Jakaya Kikwete kumrithi Ban Ki-Moon UN?

Jakaya Kikwete kumrithi Ban Ki-Moon UN?

Kutokana na sifa nzuri ya JK kimataifa zipo tetesi anaweza kumrithi katibu mkuu wa umoja wa mataifa bwana Ban Ki-Mooon muda wake ukiisha. JK ni kiongozi pekee kutoka nchi za dunia ya tatu mwenye mahusiano mazuri, ni rafiki mzuri wa china, marekani, ujeruman uingereza na ufaransa ambao ni watu wenye ushawishi mkubwa katika baraza la umoja wa kimataifa.

Wakati wa utawala wake viongozi wakuu wa Marekani walitumia muda wa kutosha kupumzika Tanzania ikiwemo Rais George Bush kukaa zaidi ya siku tatu Tanzania jambo ambalo halijawahi kutokea. Pia wakati wa mkutano wa kibiashara wa dunia marais watatu wa marekani walikutana Tanzania kwa mpigo jambo ambalo si la kawaida.

Katika mkutano wa china na afrika JK alionekana akitaniana na rais wa China kana kwamba anaongea na swahiba wake wa karibu huku akiwatambulisha watu mbalimbali kwa mkuu huyo wa uchina.

Kwa kuchaguliwa kuwa waziri wa mambo ya nje balozi Augustine Mahiga ambaye ni rafiki wa karibu wa Ban ni dhahiri Mahiga atalichomeka jina la JK kwa Ban Ki-Moon watakapokutana katika masuala ya kimataifa.
Acha kunywa viroba vile vinavyoitwa burudani akili yako kwishney
 
Kwani kutoka Boutous Ghali hadi Koffi Anaan ilichukua miaka mingapi?
Swali Zuri,jibu Ni Michache.Kumbuka Kipindi Hicho
Kanuni Za Kudumu Kuhusu Hii Nafasi Zilikuwa Bado Hazijawekwa.Lakini Pia Jiulize Kwa Nini Mwinyi, Mkapa Na JK Walikaa Ikulu Miaka 10 Tu Wakati Mwl Nyerere Alikaa 25yrs.
 
Labda kama UN....Wameishiwa watu .....kuziba nafasi hiyo ya ukatibu wa UN....???????????
 
We n.tahaaira kweli kwenye.nchi hii

Labda achaguliwe na.machizi.
 
Ni ngumu kwa muislamu..japo sijui kwaninh

naona safari hii kigezo hicho kinaweza faa kwani watataka kurudisha imani yao kwa waislam. ndo maana hata papa sasa hivi anatembelea misikiti.
 
Ban Ki-Moon UN wakati Tanzania yenyewe ina migogoro kule Zanzibar anajifanya kama ametia pamba za masikio? itakuwa maajabu asitufae sisi watanzania lakini akafae kwa Nchi nyengine ulimwenguni, Charity begins at Home.

BAN ki Moon anatokea kore ya kusini ambayo ina migogoro ya miaka na korea kaskazini lakini huyo kapeta katibu mkuu wa UN.

Matatizo ya Zanzibar ni ya wazanzibar wenyewe.Kikwete alikuwa Raisi wa serikali ya Muungano.Kwenye mambo ya muungano tuliyokubaliana na yaliyoko kwenye katiba ya Tanzania suala la uchaguzi wa serikali ya Zanzibar si jambo la muungano halimo kwenye mkataba wa muungano wala kwenye katiba.Hilo ni la wazanzibari wenyewe halimhusu Kikwete.Si kazi yake kulishughulikia atakuwa anaingilia mambo ya ndani ya Zanzibar.Nchi huru yenye Raisi,Makamu na baraza lao la mawaziri na wimbo wao wa Taifa wauimbao wapendapo hata baada ya kunywa urojo wakitaka.
 
Kwa udalali alioufanya wa kuuza Rasilimali zetu anaweza kuzawadiwa hiyo nafasi.Jambo pekee linaloweza kuwa kikwazo kwake katika kupata nafasi hiyo ni tabia yake ya kuishi angani kama popo.Labda UN wamjengee ofisi mwezini,lakini kama ofisi zitabaki kuwa ardhini hawezi kukubali huo uteuzi.
 
ban ki-moon un wakati tanzania yenyewe ina migogoro kule zanzibar anajifanya kama ametia pamba za masikio? Itakuwa maajabu asitufae sisi watanzania lakini akafae kwa nchi nyengine ulimwenguni, charity begins at home.

uchaguzi umehairishwa ,

ng'ombe jike
 
Upuuzi mtupu, wabongo bana wanatumia muda mwingi kuwazia wenzao madaraka wakati wao wana hali mbaya. Kwa lipi amrithi Ban?
 
Kama Kikwete kweli atamrithi Ban Ki-Moon kama UN General Secretary,itaonyesha wazi kwamba kuna jambo halikosawa kw kuwa frankly hastahili.Mambo mengine ambayo yanaonyesha kwamba kuna mambo nyuma ya pazia ni urafiki wa mashaka uliopo kati ya nchi za Ulaya,Marekani,China na Tanzania hata kupelekea Marais wa Marekani wawili wastahafu kukutana Tanzania wakati mmoja kwa mpigo na nadhani siku moja au mbili baada ya Rais Bush Juniour kuondoka Rais wa China akatembelea Tanzania.

Jambo lingine ambalo lilitia mashaka ni ziara ya Rais Bush Juniour Tanzania ambayo ilichukua takriban siku tatu.Kwa kumbukumbu zangu zinaonyesha kwamba hakuna Rais wa Marekani ambaye ameshawahi kufanya ziara kwenye nchi ya kigeni na kukaa huko siku tatu.

Niseme ukweli.Ni zuzu tu anayeweza kushangilia matukio haya,lakini kwa mtu diagnostic,haya ni matukio yenye utata.

Back
Top Bottom