Jamaa Amfuturu Mke wa Mtu Jioni Hii

Jamaa Amfuturu Mke wa Mtu Jioni Hii

JF2050

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Posts
2,085
Reaction score
45
Wakuu,

Nilikuwa nimesitisha kwa muda kuingia humu JF kwa ajili ya kutoa mchango wangu wa aina yoyote au kuanzisha bandiko kutokana na kuwa na kazi nyingi, lakini kwa hili nimeamua nije na kuwaandikia ili muone tulipofikia.

Majira ya saa 11 na nusu jioni nikiwa natokea eneo langu la kazi, nikakutana na vurumai njiani, watu wamekusanyika kelele nyingi, sasa ikabidi nisimame na kujionea kulikoni!

Hiki nakichukulia kama kisa kibaya zaidi kuwahi kushuhudia maishani mwangu. Kisa chenyewe ni kwamba mke wa mtu amefumaniwa na mme wake, akiwa pamoja na watu wengine, akifuturu penzi jioni hii (kwa mjibu wa mme wake huyo mke alikuwa amefunga).

Nilimshuhudia mwanaume akilia kwa uchungu usiosemekana, hasira zimempanda, akisema kwa sauti niachieni niue mtu. Bora nikafungwe maisha au ninyongwe. Watu walikuwa wamemkamata wakimfariji na kumsihi atulie.

Taarifa za awali kabla ya vurumai hilo zinadai kwamba, jamaa alishtuliwa na watu kuwa mke wake yupo kwenye kibanda fulani, ambapo huwa naona kundi la vijana wamerundikana mahali hapo; inasemekana ni studio ya muziki. Baada ya jamaa kuja na kundi la watu na kupafanyia "ambush" mahali hapo, wale wazinifu walifanikiwa kukurupuka na kutokea mlango mwingine wa hiyo studio (watu wanadai wameshtuliwa wasepe).

Ndani ya hiyo studio, wavamizi walikuta mkoba, chupi; na simu ambayo ilikuwa imezimwa. Yule mme amedai mkoba, simu, chupi na baadhi ya vitu vilivyokuwemo ndani ya mkoba ni vya mke wake. Pia amedai kumwona mke wake akitokomea na pikipiki upande wa pili na mtu ambaye hakumfahamu.

Kulikuwa na mvurugano usiokuwa wa kawaida, jamaa anaongea kwa uchungu na kudai kwamba mpango mzima wa mke wake kuzini na huyo mtu, umeratibiwa na hao vijana.

Hao vijana walikuwa wakimtia machungu zaidi kwa kurusha maneno machafu, kwamba wao hawamjui mke wake wala mtu aliyezini naye, wala yeye, halafu inakuwaje yeye anakomaa na wao badala ya jamaa aliyemmega mkewe! Nanukuu "usituzingue, acha mambo ya kifamba, kwanza we wa wapi? Yule mshikaji kaja kwetu na huyo demu ambaye sie tulijua ni mtu wake wakitaka kutengeneza nyimbo, sasa tumewakaribisha ndani chumbani, kama wamemegana sie inatuhusu nini, achana na sisi tupotezee, kama vipi kwa nini usikomae na jamaa aliyemega mkewe!".

Mme wa mama aliyefumaniwa amedai kwamba, majira ya saa saba mchana amempa mke wake hela sh 30,000/= kwa ajili ya kwenda Kariakoo kufanya manunuzi ya maandalizi ya sikukuu ya Idd; vyakula, nguo za watoto (maana amedai kuwa na watoto watatu), ikiwemo nguo za mkewe (alitaja gauni), lakini baadae, mida ya saa tisa na nusu alipewa taarifa na rafiki yake wa karibu kwamba mke wake ameonekana maeneo hayo, ndipo alipotafuta wenzake na kuamua kuja kupavamia mahali hapo.

Kulikuwa na kila dalili ya kwamba huenda umaskini ndio uliomfanya huyo mke kuasi, lakini kamwe hiyo haiwezi kuwa sababu ya msingi! Vile vile, sidhani kama huu mwezi walikuwa hawapeani mapenzi kwa sababu ya mfungo.

"I have made this letter longer than usual, because I lack the time to make it short. " —Blaise Pascal
 
Khaaaaa ukiona manyoya ujue kaliwa huyoo

"Nchi ngumu hii"
 
sasa hapo twende mbee turudi nyuma elf 30,000 kweli aende kariakoo akanunue nguo zake, za watoto, na mahitaji mengine ya Idd?

amempa mke wake hela sh 30,000/= kwa ajili ya kwenda Kariakoo kufanya manunuzi ya maandalizi ya sikukuu ya Idd; vyakula, nguo za watoto (maana amedai kuwa na watoto watatu), ikiwemo nguo za mkewe (alitaja gauni),

Ndo maana mama akaona akafuturishe mapemaaaa
 
sasa hapo twende mbee turudi nyuma elf 30,000 kweli aende kariakoo akanunue nguo zake, za watoto, na mahitaji mengine ya Idd?

Ndo maana mama akaona akafuturishe mapemaaaa

Bila shaka ni 300.000 kasahau zero moja kutokana na pressure kupanda
 
sasa hapo twende mbee turudi nyuma elf 30,000 kweli aende kariakoo akanunue nguo zake, za watoto, na mahitaji mengine ya Iddi?
Maisha bro yanatofautiana tena sana,so far huyo mwanamke ni malaya tu inaonyesha hauthamini utu wake yaani aliwe Uroda mchana live live ili aongezewe hela ya sikukuu??Na utu uzima huo bado ana idea za nguo za sikukuu?-Haya ndo madhara ya kumuoa mwanamke limbukeni na primitive (mafikirio) kimaisha

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wadau,hata kama angekuwa amepewa elfu 30,sidhani kama mke unamheshimu mmeo ndio ikawa justification ya kutoka nje ya ndoa,huo ni udhaifu binafsi wa mke,after all ni wangapi wanawake tunawaona na maisha mazuri kila kitu anapewa but bado wana misbehave out?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
dah mke kidonda jamani khaa yale pale unapopazimikia mchizi mwingine akakuja chafua duh
 
sasa hapo twende mbee turudi nyuma elf 30,000 kweli aende kariakoo akanunue nguo zake, za watoto, na mahitaji mengine ya Idd?

Ndo maana mama akaona akafuturishe mapemaaaa

Lonya lonya atapata tu tena anajaza kiloba
 
Duh! Itabidi huyo mme amtafute mwizi wake ili amle daku sasa! Si mkewe kafutariwa!
 
sasa hapo twende mbee turudi nyuma elf 30,000 kweli aende kariakoo akanunue nguo zake, za watoto, na mahitaji mengine ya Idd?

Ndo maana mama akaona akafuturishe mapemaaaa
Kaizer hiyo kwa mtanzania wa kawaida inatosha sana, mitumba ya watoto kwa kila mtoto ukijipinda sana ni 5000 so 15,000 kwa nguo na 15, 000 inayobaki ni kwa ajili ya mchele na mya,a mchanganyiko (Nyama alfu 5 au 6, mchele kilo 2 say alfu 4 na viungo vya pila 500 inatosha kabisa wajameni.

Bila shaka ni 300.000 kasahau zero moja kutokana na pressure kupanda
 
Last edited by a moderator:
Hii mbaya jamani! Haswa ukiangalia tupo kwenye mfungo wamwezi mtukufu wa ramadhani.
 
Kuna wapùuzi wameanzisha uzi kulaani CHADEMA eti haijafanya jambo. Connect the dot sasa!
 
Bila shaka ni 300.000 kasahau zero moja kutokana na pressure kupanda

wakuu, kuna watu wana shida sana, tusibeze alfu thelathini... fikiria mtu ana mshaara wa laki mbili, halafu kodi ya nyumba alfu 40, then matumizi ya kila siku nk. wapo wengi wasio hata na hizo laki mbili na wanategemea waamke wazima la sivyo paka analala jikoni

Hali ni mbaya sana na kuna kauli iliwahi kutoka kwamba siku masikini wakikosa kabisa cha kula basi watakula matajiri

namuonea huruma sana huyo aliyemegewa... waweza kuta anaishi kwa shida mawazo yake yote kwa mkewe, kumbe mkewe anaburuzwa na vibongo fleva wannabes

let us
 
Kaizer hiyo kwa mtanzania wa kawaida inatosha sana, mitumba ya watoto kwa kila mtoto ukijipinda sana ni 5000 so 15,000 kwa nguo na 15, 000 inayobaki ni kwa ajili ya mchele na mya,a mchanganyiko (Nyama alfu 5 au 6, mchele kilo 2 say alfu 4 na viungo vya pila 500 inatosha kabisa wajameni.

waweza kukuta mama alikua analia timing buku ishirini za kuongezea ili shopping iwe sawa

inasikitisha zaidi mama anapomegwa sababu ya njaa... ni bora iwe kwa tamaa yake tu
 
sasa hapo twende mbee turudi nyuma elf 30,000 kweli aende kariakoo akanunue nguo zake, za watoto, na mahitaji mengine ya Idd?

Ndo maana mama akaona akafuturishe mapemaaaa
Mkuu, zinaweza kutosha hizo na chenji ikabaki. Inategemea unanunua nguo za aina gani na mahitaji ghani.
Kwa sie tunaoishi kwa chini ya dola moja kwa siku hiyo ni ela ndefu sana

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kaizer hiyo kwa mtanzania wa kawaida inatosha sana, mitumba ya watoto kwa kila mtoto ukijipinda sana ni 5000 so 15,000 kwa nguo na 15, 000 inayobaki ni kwa ajili ya mchele na mya,a mchanganyiko (Nyama alfu 5 au 6, mchele kilo 2 say alfu 4 na viungo vya pila 500 inatosha kabisa wajameni.
MwanajamiiOne kama isingekuwa suala lako na Mbu hapa jamvini, hakyanani ningekuoa Iddi hii kumbe unajua sana bajeti aiseee

Ila jamani mi nimeona apo kwen hela tu lakini the bigger picture remains kwamba kwa nini alienda kufuturisha mchana kweupe? si angesubiri muda ufike
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom