I will the first to congrats when u reach 1000 posts. I hope you will be in JF records as you recently joined and turn 1000 in a short period. NAkuaminia muzee:biggrin1:
   
 5. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sokomoko umenifurahisha sana,,close follow up
   
 6. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jamaa leo moja ameanzisha threads 8 na post alizofanya ni 36 hadi hapa tu mie nampa hongera sana aendelee hivi hivi na kutu encourage na sie tupige mabandiko 50 per day!
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  nakushauri, ukamshauri......ahame hiyo nyumba
   
 8. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ushauri mzuri huu!
   
 9. J

  Jmpambije Member

  #9
  Oct 20, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Akihama na baadaye njemba zikaja alikohamia na hapa mama akadai zimekuja kumsalimia kwani walikuwa majirani wazuri kwenye nyumba ya awali!!!
   
 10. m

  mpangwa1 JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 279
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  amweleze kisa cha kuhama kuwa anakimbiza mzingo toka kwa hao manjemba anahisi wanamwibia...
   
 11. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  1 aongee na mkewe juu ya wasi wasi km kweli ama si kweli atajua kutoka kwenye mdomo wa mkewe
  2 aafanye kauchunguzi kdg japo kwa kuwauliza majirani wengine au aweke kijimtego au amtume mtu awe anamfatilia mkewe wakat hayupo
  3ahame nyumba
   
 12. K

  Kipenzi Chao Member

  #12
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Atakapohamia hawapo manjemba?Au ni kuzidi kuongeza idadi tu?
   
 13. K

  Kipenzi Chao Member

  #13
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kutumia mbinu namba 1 hapo juu ni sawa na kumpatia JK nafasi ya kukoment kuhusu kukamatwa kwa karatasi za kupigia kura huko Tunduma....! Kwani ungetegemea jibu gani?

  No. 2 huenda ikazaa matunda ya ukweli, lakini mara nyingi jamii huwa tunafichiana maovu kama haya...! Katika watu waliowagumu kukupa ukweli ni marafiki, na maadui wako, hasa pale wanapojua ungefanya maamuzi gani....! La msingi ni kwamba aelewe kuwa kumfumania nyoka si lazima umkute akiingia shimoni, bali hata ukimkuta akitoka ni kumfumania pia....! Mwenye macho haambiwi tazama, na akiambiwa ni tusi...! Sasa yeye anataka tumtusi? For an act to be cheating is not necessarily to be confirmed by the cheater....!

  No 3 pia sio solution, maana huko atakapohamia na manjemba wapo...! Matokeo yake atazidi kuongeza idadi tu....!
   
 14. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  wasi wasi wa mapenzi mwenzangu wauaaaaaaaaaaaa,its beta said if nothing is said at all.afanye uchunguzi kwanza kwa kina kwenye ukweli uhongo hujitenga,everything happen for a reason,smtimes silent has the loudest voice.
   
 15. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  kwani huku ni kwenye ukumbi wa uchaguzi au siasa???
   
Loading...