Tena bora uwachukie maana wakishinda uchaguzi ujue zabuni zote zitachukuliwa na utitiri wa kampuni zao kuanzia bandari, meli, madini, ardhi, ndege, gesi na kila kitu tena watafunga mikataba ya miaka Mia na watoto wenu wote wataishia kupangiwa mishahara na watoto wao hata kama watasoma vipi lazima wapangiwe ajira na wao. Tena watoto wenu hawatamiliki chochote milele. Leo mwanao yuko huru kuibuka mtu yeyote bora juhudi zake. Tatizo wavivu wengi wanaoamini iko siku watalishwa kama ndege wakati ndege wenyewe huruka mwendo mrefu kusaka chakula mara ingine wanapatwa hata na masaibu ya ajali. Ee Mungu tunusuru na janga hili maana hizi ni dalili za shetwani katua rasmi tz. Amen.