Jamal Malinzi akubali kuachia ngazi TFF

Jamal Malinzi akubali kuachia ngazi TFF

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) anayemaliza muda wake, Jamal Malinzi ametoa kauli ya kukubali rasmi kuachia kiti hicho.

Hatua hiyo imekuja kutokana na kiongozi huyo kuwekwa rumande hadi Julai 3, mwaka huu mara baada ya kusomewa mashtaka yake mahakamani jana, jambo ambalo litamfanya akose nafasi ya kuhudhuria katika zoezi la usaili wa wagombea ambalo litafungwa kesho Julai Mosi.

Malinzi amezungumza kupitia wakili wake, Aloyce Komba kwamba anawashukuru watanzania kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote akiwa Rais, na kuwataka waelewe kuwa Soka la Tanzania bila Malinzi linawezakana.

Rais huyo anayekabiliwa na mashtaka takriban 28 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kughushi nyaraka, amewataka wajumbe kuchagua mtu mwingine kwani anaamini kuwa kuna watanzania wengi wenye uwezo wa kuliongoza soka la Tanzania.

Kauli hiyo inaashiria kukubali kuachia nafasi hiyo, ikizingatiwa pia mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Revocatus Kuuli alikwishaweka msimamo kuwa mchakato wa uchaguzi hautasimama, na kwamba yeyote ambaye hatatokea kwenye usaili atakuwa amejiengua mwenyewe.
 
Malinzi katika ubora wake wa kuiua TFF
 
Safi sana malinzi, umekufa kifo kizuri. Hongera kwa "mtoa roho"
 
Yametimia......

Habari njema kwa wapenda soka nchini.....
a5186ac0041d68801bbc9e64f3785e86.jpg
e50658c2e5a0a744208abf143e310736.jpg
 
Malinzi alikuwa mchumia tumbo hana maadili ya uongozi tofauti yake na ndolanga ni kwamba ni FAT huyu TFF natamani leo leodga chila tenga arudi uongozini ,Malinzi sura imekaa kama mcheza kamari mtu asiyejiamini kabisa hakufanya chochote ndani ya TFF zaidi ya aliyoacha TENGA.
88b2c01fa88a8285b0fa5eed534e9af6.jpg
 
Maana yake ni kuwa hata asingetoa kauli hiyo, bado angekuwa keshaachia kinyang'anyiro.
 
Back
Top Bottom