Jamal Malinzi, Rais wa TFF Kujiuzulu

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,400
Hakuna uzembe na upuuzi mkubwa kama uliofanywa na TFF wakiongozwa na Jamal Malinzi...

Mbwana Samata katutoa kimasomaso watanzania. Ni mchezaji pekee kutoka Tanzania kupata tuzo kama hii... Cha ajabu TFF hawakuona umuhimu huo na kuacha kijana huyo kuwasili usiku wa saa nane bila mapokezi yoyote...

Je TFF ilishindwa nini kubadilisha tiketi hata kama imelipwa na CAF?... Mwesiga ulienda kufanya nini Abuja kama ulishindwa kufanya mipango midogo kama hii?

Bila aibu, Jamal Malinzi anaandika kwenye twirter eti Samata anafika saa nane usiku... Gabon wamefanya mapokezi makubwa sana kwa kijana wao na kumpa motisha... TFF wenyewe wako kimya wanagombania tu fedha za kiingilio...

Kwa hili lazima tuseme wazi, huyu Malinzi ni jipu. Na maramia "bora" Tenga angefanya jambo la maana.... Nashukuru sana watanzania kwa kukemea hatua hiyo pamoja na kumtaka Malinzi na Mwesiga wajiuzulu au wangolewe....

Kama mdau wa soka, ninatoa wito kwa Jamal na Mwesiga Kujiuzulu. Nawapa siku 14. Kama watakuwa hawajajiuzulu, nitaaitisha maandamano yasiyo na kikomo....
 
Nasubiri kauli ya mwasisi na mtaalam wa mabao ya netball bwana nipe naye
 
Ruge na malinzi hawa ni wahaya,Wao wanalowaza kwa sasa,Ni namna ya kumtumia Samata kujinufaisha.Kifupi Sama asipostuka,Watamgeuza mtaji wao.
 
Last edited:
Nchi nyingine za Afrika wanatamani Samatta angekuwa wa kwao sisi tunamchukulia kama nini sijui? TFF imeshindwa kumpa mapokezi ?
 
una uhakika hajapewa mapokezi? mmekuwa wavivu mnalazimisha mambo tuu kwani mlishindwa kwenda kumpokea?
 
Tatizo la viongozi wapiga deal, viongozi wengi wa soka na vyama vingine vya michezo wapo kwa ajili ya manufaa yao binafsi,
 
tff ile imejaa vila ugali tu hakuna lolote la maana linalofanyika zaidi ya kunywa bia na kugombania viingilio kwenye mechi za stand united.
kama tff wako serious na mpira wetu wasingekubali shujaa wetu pekee atue nyumbani saa nane usiku kama jambazi.
hii siyo sahihi kabisa kama wanatambua thamani na heshima aliyotupatia mbwana samatta hawana budi watuombe radhi watanzania na wajiuzulu mara moja.
hata yule bingwa wa mabao ya mkono sijui hakuliona hili?
 
Back
Top Bottom