Jaji Warioba: Sioni kwanini tusiwalipe DOWANS pesa zao....

Akiongea katika mkutano wa kufungua mpango mkakati wa TARJA, Jaji Warioba ameongea maneno yanayokanganya na kutilia shaka uweledi wake pale alipo sema haoini shida na sababu za kwanini tusiwalipe DOWANS pesa zao. Akaendelea kusema kama mahakama ambacho ndio chombo cha kutafsiri sheria kimeamua hivyo nani anayepasa kupinga?

Maoni Yangu
Huyu Mzee anaanza kupoteza weledi na anajishushia heshima yake mbele ya watanzania.

Hamna la kushangaza hapa, huyu yupo kwenye lile group la celtel au airtel, linaloididimiza TTCL.
Ndio wale wale waliovaa makoti ya kondoo kumbe ni....!
 
Hili Jambo nililisema tangu ICC ilipotoa hukumu. Kuendelea kukataa kulipa tutakuja kulipa pesa
nyingi kwasababu ya RIBA (sasa hivi zimeshafikia 111 bilioni). Kama tuna uchungu kweli na nchi
hii, tunachoweza kufanya sasa hivi, kwanza ni kuishauri serikali ilipe hilo deni haraka. Pili ni sisi
watanzania kushinikiza wale wote waliotuingiza kwenye ufisadi huu wanachukuliwa hatua za
kisheria (watuhumiwa wanafahamika, rejea tume ya Mwakyembe).

Kama yule anayetakiwa kuwachukulia hatua za kisheria watuhumiwa wote HATAKI, basi sisi wananchi
tumuwajibishe yeye kwanza. Tuache siasa tutende yale yanayowezekana na yalioyo ndani ya uwezo wetu.
 
kwanini tusiwabane hao wezi wa Dowans moja kwa moja walipe hilo deni manake ndio walikula hizo pesa, hatuhitaji serikali ilipe hilo deni bali serikali iwabane hao wezi mpaka walipe.
 
Hugo Chavez alipotaifisha sector ya mafuta nchi ilikuwa na utawala wa sheria pia, Tusifike huko cha msingi hapa mkataba huo ulikuwa fundamentally flawed na haututendei haki sisi watanzania hata kidogo. Warioba is t defending the indefensible. Kwani what happened to growing old gracefully these days?
 
Hii nchi inakua kama inaongozwa na comedians. hao walosababisha hiyo hasara wanaishi sayari gani. kama ni hii tunayoishi viumbe hai ni kwa niniwasikamtwe. Unajua gongo ni kama bangi tu huwa inakaa mwilini muda mrefu sana . Huyu mzee badala ajipumzikie mungu kamjalia ajapata hata maradhi ya figo ama ini kwa kunywa macho ya simba sasa anatetea upumbavu. kwa hiyo hata mahakama ikihalalisha ufisadi na sisi tuunge mkoo? Embu aende zake akachunge mbuzi huko kwao.
 
Jaji Warioba ni bora tu angejikalia kimya kuliko kila kukicha anajiingiza kwenye siasa uchwara za nchii.

Mahakama hizo anazoongelea tuheshimu maamuzi yake ni hizi hizi "HIGHCOURT BAZAARS" kama zinavyofahamika kwenye corridor
za wanasheria, where the highest bidder atashinda kesi yeyote ya kibiashara au Mahakama zileee za enzi za Mwalimu?

Kuliko kuonekana kituko ni bora akae kimya tu, kwani hata wanasheria wenzake ambao wanapractice wanalijua hilo na kila
Jaji siku hizi ana "price tag" yake, tatizo ni kufika bei tu.

Kwenye DOWANS wala tusijitoe akili hapa na kujifanya sheria ifuate mkondo, as if tupo RWANDA sheria inapofanya kazi,
DOWANS was and will remain DILI la watu powerful na ni HAKI na WAJIBU wa kila MZALENDO kupinga ushenzi huu.
 
Akiongea katika mkutano wa kufungua mpango mkakati wa TARJA, Jaji Warioba ameongea maneno yanayokanganya na kutilia shaka uweledi wake pale alipo sema haoini shida na sababu za kwanini tusiwalipe DOWANS pesa zao. Akaendelea kusema kama mahakama ambacho ndio chombo cha kutafsiri sheria kimeamua hivyo nani anayepasa kupinga?

