Jamani, Dr. Ulimboka yuko wapi siku hizi?

Jamani, Dr. Ulimboka yuko wapi siku hizi?

Nipo mkuu..una shida gani na mimi?
Oh, ulipo malyafyale? Twa masiku? Ulinkafu? Twa mbombo? Ulikatiwa sh ngapi hadi ukatengua ahadi yako ya kutwambia ukweli waliokung'oa kucha, meno na kuvunja korodani? Bado unafanya kazi ya utabibu? Unaishi wapi? Maswali ni hayo tu malafyale. Ndaga na malole fijo!
 
Huyu Daktari alipata madhara makubwa kule Mabwepande na baada ya kunusurika kifo, aliaahidi kuwa atasema kila kitu kuhusu watesi wake.

Kutokana na mateso aliyoyapata daktari huyu, gazeti moja maarufu lilifungiwa kwa kutoa habari za mhuka mkuu wa kadhia hii ambaye lilidai yuko Magogoni.

Sasa huyu daktari amepotea wala haongei tena. Je yuko wapi na je anaendelea na kazi yake ya udaktari au bado anajipanga kutoa taarifa kamili?

Kuna daktari mwenzake mmoja naye alipata madhara makubwa ya kupukutika ngozi na kunyonyoka nywele ambapo alikwenda kuponea India.

Rafiki yake mkubwa aitwae Six akapita sehemu mbali mbali ikiwa ni pamoja na kanisani na kutangaza kuwa rafiki yake amepewa sumu. Dr mwenyewe aliporudi baada ya kunusurika kifo aliaahidi kuwa ataweka mambo hadharani. Wakati anaendelea kutangaza kuwa ataweka mambo hadharani, tukasikia ghafla kapewa uwaziri.

Kuanzia hapo akasitisha matangazo ya kuwa ataeleza kilicho mpata na hivyo kumfanya rafiki yake Six kuonekana ni mnafiki na mwongo mkubwa. Sasa hicho kimya chake kinaeleweka kwani keshapewa fidia.

Sasa rafiki yangu "Dr. Mabwepande" kapewa nini hadi awe kimya namna hii na kusahau ahadi zake?!
Nasikia alifariki baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani
 
Oh, ulipo malyafyale? Twa masiku? Ulinkafu? Twa mbombo? Ulikatiwa sh ngapi hadi ukatengua ahadi yako ya kutwambia ukweli waliokung'oa kucha, meno na kuvunja korodani? Bado unafanya kazi ya utabibu? Unaishi wapi? Maswali ni hayo tu malafyale. Ndaga na malole fijo!
Kwa sasa nipo Malawi nalima chai .......na tumbaku
 
Huyu jamaa siku hyo anatekwa nakumbuka tulikuwa bakulutu bar (govorners sahv)tuliskia kuna mtu yuko bar fulani ametekwa

Ova
 
Wakuu habari za mihangaiko, natumai wote wazima wa afya mkiendelea na majukumu yenu ya kikazi. Basi nikaona leo si vibaya kujikumbusha kidogo mkasa uliomkuba dkt Ulimbona hapo miaka ya 2012.

Tupate story fupi juu ya mkasa wake ulivyotokea na kwa anayefahamu je yupo wapi hivi sasa na bado anaendelea na taaluma yake ya udaktari au alishaachana nayo tangu matatizo haya yamkute.

Na Mwandishi Wako:

"NI saa 12:45 asubuhi, bado kiza kimetanda katika eneo hili la Msitu wa Mabwepande. Mbele yangu namwona mtu akiwa amekaa chini, pembeni ya barabara akiwa amelowa damu mwili mzima.

"Ninapomkaribia nasikia sauti ya mtu huyo ikisema kwa taabu; naomba msaada jamani… naomba msaada jamani, hivi ndivyo anavyoanza kusimulia Msaidizi Mkuu, mtu wa kwanza kumwona Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka baada ya kutekwa, kupigwa na kutupwa katika Msitu wa Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Mara baada kumwona daktari huyo akiwa katika hali hiyo, alijaribu kumkokota kumtoa eneo hilo, lakini alishindwa kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo.

Baada ya hapo, aliamua kusubiri mtu mwingine apite eneo hilo ili amwombe wasaidiane kumpeleka Kituo cha Polisi Bunju.

Anasema muda mfupi baadaye aliona gari likija mbele yao, akalinyooshea mkono kulisimamisha. Liliposimama, akamweleza dereva hali aliyokuwa nayo Dk Ulimboka na kwamba anahitaji msaada wa haraka.

Msaidizi Mkuu ambaye hadi wakati huo alikuwa hamfahamu mtu ambaye alikuwa akimsadia kuwa ni kiongozi wa madaktari kutokana na sura yake kuvimba, anasema walimwingiza katika gari hilo na kumpeleka Kituo Kidogo cha Polisi Bunju.

Anasema, Dk Ulimboka wakati huo alikuwa akiendelea kuvuja damu katika baadhi ya majeraha yake huku akiwa hana suruali na kubaki na bukta tu, huku akizungumza kwa taabu.
Kituo cha Polisi Bunju
Baada ya kumfikisha kituoni hapo, walitoa maelezo namna walivyomwokota na kumsaidia kumfikisha hapo.
Polisi baada kumhoji Dk Ulimboka, aliwatajia namba ya simu ya rafiki yake aitwaye Dk Deo.

Walipompigia na kumweleza tatizo hilo, aliamua moja kwa moja kwenda Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, kutoa taarifa hizo na hatimaye kuandamana na watu kadhaa kutoka hapo akiwamo Mkurugenzi wake, Hellen-Kijo Bisimba.

Wawasili kituoni
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania wa kituo hicho, Onesmo Olengurumwa, anasema waliwafika Polisi Bunju saa 3:36 asubuhi na kumkuta Dk Ulimboka akiwa amekalishwa kwenye benchi huku damu ikiwa imeganda kwenye majeraha mwilini.

Olengurumwa anasema waliwahoji polisi waliokuwa kituoni hapo kwa nini wakae na mtu aliyeumia kiasi hicho muda mrefu bila ya kuita gari la wagonjwa kumchukua ili kuwahi kupatiwa matibabu.

Olengurumwa anasema polisi walisema kwamba, walikuwa wanawasubiri ndugu zake wafike.
Baada ya muda mfupi, akiwa ameingizwa kwenye gari kupelekwa hospitali, Dk Ulimboka aliomba maji ya kunywa akisema ana kiu sana, lakini alipopewa, alikunywa kidogo akashindwa.

Anasema wakiwa njiani, alikuwa akilalamika kuwa anasikika maumivu makali huku akisisitiza kuwa tukio la kutekwa na kupigwa lilikuwa la kumuua.

"Jamani hawa watu walitaka kuniua walikuwa wamepanga kuniua," alisikika mara kwa mara akisema Dk Ulimboka wakati anapelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu.

Maelezo ya Dk Ulimboka
Baada ya Dk Ulimboka kuokotwa aliweza kuzungumza na kurekodiwa muda mfupi baada ya kutolewa msituni na mazungumzo yake yalikuwa hivi;
“Nilikamatwa na watu hao usiku wa Jumanne nikiwa maeneo ya Leaders Club, Kinondoni na daktari mwenzangu baada ya kupigiwa simu na mtu mmoja ambaye alidai kuwa anafanya kazi Ikulu.

“Kuna jamaa mmoja anafanya kazi Ikulu, kama siku tatu mfululizo alikuwa akitaka kukutana na mimi ila nilishindwa kukutana naye kwa kuwa nilikuwa na kazi nyingi na wakati mwingine mpaka usiku,” alisema Dk Ulimboka.

Huku akizungumza kwa taabu kutokana na mdomo wake kuvimba, alisema siku hiyo mtu huyo alimpigia tena simu na kumtaka wakutane.
“ Jana (Jumanne) alinipigia simu na nikamwambia daktari mwenzangu twende tukaonane naye, wakati huo alitueleza kuwa alikuwa maeneo ya Kinondoni Stereo,” alisema Ulimboka na kuongeza:
“Tulipofika maeneo hayo tukampigia simu na akatueleza kuwa alikwisha ondoka, baadaye tukamweleza sehemu tulipo mimi pamoja na mwenzangu.”

Alisema kuwa, wakati anakutana na mtu yule maeneo ya Leaders Club, hakuwa na amani.
“Kwa kweli siku ile nilivyoonana na mtu yule sikuwa na amani kabisa ya kukaa eneo lile,” alisema Dk Ulimboka.

Alisema kuwa wakati wakiendelea na maongezi ya kawaida, bado aliendelea kuwa na mashaka na mtu yule.
“Katikati ya maongezi nikaona ameanza kuzungumza na simu, kila tukitaka kuagana alikuwa akizungumza na simu, sijui nini kilikuwa kinachelewesha sisi kuagana,” alisema Dk Ulimboka na kuongeza:
“ Ghafla walitokea watu kama watano na kusema kuwa hawana tatizo na mtu yeyote katika eneo hilo isipokuwa mimi.
Wakati sijakaa sawa, waliniburuza hadi barabara ya lami kwa kuwa eneo hilo lilikuwa karibu na barabara.”

Aliongeza, “Nilipowauliza wananipeleka wapi, wakaniambia kuwa mimi nasumbua sana na nitajua hukohuko, waliniingiza katika gari jeusi, lakini halikuwa na namba. Niliwauliza kosa gani nimefanya? Hawakunijibu kitu na kusema, we twende utajua hukohuko.’’

Alisema alipokuwa ndani ya gari hilo watu hao walimpiga na kwamba walipofika maeneo ya Victoria, walichukua sweta nyeusi na kumfunga usoni, jambo lililomfanya ashindwe kuona kinachoendelea ikiwa ni pamoja na alikokuwa akipelekwa.

“Walinipiga mateke ya mbavuni, wakati mwingine walitumia vitako vya bunduki, kila nilipokuwa najaribu kuangalia ninapokwenda nilishindwa,” alisimulia Dk Ulimboka.

Alisema kuwa watu hao walimpeleka katika nyumba moja ambayo hakujua iko sehemu gani ambapo walimshusha na kuanza kumshambulia kwa mateke mfululizo kila sehemu ya mwili.

Wakati huo, wote walimshinikiza awaambie nani yupo nyuma ya mgomo wa madaktari.

“Tangu saa sita usiku mpaka saa 9:00 alfajiri walikuwa wananipiga tu, kuna wakati nilijaribu kukimbia wakapiga risasi juu nikasimama na sikuweza kukimbia tena,” alisema Dk Ulimboka na kuongeza:
“Nilisimama, wakaendelea kunipiga, niliwasikia wakisema ama wanichome sindano ya sumu nife au kunikanyaga na gari. Baadaye wakaanza kuning’oa meno na kucha kwa kolea huku wakinilazimisha kusema nani yupo nyuma ya mgomo wa madaktari."

Alisema kuwa, watu hao walikuwa na bunduki kubwa ambayo hakuweza kuitambua ni aina gani.
“Waliniambia kuwa ninajua ninachokifanya hivyo wanaweza kunichoma sindano ya sumu nife au wanikanyage na gari nife,” alisimulia.

Dk Ulimboka alisema kuwa awali hakuwa na shaka na watu hao kwa kuwa alidhani ni polisi, lakini baadaye alishindwa kuwaelewa kwani watu hao walimchanganya.
“Sikuweza kuwatambua ila naweza kusema ni askari, walipokuwa wananipeleka niliwauliza mnanipeleka wapi na wakati huo nilikuwa sioni mbele ila ilikuwa kama maeneo ya Mwenge hivi,” alisema Dk Ulimboka.

Alisema kuwa baadaye alipoteza fahamu na hakuweza kuona chochote zaidi ya kusikia sauti za watu hao kwa mbali.
“Nilikuwa sioni na nilipoteza fahamu nikawa nasikia tu wakinibeba, gari lilitembea muda mrefu, sikujua ni wapi tunakwenda, kumbe ndio huko Mabwepande,” alisema.

Alisema kuwa walifika maeneo ya barabara ya vumbi na baadaye wakamshusha na kumbeba hadi msituni.
“Waliniburuza na kuniacha huko na muda wa saa kumi alfajiri ndipo nikazinduka na kuanza kujiburuza kuelekea barabarani ambako nilisaidiwa na mtu mmoja ambaye simtambui,” alisema Dk Ulimboka.

Na hii ni historia fupi juu ya mkasa uliowahi kumtokea dokta Steven Ulimboka, Je yupo wapi hivi sasa
 
Stori yake ilinisisimua sana sijui sahivi yuko wapi simsikii tena!. Hapo ndo nilianza kujua kumbe wanaoandikaga vitabu vya mauwaji na kutekwa ni kweli haya Mambo!!!
Sidhani Kama walitaka kumuua naona hawakudhamiria ila lilikuwa ni kalipio kali ambalo walilifanya asilimia 50 abaki na 50 nyengine asibaki..!

Hii pia inatutaka tufikiri kuwa sio kila anaewataka watu waandamane au vipi basi anaweza kuwa pekee!.. huenda kulikuwa na watu nyuma kweli na huenda kule ilikuwa ni kuwapa ujumbe pia kuwa wamefahamika!!.. utata mwengine ni kuwa huyo aliejitambulisha ya kuwa ametokea ikulu!!.. so hii inamaanisha kitengo kilitumika! Au ni watu tu walitaka kuuchafua uongozi wa jakaya..??!!! Hili nalo la kuweka kwenye ulizo kubwa.
 
Kwa kifupi jamaa serikali ilikwenda kumalizana nae kama vile walivyomalizana na familia ya yule binti aliyechapwa risasi na polisi siku ya maandamano ya chadema.
 
Stori yake ilinisisimua sana sijui sahivi yuko wapi simsikii tena!. Hapo ndo nilianza kujua kumbe wanaoandikaga vitabu vya mauwaji na kutekwa ni kweli haya Mambo!!!
Sidhani Kama walitaka kumuua naona hawakudhamiria ila lilikuwa ni kalipio kali ambalo walilifanya asilimia 50 abaki na 50 nyengine asibaki..!

Hii pia inatutaka tufikiri kuwa sio kila anaewataka watu waandamane au vipi basi anaweza kuwa pekee!.. huenda kulikuwa na watu nyuma kweli na huenda kule ilikuwa ni kuwapa ujumbe pia kuwa wamefahamika!!.. utata mwengine ni kuwa huyo aliejitambulisha ya kuwa ametokea ikulu!!.. so hii inamaanisha kitengo kilitumika! Au ni watu tu walitaka kuuchafua uongozi wa jakaya..??!!! Hili nalo la kuweka kwenye ulizo kubwa.
kweli mkuu na kipindi cha jakaya mambo ya utekaji nyara yalishika kasi kweli
 
Kwa mateso yale hata angekuwa nani hawezi kuendelea kuwa ndani ya mipaka ya Tanzania.
Lazima ukaendeleze taaluma sehemu ambako wanahitaji watu.
 
Mtesi wake aliyetajwa Ramadhani Ighondu kateuliwa kugombea jimbo moja na Nyalandu huko kwao Singida. Naona kama Ahmed Msangi angetia nia nae angeteuliwa kugombea.
 
Mtesi wake aliyetajwa Ramadhani Ighondu kateuliwa kugombea jimbo moja na Nyalandu huko kwao Singida. Naona kama Ahmed Msangi angetia nia nae angeteuliwa kugombea.
Huyu jamaa katili Sana, Wana CCM wenzangu Bora Jimbo analogombea liende upinzani. Huyu Ighondu ni zaidi ya ibilisi.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom