Jakaya Kikwete Cardiac INS

Jakaya Kikwete Cardiac INS

drilling

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
4,905
Reaction score
5,088
Napenda nifahamu sheria zenu mwanafunzi anapokuja kujifunza kwenu mwaka 1 katoka chuo akajifunza kipindi cha miezi 6 akafanya kosa, inawezekana kufukuzwa bila kutaarifiwa wazazi wake?

Kama kafanya kosa mara ya kwanza, mnapiga simu kwa mzazi kuhusu mtoto wake kafanya kosa hili anajaribu kukanywa na mzazi, lakini mnawezaje kumfukuza bila wazazi kujua, na pia bila kumpa barua ya miezi 6 aliyofanya badala yake mnampa barua ya kumfukuza na mda wake woote miezi 6 umepotea, hamuoni kuwa mnawaumiza wazazi na pia kumfanya kijana kukata tamaa, sheria yenu ipoje?

Yupo intership akili yake bado ya kichuo na pia watoto woote hawafanani tabia. Jaribuni kumuweka sawa kwa makosa anayofanya hakuna binadamu asie kosea, na pia angalieni majungu muwe wapole kwa vijana wetu muwe na tabia ya kusamehe sio kufukuza mzazi kaanza na mtoto wake kuanzia chekechea mpaka kamaliza chuo na anakuja kujifuza aliyosemea anafanya kosa mnafukuza tu, mbona secondari mtoto akifanya kosa wazazi wanaitwa, jifunzeni kusamehe ipo siku mungu atalipa kwa watoto wenu
 
Sema mkuu kuhusu mzazi hapo napinga, huyo anachukuliwa ni mtu mzima, almost 20+ years, kwa hio anajua kipi kibaya na kizuri, atafukuzwa akiumua kukuambia sawa, akiona vibaya hatasema
 
Pole,chuoni unafukuzwa bila kumtaarifu mzazi,huko siyo sekondari au primary.
 
Pole sana mkuu. Mwanachuo si mtoto. Ana umri zaidi ya miaka 18. Anajitambua. Hivyo akienda kinyume na kanuni na sheria ndogondogo za chuo, senate inapitia prospectus tu na kufanya maamuzi. Hilo halimhusu mzazi. Hayo mengine watajua mwanachuo na mzazi wake. Anachoweza kufanya ni kuandika barua kuomba msamaha kwa senate (clemency).

Vijana wengi siku hizi wanakua kiumri tu ila kichwani, uwezo wa kupambanua mambo na kufanya maamuzi sahihi ni mdogo sana. Anapofikia hatua ya kuwa intern, huyo tunaamini ni mfanyakazi ambaye yuko tayari kutoa huduma kwa jamii. Ukisema bado ana akili za kichuochuo, sasa atakua lini kiakili?
 
kulikuwa hakuna haja ya kumfukuza ni kumrekebisha ukiisha mfukuza maana yake kazi aliyojifunza hawezi tena kupata,
 
kulikuwa hakuna haja ya kumfukuza ni kumrekebisha ukiisha mfukuza maana yake kazi aliyojifunza hawezi tena kupata,
Inawezekana kosa lake ni kubwa. Mwanachuo hawezi kufukuzwa kwa kutoingia darasani mara moja au mbili. Labda utuweke wazi. Sababu ya kufukuzwa kwake ni ipi? Ingia kwenye mtandao wao (website ya chuo), download prospectus, na usome kunakohusiana na makosa na adhabu zake. Sheria huwa ziko wazi kwa kila mtu.
 
kulikuwa hakuna haja ya kumfukuza ni kumrekebisha ukiisha mfukuza maana yake kazi aliyojifunza hawezi tena kupata,
Unaleta uchungu wa mzazi... kwenye Uhai wa watu... Kada ya afya ni kama nyeti... mwambie akasome Vitu vyengine!
 
Samahani naomba kujua kosa la mwanachuo husika na jinsia yake
 
Inawezekana kosa lake ni kubwa. Mwanachuo hawezi kufukuzwa kwa kutoingia darasani mara moja au mbili. Labda utuweke wazi. Sababu ya kufukuzwa kwake ni ipi? Ingia kwenye mtandao wao (website ya chuo), download prospectus, na usome kunakohusiana na makosa na adhabu zake. Sheria huwa ziko wazi kwa kila mtu.
Kafukuzwa intern mkuu.

Tungejua kosa ingekuwa vzr kujudge mkuu
 
Back
Top Bottom