Maoni Yangu
Huyu Mzee anaanza kupoteza weledi na anajishushia heshima yake mbele ya watanzania.

Hana lolote yeye aendelee kula pesa za walipa kodi, lakini tutabadili sheria inayomfanya aendelee kula pesa za walipa kodi. Katika mawaziri wakuu wabovu tuliowapata yeye, Sumaye, Msuya et al ni liability kwenye society.
 
hapa nafikiri angezungumzia suala lakuwashitaki wale wote waliotufikisha hapatulipo kuhusu sakata la dowans, na sio kukimbilia kuiilipa kampuni hewa. na hat si kuwashitaki tu balikuwafilisi mali zao zote ndani na je ya nchi walipe hilo deni.
 
Nimeisoma kwenye mwananch hii,japo anatetea utawala wa sheria,ila mahakama ni RUNGU lingne linalotumaliza
Akiongea katika mkutano wa kufungua mpango mkakati wa TARJA, Jaji Warioba ameongea maneno yanayokanganya na kutilia shaka uweledi wake pale alipo sema haoini shida na sababu za kwanini tusiwalipe DOWANS pesa zao. Akaendelea kusema kama mahakama ambacho ndio chombo cha kutafsiri sheria kimeamua hivyo nani anayepasa kupinga?

Maoni Yangu
Huyu Mzee anaanza kupoteza weledi na anajishushia heshima yake mbele ya watanzania.
 
Huo ndiyo utawala wa sheria tukianza Kupinga maamuzi halali ya muhimili muhimu Kama mahakani tunakuwa hatufuati utawala bora ambao ndiyo unafuata sheria na mahakani ndiyo inayotafsiri sheria hizo. Hi Gera mh. Warioba kwa msimamo huo najua kuna watu wataanza kusema umenunuliwa na Lowassa! Keep on the good work. Salute!
 
Mkuu ebu soma habari yote hapo chini na useme warioba amekosea wapi!

1. Mkataba muingie nyie
2. mkataba mvunje nyie
3. mkubali kwenda mahakamani
4. mahakama iamue
5. mkatae kulipa deni

THINK...The whole saga doesnt make sense at all!

sheria na siasa ni vitu viwili tofauti,deni litalipwa tu!

Warioba: Simuoni kiongozi anayepambana na ufisadi Send to a friend

Friday, 04 November 2011 21:55
0diggsdigg

AWALAUMU WATU WANAOPINGA MALIPO YA DOWANS, ATAKA MAHAKAMA ZIHESHIMIWE
Raymond Kaminyoge
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema haoni nia ya dhati kwa viongozi wa ngazi za juu wa serikalini kupambana na ufisadi badala yake, suala hilo limekuwa likizungumzwa kisiasa."Viongozi wa ngazi za juu wanazungumzia mafisadi lakini hawawachukulii hatua za kisheria, huu ni upungufu mkubwa katika utawala wetu," alisema Jaji Warioba Dar es Salaam jana alipokuwa akizindua Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Chama cha Majaji Wastaafu Tanzania (Tarja).

Warioba ambaye aliwahi kuongoza Tume ya Kero ya Rushwa wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu ya Benjamin Mkapa alisema viongozi wa Serikali wanashindwa kutofautisha masuala ya kisiasa na ya kisheria: "Sheria ni kuchukua hatua siyo kuhutubia kwenye majukwaa. Nawaasa majaji wenzangu wastaafu tujitahidi kutoa ushauri kwa viongozi na wananchi kuhusu umuhimu wa kufuata sheria," alisema.
Kauli ya Jaji Warioba imekuja kipindi ambacho jamii ya Watanzania imegawanyika kuhusu vita dhidi ya ufisadi kutokana na watuhumiwa kutofikishwa katika vyombo vya sheria kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kukosekana kwa ushahidi dhidi ya tuhuma zinazowakabili.

Dowans walipwe
Katika hotuba yake, Jaji Warioba pia alizungumzia suala la malipo ya Kampuni ya Dowans akisema Serikali inawajibika kutekeleza amri ya Mahakama kwa kuilipa kampuni hiyo ya Costa Rica na kwamba kufanya hivyo ni kuzingatia utawala bora na wa sheria lakini akataka mafisadi waliohusika wachukuliwe hatua.

