Jamal Malinzi akubali kuachia ngazi TFF

Jamal Malinzi akubali kuachia ngazi TFF

Yaani baada ya kuvimbiwa hela za tff asubiri kwanza ahukumiwe ndio atoe shukrani.yani malinzi sura yke ya uwiziuwizi tu hajui soka lolote yeye aliingia hpo kwa upigaji
 
Bora bwanyenye jizi lipumzike maana limeharibu soka hadi aibu.
 
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) anayemaliza muda wake, Jamal Malinzi ametoa kauli ya kukubali rasmi kuachia kiti hicho.

Hatua hiyo imekuja kutokana na kiongozi huyo kuwekwa rumande hadi Julai 3, mwaka huu mara baada ya kusomewa mashtaka yake mahakamani jana, jambo ambalo litamfanya akose nafasi ya kuhudhuria katika zoezi la usaili wa wagombea ambalo litafungwa kesho Julai Mosi.

Malinzi amezungumza kupitia wakili wake, Aloyce Komba kwamba anawashukuru watanzania kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote akiwa Rais, na kuwataka waelewe kuwa Soka la Tanzania bila Malinzi linawezakana.

Rais huyo anayekabiliwa na mashtaka takriban 28 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kughushi nyaraka, amewataka wajumbe kuchagua mtu mwingine kwani anaamini kuwa kuna watanzania wengi wenye uwezo wa kuliongoza soka la Tanzania.

Kauli hiyo inaashiria kukubali kuachia nafasi hiyo, ikizingatiwa pia mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Revocatus Kuuli alikwishaweka msimamo kuwa mchakato wa uchaguzi hautasimama, na kwamba yeyote ambaye hatatokea kwenye usaili atakuwa amejiengua mwenyewe.
nachowaza huu Uchaguzi utakua una chembechembe za HAPA KAZI TU, yaani "Mfumo" umeingilia huu uchaguzi.
Ila kama ni kwa nia njema basi haina noma, wacha tu "mfumo" ufanye kazi yake
 
huyu jamaa hafai kabisa kwenye iyo nafasi, yapasa afukuzwe mbali.
 
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) anayemaliza muda wake, Jamal Malinzi ametoa kauli ya kukubali rasmi kuachia kiti hicho.

Hatua hiyo imekuja kutokana na kiongozi huyo kuwekwa rumande hadi Julai 3, mwaka huu mara baada ya kusomewa mashtaka yake mahakamani jana, jambo ambalo litamfanya akose nafasi ya kuhudhuria katika zoezi la usaili wa wagombea ambalo litafungwa kesho Julai Mosi.

Malinzi amezungumza kupitia wakili wake, Aloyce Komba kwamba anawashukuru watanzania kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote akiwa Rais, na kuwataka waelewe kuwa Soka la Tanzania bila Malinzi linawezakana.

Rais huyo anayekabiliwa na mashtaka takriban 28 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kughushi nyaraka, amewataka wajumbe kuchagua mtu mwingine kwani anaamini kuwa kuna watanzania wengi wenye uwezo wa kuliongoza soka la Tanzania.

Kauli hiyo inaashiria kukubali kuachia nafasi hiyo, ikizingatiwa pia mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Revocatus Kuuli alikwishaweka msimamo kuwa mchakato wa uchaguzi hautasimama, na kwamba yeyote ambaye hatatokea kwenye usaili atakuwa amejiengua mwenyewe.

Mission Accomplished.
 
Back
Top Bottom