Jamani asiwadanganye mtu — kuokoka ni kutamu!

Jamani asiwadanganye mtu — kuokoka ni kutamu!


  • Walokole tafuteni kitu kingine cha kuongelea.. nyie kila saa ni uchawi na mapepo. Ingekuwa magonjwa yanatoweka kwa kukemea basi walokole wote msingekua mnaenda hospitali.
Siku ukiona ukuu wa Mungu hutasema haya hata sisi tulikuwa wabishi sn ...
 
Hehee. Hii mada itawaacha wapinzani wa wokovu wakikuna vichwa, maana kila pointi ina ushahidi wa maisha na wa Neno la Mungu.
Yes, watu wasije wakafikiri nimejitungia tu. Ushuhuda huo ni udhihirisho wa ukweli wa ahadi za Mungu
 
Hii sio chit chat. Nimethibitisha kwa macho na masikio yangu, na kuonja kwa nafsi yangu. Tangu nilipompokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wangu, nafaidi utamu huu:
  • Siogopi wachawi wala siogopi kulala kwenye nyumba zenye vibwengo – wachawi wakinijia, nawapiga 'knock out' kwa Jina la Yesu (Isa 54:17).
  • Nikiomba napewa – kila sala yangu imekuwa na matunda (Mt 7:7).
  • Magonjwa ya zinaa hayanipati ng'oo – uasherati kwangu ni mwii... ni mwiko (1 Kor 6:18).
  • Na-save pesa nyingi za matibabu – kwa kuwa magonjwa mengi nayakemea na yanatoweka kwa Jina la Yesu (Isa 53:5).
  • Nina amani isiyoelezeka – amani aliyonipa Yesu haipatikani kwa njia nyingine (Yn 14:27). Nina amani hata katikati ya majaribu na dhoruba (Yn 20:19).
  • Sipati kamwe hangover ya walevi – furaha yangu haina majuto. Nikifurahi leo, sijuti wala kuona aibu kesho (Flp 4:4).
  • Sipatwi na mikosi na mabalaa ya kulogwa – kwakuwa hakuna uchawi unaofanikiwa juu yangu (Hes 23:23).
  • Bwana ndiye Mchungaji wangu, hivyo sipungukiwi na kitu (Zab 23:1). Mungu amekuwa akibariki kazi za mikono yangu kila siku mjini na mashambani (Kum 28:3)
  • Namshinda shetani na mapepo yake kirahisi kabisa – akiinua kichwa, nambamiza chini na kumtimua kwa Jina la Yesu (Yk 4:7).
  • Mungu amenipa maarifa mengi ya kikazi na kimaisha kama alivyofanya kwa Bezaleli(Kut 31:2-5)
  • Sina hofu ya kifo – kufa kwangu ni faida (Flp 1:21). Ni faida kwa sababu nikifa nitafufuka tena na kuvishwa taji ya uzima (2 Tim 4:8), katika makao ambayo Yesu alienda kuniandalia mbinguni (Yn 14:2).
Kama huo sio utamu ni nini?
Ndugu zangu, shetani ni muongo. Anawashawishi watu wasiokoke ili wakose baraka hizo. Kuokoka sio hadithi, sio kuwa taahira — ni maisha ya ushindi, furaha na uhakika wa uzima wa milele.

Mimi nimeonja, na nimethibitisha mwenyewe kuwa kweli Bwana Yesu ni mwema! (Zaburi 34:8). Na wewe onja leo maisha ya wokovu kwa kutubu dhambi zako na kuziacha, kisha umpokee Yesu moyoni mwako kwa imani, awe Bwana na Mwokozi wako.
Safi kabisa
 
Hakika Kumwamini Yesu kuna baraka sana. 2kor 5:17, "Hata imekuwa, Mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama yamekuwa mapya". Nimeokoka nikiwa mwanafunzi wa sekondari O'level, na sasa ni zaidi ya miaka 25, ninauona wema wa Mungu maishani mwangu. Yesu yu karibu kurudi, fanya hima ndugu kuokoka, kabla neema hii haijafungwa.
Outstanding. Huo ni ushuhuda msafi kabisa. Miaka 25 unakula utamu. Wow, shuhuda za namna hii shetwani hapendi watu wazisikie. Lakini leo tumemwaibisha. Mungu akubariki sana ndugu yangu kwa ku-share jinsi unavyouona wema wa Mungu tangu O-level. Hakika kila amwaminiye Mwana wa Mungu anao ushuhuda (1 Yohana 5:10). Haleluya!
 
Upo duniani au umeshakwenda mbingu?
Nipo duniani ndugu yangu. Nikiingia mbinguni sitakuwa na mawasiliano tena na wewe. Mungu amenituma nikuambie wewe na wengine, uzuri wa kuokoka: Unabarikiwa hapa duniani na mbinguni utapata raha ya milele. Usikawie kuokoka. Yesu akirudi kabla hujaokoka, utalia na kusaga meno, maana utaachwa katika dhiki kuu ambayo haijawahi kuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
 
....na kuhuzunisha.
Acha shetwani ahuzunike tu, ni halali yake. Amewadanganya sana watu. Sasa ni wakati wa kufumbuliwa macho. Ni wakati wa kuijua kweli, kwamba kuokoka ni jambo lenye baraka na sio huzuni
 
Your curt repudiation, though perhaps cathartic to your own inclinations, is the rhetorical equivalent of attempting to eclipse the sun with a thimble. The transformative veracity of salvation is neither contingent upon your concurrence nor susceptible to the erosion of casual derision; it is self-authenticating, anchored in an immutable ontological constancy that transcends the ephemeral tides of human opinion. But alas, one cannot fault the blind for failing to appreciate the sunrise.
 
Your curt repudiation, though perhaps cathartic to your own inclinations, is the rhetorical equivalent of attempting to eclipse the sun with a thimble. The transformative veracity of salvation is neither contingent upon your concurrence nor susceptible to the erosion of casual derision; it is self-authenticating, anchored in an immutable ontological constancy that transcends the ephemeral tides of human opinion. But alas, one cannot fault the blind for failing to appreciate the sunrise.
Rubbish.
 
Back
Top Bottom