Kauli hiyo ya kwanza ya Jaji Warioba kuhusu sakata hilo la Dowans imekuja kipindi ambacho Watanzania wengi wakiwamo wanaharakati wanapinga malipo hayo ya Sh110 bilioni kwa Dowans kiasi cha kutaka kuandamana kuyapinga.
Wakati wanaharakati hao wakiwamo wanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wakipinga malipo hayo, jana Jaji Warioba alitofautiana nao akisema jambo hilo si la kisiasa bali kisheria.

Jaji Warioba aliwashangaa baadhi ya viongozi wanaosimama hadharani na kupinga hukumu hiyo ya Mahakama.

Ingawa hakuwataja kwa majina, lakini viongozi wa kisiasa ambao wamekuwa wakipinga malipo hayo kwa nguvu zote ni pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe.
"Nashangaa viongozi wa nchi inayofuata utawala bora na wa sheria wanapinga hukumu iliyotolewa na Mahakama isitekelezwe, tunaonyesha mfano gani kwa jamii tunayoiongoza? Leo tunaikataa hukumu ya kesi ya Dowans, kesho haijulikani tutaikataa kesi gani, hii itatufanya tuwe na jamii ya watu wasiofuata sheria."

Warioba ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), alitoa mfano mwingine wa kesi ya uhaini katika utawala wa Awamu ya Kwanza ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere akisema katika kesi hiyo, wananchi walilalamikia adhabu iliyotolewa na Mahakama kuwa ilikuwa ndogo mno.

"Hata Serikali ilikiri kuwa kweli adhabu hiyo iliyotolewa kwa wahaini ilikuwa ndogo, lakini haikuchukua hatua ya kuikataa adhabu hiyo, iliheshimu uamuzi wa Mahakama," alisema Warioba.

Alizishangaza pia taasisi zinazojihusisha na masuala ya haki za binadamu kupinga malipo hayo kwa kampuni ya Dowans.Mahakama Kuu ya Tanzania iliisajili Tuzo ya Dowans iliyopewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara ( ICC) ya kutaka kulipwa Sh94 bilioni na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Baada ya kupitia tuzo hiyo iliyokuwa imesajiliwa na Dowans katika Mahakama hiyo, ilitoa uamuzi wa kutaka kampuni hiyo iliyorithi mkataba wa kifisadi wa Richmond ilipwe Sh110bilioni ikiwamo riba kwani hukumu ya ICC iliyotolewa Novemba, mwaka jana imezingatia masharti ya kisheria ya mkataba kati ya pande mbili.
Hata hivyo, hatua hiyo imekuwa ikipingwa vikali na kina Sitta na Dk Mwakyembe ambao wamepata nguvu ya wanaharakati ambao sasa wanaandaa maandamano makubwa nchi nzima.

Uhuru wa mahakama
Akizungumzia Mahakama, Jaji Warioba alisema chombo hicho kitakuwa huru kikipata uhuru wa kuwa na bajeti wanayoweza kujipangia wenyewe nini cha kufanya.Alisema utaratibu wa sasa wa kuomba fedha Hazina katika kila shughuli zinazotakiwa kufanywa na chombo hicho unakwamisha uhuru wake.

"Bunge liko huru kwa sababu wana bajeti yao ambayo wao wenyewe wanaigawanya kutekeleza majukumu yao, katika Katiba Mpya hilo lipewe kipaumbele," alisema.

Kuhusu Katiba Mpya, Waziri Mkuu huyo mstaafu alisema maoni ya wananchi katika uandaji wake ni ya muhimu kwa sababu wao ndiyo wenye uwezo wa kueleza ni Tanzania ya aina gani wanayoitaka.

"Lakini ukiwahoji viongozi hasa wa kisiasa kuhusu Katiba, wao watakueleza madaraka makubwa ya Rais au Tume ya uchaguzi iwe huru mambo ambayo hayawezi kumaliza matatizo ya wananchi," alisema.
Rais wa Tarja, Jaji Robert Mihayo alisema ingawa nchi inafuata misingi ya utawala bora na wa sheria, vitendo vinavyofanyika vinakiuka misingi hiyo.

Kuhusu mpango huo wa miaka mitano, Jaji Mihayo alisema utakifanya chama hicho kuwa mwelekeo mzuri wa kiutendaji. "Chama kitakuwa na ratiba ya shughuli za kufanya katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2011 hadi 20015."
Alisema hiyo itawafanya hata wafadhili wenye nia ya kukisaidia kufahamu shughuli zake ambazo alisema ni pamoja na utoaji wa ushauri na mafunzo kwa mahakimu na majaji nchini ili kuimarisha utawala bora na wa sheria.

"Unajua Hakimu akifanya kosa wakati akitekeleza majukumu yake kama vile kupokea rushwa inakuwa aibu yetu kwa sababu naye anaweza siku moja kuwa jaji ndiyo maana inabidi kuwa karibu nao," alisema Jaji Mihayo.Mpango mkakati huo umefadhiliwa na Mfuko wa Asasi za Kiraia na Taasisi ya 2000 Agenda Participation.

Wan jf habari zenu!
Kimsingi mi na mawazo tofauti kidogo na wote wanaopinga Dowans isilipwe,nchi yetu inafuata utawala kisheria,na kwa kuwa kila mhimili una kazi yake kikatiba,mahakam kuu imeshakazia hukumu ya dowans kwamba ilipwe pesa zake.

1.hapa nchini uamuzi wa mahakama unaweza kupingwa nje ya mahakama kwa mabango na maandamano?

2.mi naamini mahakama zetu bado zina reputation ndo maana hukumu zingine zinatolewa wala hakuna anayetishia kuandamana.

3.kuandamana na kupinga hukumu ya mahakama ni kukiuka katiba pia.

4.mi nadhani tusiendelee kupinga huku maamuzi ya mcingi yanabaki yaleyale,hivyo ni kuendelea kuwachangia wamiliki wa dowans riba.
hivi tukiendelea kubishana hadi deni likafika bill 130 itakuwa faida au hasara kwetu?

5.wanasheria waje na majawabu ya kuiepeuka basi si kupinga tu kimsimamao leteni solution ya naman gani hukumu ya mahakama kuu inaepukwa nje ya mahakama.
je kuna hukumu ya mahakama kuu iliyowahi kupingwa nje ya mahakama ? kama hilo linawezekana basi watu wangeandamana kupinga hukumu kama ya akina zombe kuwa si halali.
6.Tuwalipe kutekeleza hukumu ya mahakam then,tuendelee kuwatafuta waliotufikisha hapa,na wachukuliwe hatua.

MAHAKAMA NI MHIMILI HURU KAMA BUNGE NA EXECUTIVE .MAAMUZI YAKE HATA KAMA HAYAPENDEZI HAYAKWEPEKI NJE YA MHIMILI WENYEWE.
 
...hajakosea kusema hayo. Kama tutaheshimu sheria na maamuzi ya mahakama basi ni rahisi pia kuwahukumu waliotufikisha hapa.
 
Utawala wa Sheria ndiyo unataka hivyo. Je, pingamizi lililowekwa na wanaharakati lilifanikiwa mahakamani?

Unaoneka kiasi gani unapishana na sheria suala la sheria ni taaluma sio porojo za vijiweni kama unavyotaka kuleta..

Wanaharakati ndio wanaweza kuingilia hukumu ya mahakama?

Wanaharakati ni kina nani na wamelisaidia nini taifa letu zaidi ya kujipatia pesa kupitia NGO zao..zinduka wewe
 
Hatuna ujanja ndugu zangu,lazima tulipe. Tumeingizwa katika deni kubwa la bilioni 111 kwasababu ya ugomvi unaondelea kati ya makundi hasimu ndani ya CCM. Ili kama taifa tusiendelee kupoteza pesa kwa kulipia riba,hazina na tanesco wakae mara moja na dowans wakubaliane namna ya kulipa. Tusiendekeza siasa za visasi wakati mwisho ni walipa kodi wa nchi hii tutalipa deni.
 
Akiongea katika mkutano wa kufungua mpango mkakati wa TARJA, Jaji Warioba ameongea maneno yanayokanganya na kutilia shaka uweledi wake pale alipo sema haoini shida na sababu za kwanini tusiwalipe DOWANS pesa zao. Akaendelea kusema kama mahakama ambacho ndio chombo cha kutafsiri sheria kimeamua hivyo nani anayepasa kupinga?

Maoni Yangu
Huyu Mzee anaanza kupoteza weledi na anajishushia heshima yake mbele ya watanzania.

Sioni namna ya kuzuhia kuwalipa hawa watu!! kuna mmoja kasema humu kwamba
  • Mkataba tumeingia wenyewe
  • Mkataba tumehuvunja wenyewe
  • Mahakamani tumekubali kwenda wenyewe
  • Hukumu imetoka. Tuikatae?
Binafsi nashauri DOWANS walipwe ili deni lisiendelee kuongezeka.
Jambo la msingi serikali hitaifishe mali zote za waliohusika na kutufikisha hapa, kufidia pesa ya umma. Tatizo linakuja hapa, hii serikali ya magamba itakubali kufanya maamuzi magumu kutaifisha mali za washirika wao?
 
Kati ya kazi nisizoziheshimu hapa duniani kazi ya uanasheria ni mojawapo. Hii si kazi bali ni mfumo wa kihuni uliowekwa na wanadamu kufanya ovu liwe sahihi na sahihi liwe ovu. Halafu watu wanaita taaluma na wanasomea hadi PhD. Watu wangapi leo wenye haki lakini wapo pale gerezani Segerea au Ukonga kisa kuna wahuni fulani wametumia sheria na kuwafunga watu miaka mingi? Ni sawa kabisa na suala la Dowans. Wanasheria wanaungana na wanasiasa kuifilisi nchi. Na huyu babu mzee kabisa anasimama haoni aibu (maana naye ni mwanasheria na wanasheria hawana aibu) anaongea kavu kavu eti Dowans walipwe. Kwangu mimi sina shida wakilipwa poa tu nitaendelea na kazi yangu...na kazi yangu ni nzuri tu natosheka nayo. Lakini wasituaminishe kwamba hakukuwa na jinsi yoyote serikali ingeshindwa kukwepa kulipa mafisadi eti kwa sababu ya sheria fulani fulani za kibiashara. Wote tunafahamu kuwa serikali ni ya kifisadi wakitumia sheria za kifisadi kuwalipa mafisadi ambao ni wao wenyewe. Ni wanasheria tu akina Warioba wasioona hilo.
 
Tunataka sheria inayoamua kwa haki sio ujanja kama ilivyo swala la dowans! Hakuna mtu aliye juu ya sheria lkn sheria inapasa kuangalia na kuamua matakwa ya wengi, sheria ikitetea wizi na unyonyaji bado tuikubali tuu? tunasema hapana na tutaandamana mpaka kieleweke!
 
Akiongea katika mkutano wa kufungua mpango mkakati wa TARJA, Jaji Warioba ameongea maneno yanayokanganya na kutilia shaka uweledi wake pale alipo sema haoini shida na sababu za kwanini tusiwalipe DOWANS pesa zao. Akaendelea kusema kama mahakama ambacho ndio chombo cha kutafsiri sheria kimeamua hivyo nani anayepasa kupinga?

Maoni Yangu
Huyu Mzee anaanza kupoteza weledi na anajishushia heshima yake mbele ya watanzania.

ONLY83, Suala la msingi hapa si weledi ni sheria na Mzee Warioba Jaji aliyebobea na mtumishi wa Umma wa siku nyingi alisema ukweli mtupu. Mahakama imetoa hukumu inapaswa kutekelezwa. Wizi uliofanyika siyo la kisiasa ni suala la kisheria kwa hiyo wahusika walipaswa wawe wamepelekwa Mahakamani na walipaswa wawe wametumikia vifungo wanavyostahili kwa dhambi waliyoifanya ikiwa ni pamoja kufilisiwa. Mbona unashindwa kuona na kuelewa mambo ya kweli aliyoyasema Jaji Joseph Sinde Warioba? Amesema mambo yafuatayo na kwa tafsiri yangu mambo hayo ni: 1) Suala la Dowans siyo la kisiasa ni la kisheria kwa hiyo lisigeuzwe kuwa mtaji wa kisiasa, na mimi nakubaliana naye asilimia mia kwa sababu wanaopiga kelele Dowans, dowans hawajawahi hata siku moja kuwapeleka watuhumiwa wa ufisadi Mahakamani ni kelele tu za kujitafutia umaarufu wa kisiasa na hilo haliwasaidii Watanzania wenye njaa na wanaokufa kwa magonjwa. Kama wapiga kelele hawa za Dowans wako serious wangefungua mashtaka dhidi ya "watuhumiwa wa ufisadi. 2) Wahusika wapelekwe Mahakamani na sheria ichukue mkondo wake, 3) Utawala umeonyesha upungufu katika kushughulikia mambo ya ufisadi. Sasa unaposema Mhe. Jaji Warioba amekosea amekosea nini? Nimewashangaa na wengine wanasema "Gongo na uzee! Kichwa cha Mzee Warioba safi sana amesema kweli na anapaswa kupongezwa siyo kubezwa. Ila tu kama mtu hana akili ya kutafsiri anayoyasikia na anayoyasoma!
 
Wan jf habari zenu!
Kimsingi mi na mawazo tofauti kidogo na wote wanaopinga Dowans isilipwe,nchi yetu inafuata utawala kisheria,na kwa kuwa kila mhimili una kazi yake kikatiba,mahakam kuu imeshakazia hukumu ya dowans kwamba ilipwe pesa zake.

1.hapa nchini uamuzi wa mahakama unaweza kupingwa nje ya mahakama kwa mabango na maandamano?

2.mi naamini mahakama zetu bado zina reputation ndo maana hukumu zingine zinatolewa wala hakuna anayetishia kuandamana.

3.kuandamana na kupinga hukumu ya mahakama ni kukiuka katiba pia.

4.mi nadhani tusiendelee kupinga huku maamuzi ya mcingi yanabaki yaleyale,hivyo ni kuendelea kuwachangia wamiliki wa dowans riba.
hivi tukiendelea kubishana hadi deni likafika bill 130 itakuwa faida au hasara kwetu?

5.wanasheria waje na majawabu ya kuiepeuka basi si kupinga tu kimsimamao leteni solution ya naman gani hukumu ya mahakama kuu inaepukwa nje ya mahakama.
je kuna hukumu ya mahakama kuu iliyowahi kupingwa nje ya mahakama ? kama hilo linawezekana basi watu wangeandamana kupinga hukumu kama ya akina zombe kuwa si halali.
6.Tuwalipe kutekeleza hukumu ya mahakam then,tuendelee kuwatafuta waliotufikisha hapa,na wachukuliwe hatua.

MAHAKAMA NI MHIMILI HURU KAMA BUNGE NA EXECUTIVE .MAAMUZI YAKE HATA KAMA HAYAPENDEZI HAYAKWEPEKI NJE YA MHIMILI WENYEWE.

Hata UBAGUZI WA RANGI Afrika Kusini nao ulikua unatambuliwa na sheria rasmi.

Kwa hiyo si kila jambo linalotambulika kisheria linamaanisha linatoa HAKI,... We jiulize maswali machache tu haya:

Mahakama yenyewe ni iliyohukumu ni ipi: ICC

Je liliwahi fikishwa kwenye Mahakama zetu za ndani kwanza: Hapana

Je ICC ina majaji iliyowaajiri: Ndiyo

Je Jaji wa kesi ya DOWANS alikuwa mwajiriwa wa ICC: Hapana

Je alifanya kazi ya kuhukumu kwa niaba ya ICC: Ndiyo

Jiulize ICC walimpa mkataba wa kumlipa kiasi gani kwa kesi hii: UTAJAZA lakini haiwezi kuzidi USD 300,000(Kama "Consultation" Fees)

Kesi ilikua inasikilizwa wapi: MOVENPICK HOTEL

Kesi yenyewe ilikua ya madai ya kiasi gani: USD 64,000,000( 64 Million US Dollars)

Kulikua na Polisi au Askari wowote wa Mahakama: HAPANA

Wahusika wakuu wa kesi: DOWANS(Kampuni Binafsi) Vs TANESCO( Shirika la UMMA- a.k.a HALINA MWENYEWE)

Huyu "jaji" alipatikanaje : UTAJAZA Mwenyewe

SASA KWA MAZINGIRA HAYO JUU HEBU OTEA "JAJI" ATATOA HUKUMU GANI.

Then unashauri watanzania tukakodishe bendi na matarumbeta kusherehekea hukumu hiii iliyotolewa katika mazingira
ya kishenzi kama haya.

YOU NEED YOUR HEAD EXAMINED BY A PSYCHIATRIST ASAP!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom