Jama hii inawezekana katika real life situation?

Jama hii inawezekana katika real life situation?

Kaka Kapo

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2012
Posts
547
Reaction score
350
Nlikuwa naangalia sinema flani ya mapenzi (love story) ndani kunamacharacter wawili mmoje ke mwingine me. Katika kuishi kwao wakatofautiana wakawa hawako kwenye hali nzuri kwa kipindi kifupi ndani ya kipindi hicho wakiwa kwenye mvurugano ke akawa na mawasiliano na jamaa mwingine wakafikia point wakavunja amri ya sita. Ule mvurugano ukaisha then wapenzi hawa wakarudia katika hali ya kawaida me akabain kuna mawasiliano kati ya ke na Mchizi wa pembeni akachunguza chunguza akakuta ujumbe kwny simu ya ke unamwomba ke aende kwa Mchizi ths tym awe kajianda ili Wale tunda vizuri coz last tyme hawakuenjoy it was quick and ya woga! Me akamuliza ke ke akakubali akasema ni kweli alienda kwa jamaa sababu kuu nikumweleza hardtime anazoface akiwa ofisini na hayuko kwenye goodterms na jamaake kilichotokea hakuplan and anajutia na pia anaomba msamaha na hata rudia tena na anampenda sana! Baada ya kuambiwa yote hayo jamaa akampigia simu mhusika wa pembeni jamaa akamwambia kilichotokea pale hata yeye hakielewi na anaomba asamehewe na kaahidi kutomtafuta tena ke. Akamsisitiza jamaa Kuwa asimwache ke coz kweli ke anampenda! Me nae akamuuliza jamaa kama anampango nae wowote amwachie jamaa akajibu ni kweli anawaza kitu kama hicho lakini baada ya kutokea kilichotokea binti amekataa na amekuwa akisisitiza anampenda mpenzi wake so amweshimu! Story ni ndefu tuifupishe kwa kusema me aliamua kumsamehe ke wakaendelea. Nnachojiuliza je hali kama hii katika halialisi inawezekana au ndo kimuvi muvi? Si vibaya tukachangia moja mbili katika kujifunza kwa scenario kama hizi
 
^^
Labda inawezekana Dunia pana hii..
Dont tell me ni bongo movie
^^
 
Tupe jina la movie kama unaikumbuka jinale....
 
Kuna mtu wangu wa karibu alitokewa na mkasa unaendana na muvi hii, "mkewe katoka kwenda bar kupata moja baridi, moja moto bahati nzuri au mbaya baada ya kulewa akabanjuliwa na mkware mmoja, aliporudi home roho ilimsuta mpaka akamwambia mumewe kuwa alitoa uroda kwa mkware hata hawafahamiani.... mwisho wa siku alisamehewa! "..
Ni wachache wanaweza hivi...
 
Labda kwenye bongo movie kihalisia me nadhani ni imposible.
 
Hapa kuna mambo mawili au zaidi. Moja kuna suala la mwanamke kumegwa nje kwa sababu ana ugomvi na wake wa moyoni. Hii inawezekana sana tu ukizingatia kuwa wanawake mara nyingi wanapokuwa katika kipindi cha mkanganyiko wa kihisia wanakuwa so vulnerable. Ikitokea mtu akaonesha anajali na kumfariji vizuri, kuliwa mzigo sio jambo la kushangaa. Na hii inaweza kutokea hata kwa wanaume (Ni mara nyingi tu, tunasikia watu wanasema hata humu kuwa wakigombana wanatafuta nyumba ndogo za kupozea machungu yao). Ndio maana kuna jamii haziruhusu unnecessary mingling of opposite sex kwa kuwa saa nyingine mihemko kuizuia huwa ni tabu sana!

Suala la pili ni kuhusu kusamehe. Hili nalo linawezekana hususani kwa watu wa Marekani na Ulaya, lakini kwa wabongo ni tabu sana ingawa inawezekana pia.

Sasa sijajua mtoa mada ulikusudia tujadili uwezekano wa kipi hasa.
 
Kwa wanaofahamu kuwa jamii huiumba/huizaa fasihi hawawezi kubishia kuwa matukio hayo ya cheating and forgiveness yapo ndani ya jamii pia. Kunawatu wanacheat kwenye ndoa na wanasameheana
Kwa sababu Moyo wa kutotaka kusamehe umewatawala watu wengi ndio maana inaonekana kukosa uhalisia au haiwezekani kabisa.
Wandugu kumbukeni FORGIVENESS IS THE BEST REVENGE.
 
Inawezekana mtu akiomba msamaha wa dhati.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Inawezekana tena bila wasiwasi
 
Watu wanachakachua hadi wanazaa nje na wanasameheana mtoto analelewa na baba wa kambo! Kua uyaone.
 
To forgive is divine. Ili uwe na peace of mind, lakini haina maana urudiane na huyo mtu. Kwa wale ambao wana experience ya hii ishu, believe me ni ngumu. Kama movie pouwa, lakini real like there is a big difference. Been there...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom