Jamani, Dr. Ulimboka yuko wapi siku hizi?

Sijui kwa nini, lakini nimejikuta nimemkumbuka Dr Ulimboka! Sijui anaendeleaje, afya yake anaendeleaje, na huduma yake ya udaktari anaendeleaje! Namtakia afya njema na maisha marefu!
 
aaah yupo lakiini kama hayupo sipati picha akipatwa raibu saanane itakuwaje
 
Atakuwa muhimbili a naendelea na kazi ya udaktari
Hakuwa daktari wa Muhimbili. Sikumbuki vizuri lakini ilikuwa international organisation. Alikuwa na solidarity tu na wenzie kwa sababu alikuwa kiongozi wao.
 
Dr.Ulimboka alitekwa katika awamo ya nne akapelekwa kuteswa mabwepande na baadaye kuokotwa, sababu kubwa ya kutekwa kwake inaelezwa kuwa ni kuwatetea madaktari kitu ambacho watawala hawakukitaka.

Yale aliyoyatetea Ulimboka yalipuuzwa na awamu iliyopita lakini ilipoingia awamu mpya Cha KwanZa ilitaka kuweka mazingira ya huduma za afya kuwa mazuri japo baadaye kasi ya utoaji huduma bora imeshukwa kwa kukosekana motisha kwa watoa huduma, kukosekana kwa madawa na vifaa vya kutolea huduma.

Yamkini waliomtesa wanatibiwa au ndugu zao wanatibiwa na madaktari walewale aliokuwa anawatetea Ulimboka, yamkini waliohusika Leo hii damu ya Ulimboka inawatesa huko walipo na hakuna anayewasikiliza. Yamkini walioandaa hizo njama leo hawathaminiwi na wanateseka kwa ufukara ila mteswa amebaki Shujaa kwenye jamii.

Natamani kusikia alipo Shujaa huyu na ningetamani kujua wale waliotuhumiwa kumteka walifanywa Nini?
 
Nipo mkuu..una shida gani na mimi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…