Jakaya, ahadi ya TRL vipi?

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
24,873
11,252
Bwana JK, uliahidi kitu leo kuhusu TRL kule tabora!!! vipi ndugu yetu, when will you be reliable??
 
Bwana JK, uliahidi kitu leo kuhusu TRL kule tabora!!! vipi ndugu yetu, when will you be reliable??
Yaani we acha tu mkubwa sisi tunamsilikizia tushamzoea mzee wa ahadi nyingi zisizotekelezeka. Best hata kama hili suala litaingizwa kwenye ilani ya chama sijui kama litatekelezeka.
 
He, hivi kumbe kimya? Basi mimi nimepitia hapa nione kama kutakua na post (kuhusiana na alichosema kuwa tutajua mustakabali wa TRL alhamisi) baada ya taarifa ya habari kumbe hakukua na kitu?

Ndio shida ya rais kutoa matamshi wakati watu wa chini yake si wawajibikaji.

Bahati yake waTanzania walio wengi (nje ya miji) hata hawajui kinachoendelea na kuwa rais hatimizi ahadi, hivyo haita athiri nafasi yake ya kuchaguliwa tena!

Mtaambiwa "Alimaanisha Alhamisi ijayo!"
 
Hizo ndio siasa, akina mama tabora wamepiga makofi, akina waandishi wa bongo wamepoteza wino na mwisho wa siku tunaishia kuuma meno!!

Nimesikitika sana kwakweli...
 
Bwana JK, uliahidi kitu leo kuhusu TRL kule tabora!!! vipi ndugu yetu, when will you be reliable??

Hivi De Novo ni ahadi gani iliwahi kuahidiwa na huyu mkwere ikatekelezwa? Just enjoy your week-end acha kufuatilia hizi porojo usije ukafa kabla ya siku zako mkuu.
 
Hivi De Novo ni ahadi gani iliwahi kuahidiwa na huyu mkwere ikatekelezwa? Just enjoy your week-end acha kufuatilia hizi porojo usije ukafa kabla ya siku zako mkuu.

inauma sana lakini tukinyamaza nani atasema?
 
Wajameni ni kazi bure kutegemea huyo mtu atekeleze chochote anachosema..juzi tabora alipokuwa anahutubia siku ya wanawake alitoa ahadi ya kujenga barabara ya tabora-nzega kwa lami wenye akili wakayaacha mambo pale pale wale wasukuma/wanamwezi wanaozani atatekeleza kalagabaho..huyo jamaa ni msanii maarufu!
 
My point here ni kwamba JK aache kutufanya wajinga au mabibi ambao anaweza akaahidi chochote, achuje maneno hata kama vigelegele vitapungua!!!!!!!!!!!!
 
Hivi De Novo ni ahadi gani iliwahi kuahidiwa na huyu mkwere ikatekelezwa? Just enjoy your week-end acha kufuatilia hizi porojo usije ukafa kabla ya siku zako mkuu.
Zipo nyingi tu zimetekelezwa kama huna macho huoni na hii ya Trl saa mbili jioni baraza la mawaziri limesema haya yafuatayo:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Baraza la Mawaziri leo, Ijumaa, Machi 12, 2010, katika kikao chake kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam, chini ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limejadili hali ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na kufanya maamuzi ya msingi kwa kukubaliana kama ifuatavyo:
· Kwamba Serikali ianze mara moja kujadiliana na RITES, mbia wa Serikali katika kampuni ya TRL, kwa lengo la Serikali kununua hisa 51 za RITES katika kampuni hiyo. Kwa sasa RITES inamiliki asilimia 51 na Serikali inamiliki asilimia 49 katika TRL.
· Kwamba baada ya hapo, Serikali itafanya matayarisho ya msingi ikiwa ni pamoja na kurekebisha kasoro na kuangalia mustakabali wa TRL, na kuiandaa kampuni hiyo kwa ajili ya kutafutiwa mbia mwingine wa kushirikiana na Serikali katika kuendesha TRL.
(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU WA BARAZA LA MAWAZIRI

OFISI YA RAIS,
IKULU.

12 Machi, 2010
 
inauma sana lakini tukinyamaza nani atasema?

Usiumie bure wewe na hao wa Tabora; sioTRL tu aliiahidi pia kuimalisha shirika la ndege la ATCL na sasa imebaki ndege moja tu ambayo ikiharibika wa Kigoma itabidi waende DRC kwa boat kuhudumiwa!!!
 
Hivi katika pitapita zake zote JK hajakutana na Sir Richard Branson amshawishi kampuni yake ya Virgin iwekeze TRL?

Mambo mengine tunaona hayawezekani, lakini labda tenda zinatangazwa ambako siko.

Ninashauri yule mTanzania aliyeko kwenye ofisi ya uwekezaji ya Tanzania, London, afanye kazi yake. Ile reli ni kitu muhimu eti, unadhani watu wakipewa option ya reli kufuliwa Dar- Moshi- Arusha wataacha kupanda kama ikiwa na hadhi? Tena watapata faida tu
 
U still have hope in his promises? Mie nilikata tamaa zamani. 2006 baada ya kuona wezi, wauza unga na wala rushwa kuambiwa wajirekebishe. Labda na RITES wameambiwa wajirekebishe!
 
Zipo nyingi tu zimetekelezwa kama huna macho huoni na hii ya Trl saa mbili jioni baraza la mawaziri limesema haya yafuatayo:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Baraza la Mawaziri leo, Ijumaa, Machi 12, 2010, katika kikao chake kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam, chini ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limejadili hali ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na kufanya maamuzi ya msingi kwa kukubaliana kama ifuatavyo:
· Kwamba Serikali ianze mara moja kujadiliana na RITES, mbia wa Serikali katika kampuni ya TRL, kwa lengo la Serikali kununua hisa 51 za RITES katika kampuni hiyo. Kwa sasa RITES inamiliki asilimia 51 na Serikali inamiliki asilimia 49 katika TRL.
· Kwamba baada ya hapo, Serikali itafanya matayarisho ya msingi ikiwa ni pamoja na kurekebisha kasoro na kuangalia mustakabali wa TRL, na kuiandaa kampuni hiyo kwa ajili ya kutafutiwa mbia mwingine wa kushirikiana na Serikali katika kuendesha TRL.
(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU WA BARAZA LA MAWAZIRI

OFISI YA RAIS,
IKULU.

12 Machi, 2010

So huu ndio utekelezaji? Kutumia kodi zenu kununua hisa za hawa matapeli? No wonder waziri husika alisema huu mkataba usingevunjwa ila ungeendelea kufanyiwa marekebisho as if ulidondoka toka mbinguni.

By the way hivi sisi kama wenye nchi hatuna haki ya kujuwa ni hasara kiasi gani tumepata katika hii deal fake? Nakumbuka tuliwakopesha mara mbili hawa jamaa pesa ya mshahara. Mara ya kwanza bilioni 3 mara ya pili sikumbuki amount. Sijuwi wamekata hayo mabilioni au ndio tumeliwa kama zingine?Na je hatua gani zimechukuliwa dhidi ya hao waliotuingiza kwenye huu utumbu kama onyo kwa wengine lisitokee huko mbele ya safari?
 
Back
Top Bottom