Jaji Warioba: Sioni kwanini tusiwalipe DOWANS pesa zao....

Japo alichokisema ktk misingi ya ksiheria yupo sahihi lakini nachelea kupingana naye kwa kuwa wananch ndo walipaji wakuu wa deni hlo kupitia kodi zetu na siku zote katiba ambayo imebeba sheria zote ipo haipo juu ya wananchi hvyo kupitia umoja wetu tunaweza kuzuia malipo haya dhalimu kwa mafisadi wachache wa nchi hii.HUu ni mtizamo wangu finyu wa mawazo ambao haufungamani na upande wa kisheria kwenye shubiri hii ya dowans
 
Hapa napenda tena kuongeza neno la ziada kwamba Serikali ya Tanzania na vyombo vyake vya kiutendaji imepoteza umakini wake na ndicho kinachosababisha mabilioni hayo yote (nisiyotaka kutamka) yalipwe. Serikali ya Danganyika haina budi kulipa fedha hizo maana iliingia mkataba kijinga-jinga ama kwa rushwa waliyopokea wahusika waliosaini mikataba hiyo. Ndiyo maana nakubaliana na Mhe. Jaji Warioba kwamba Dowans awe yupo ama hayupo, awe fisadi asiwe fisadi walipwe halafu mafisadi wakamatwe mara moja wapelekwe Mahakamani na ikiishathibitika wameiba waende magereza NA KUFILISIWA. Hapo ndio nitaamini wanaopiga kelele kwenye majukwa ya siasa wako serious otherwise it craaaaaaaaap! And this nonesense of politicizing "ufisadi" should end immediately. Wanasiasa wasituzuge hapa kwa ujanja ujanja wa kutafuta umaarufu. Kama kweli wana uchungu na Watanzania wafungue kesi Mahakamani wakishinda hawa watuhumiwa wa ufisadi wanazo pesa zitalipwa kwani Mahakama itawaamuru walipe hizo pesa kama ambavyo imeamuru Dowans ilipwe. Unafiki hautatufikisha mahali popote. Siwaamini wanasiasa wapiga kelele bila vitendo. Wafanye haraka kuwafungulia mafisadi kesi Mahakamani!
 
Yeye alijilipa kupitia Mwananchi Gold hivyo haoni tatizo kwanini na hao wengine wasilipwe.

Kwa wale ambao wamesahau kilichotokea someni hapa chini. Fedha ya Watanzania imepotezwa kwenye mradi ambao haukukamilika:

Tanzania embarks on value addition to gold exports

2005-12-02 08:50:40
By Patrick Kisembo
Tanzania’s S earnings from the mineral sector are set to soar following the inauguration of the first gold refinery in the country.
It will be charged with value-addition to the country’s gold exports, hitherto exported raw.
The refinery targets small-scale miners who, without a definite market, have been loosing out to middlemen and businessmen in the black market.
President Benjamin Mkapa officially opened Mwananchi Gold Company Limited, located at Vingunguti Industrial Area, Dar es Salaam, yesterday.
Speaking at the inauguration of the refinery, the chairman of Mwananchi Gold Company Ltd board of directors, Justice Joseph Sinde Warioba, told the gathering that artisanal miners have been operating in a fiercely competitive business environment, which most of the time undermined their earnings.
’Small-scale miners are faced with a lot of problems in the same way as small-scale farmers do. They lack the necessary expertise in mining as well as having limited capital to run their businesses,’ Justice Warioba said.
He added: ’They also lack proper facilities and a reliable market to sell their ware.’
Justice Warioba commended the government for putting in place good policies to govern the mining sector. He said the policies would in the long run boost their returns.
’Our objective now is to buy 99.999 per cent to 100 per cent of the gold mined in the country at very attractive prices and refine them to finished product before exporting it as processed gold.’
Warioba stressed that the aim of the company was to help small-scale miners.
’As the company grows and expands, commercial miners would be invited, but as of now, we want to assist artisanal miners first,’ he said.
Justice Warioba said that efforts were being made to educate artisanal miners of the company’s objectives.
He said that the core responsibility of the firm would be to break vicious cycle of middlemen who defraud small-scale miners of income.
The company’s managing director, Isaac J. Manyalla, said that gold production and exports make up a significant proportion of the country’s exports.
’Production and export of gold from Tanzania at present is estimated to be 50 tonnes, valued at $700 million, per year compared with three tonnes per annum in 1995,’ he said.
Last year, he said, the mineral sector ploughed an estimated 20bn/- in social development projects.
Manyalla said that, at present, Tanzania ranks third to South Africa and Ghana in Africa in gold business.
He added that, although production of gold had increased substantially, the contribution of local small- and medium-scale miners had remained negligibly small.
’All along, the small-scale miners have not had a reliable window to sell the small quantities they get. As a result, most of the small and medium scale production is not included in government revenue,’ he noted.
He added that the meagre amounts earned through risky and exhausting manual work fetch lower prices for the miners and inevitably, find their way into the international market clandestinely.
’When you export unfinished products you loose not only in terms of lower prices, opportunities for job creation and revenue, but also other precious minerals that are usually by-products of the targeted minerals,’ he emphasised.
Deputy Minister for Minerals and Energy Dr Ibrahim Msabaha said that the inauguration of refinery would hasten the development of the mineral sector.
’We need to get more investors and miners in the sector to create more jobs, increase national income as well as fight poverty,’ Dr Msabaha said.
He said further that since 1995 commercial and small-scale miners have invested more than $2.5 billion in the sector.
’And all we need is to add value to the minerals to enable Tanzanians to own mineral areas and to ensure that all people around mining areas benefit from the business,’Dr Msabaha said.
The government owns 35 per cent of the 80 per cent owned by Tanzanians, while the rest belongs to a consortium of Tanzanian companies under the umbrella of Mwananchi Trust.
The company is incorporated in Tanzania, although it is owned by Italian shareholders who own the remaining 20 per cent.
SOURCE: Guardian
 
Ulitaka apinge kishabiki kama chadema wanavyofanya?.
Nadahan Hapa Great Thinkers Wamepungua!! Kwa Tafakuru ya Haraka Jaji Warioba alikuwa anajitahidi Kusema kuwa Kama Mtu ukipanda Bangi au Zabibu Usitegemee Kuvuna Zao Jingine Ila Utavuna Zao Hilo hilo!! Hivyo sisi Katika Taifa tumepanda zao la ufisadi tusitegemee Kuvuna zao Jingine tuendelee kutegemea kuvuna ufisadi!! Hivyo Dowans/Richmond ni zao la Ufisadi kwa nini sasa tuyakimbie Mavuno???
 
kuna kitu lazima tuige kutoka katika mataifa makubwa kama marekani, wao wanafuata utawala wa sheria lakini ikitokea mtu au kampuni imedhurumu rasilimali au fedha za marekani , na walipopeleka mahakamani wameshindwa basi jawabu ni dogo tu mlipeni mtu huyo au kampuni hiyo bila wasiwasi. baada ya kumlipa mtu huyu serikali inatoa order kwa kitengo maalum ndani ya CIA ambacho kazi yake ni kuifuatilia hii kampuni na kuhakikisha serikali inarudisha fedha zote na faida ikiwemo kuweka mitego kwenye ukwepaji kodi , au ikishindikana ni kufanya ujambazi wa kutumia peni na mitandao kwenye akaunti za kampuni hii

lazima Taifa lianzishe kitengo ndani ya usalama wa taifa kitachoshughulika na kampuni hizi zinazochota pesa za watanzania bila ya kuvuja jasho. ikiwezekana tuweke mitego nasi kwenye kodi, kuiba kwenye akounti za kampuni hizi na ikishindikana kabisa basi ni kuua watuhumiwa hawa kwa siri kwani mali ya taifa haiwezi kupotea kijinga kiasi hiki
 
@Alwatan. Mkuu inaonyesha hujui kwanini kesi ilipelekwa ICC. Tumejadili sana hapa kwamba tatizo la mkataba wa Dowans ulisainiwa kinyume na sheria zetu za manunuzi. Lakini umeme wao tumetumia. Ina maana tuliubariki huo mkataba na mapungufu yake. Ikiwa imebakia miezi 3 mkataba uishe akina Sitta wakalazimisha uvunjwe. Kwasababu tulikua tumekubaliana sheria zitakazotumika ni za ICC,Dowans wakaenda huko. Kesi imefanyika hapa,tumeshindwa. Mahakama yetu imesajili tozo,bado baadhi yetu tunapinga kulipa,huku riba ya deni ikiongezeka. Mitambo imeuzwa kwa Wamerekani,wanazalisha umeme,wanatuuzia,wanatengeneza faida wanarudisha kwao. Lakini Tanesco shirika letu lilipotaka nunua hiyo mitambo,hawa wanasiasa uchwara wanaopinga tusilipe walikataa. Sasa kama siyo chuki na visasi ambavyo vinazidi kuongezea deni sisi wananchi ni nini? Sisi tunapokua gizani,mashujaa wa kupinga malipo wamewasha jenereta zinazonunuliwa na kuendeshwa kwa kodi zetu.
 
Akiongea katika mkutano wa kufungua mpango mkakati wa TARJA, Jaji Warioba ameongea maneno yanayokanganya na kutilia shaka uweledi wake pale alipo sema haoini shida na sababu za kwanini tusiwalipe DOWANS pesa zao. Akaendelea kusema kama mahakama ambacho ndio chombo cha kutafsiri sheria kimeamua hivyo nani anayepasa kupinga?

Maoni Yangu
Huyu Mzee anaanza kupoteza weledi na anajishushia heshima yake mbele ya watanzania.

wana JF
Namwelewa sana Jaji Warioba. Kwa misingi na macho ya kisheria ni dhahiri ameegemea kulinda heshima na hadhi ya mhimili mahakama. Nahisi anahofu pia kujenga Precedence kuwa iwapo maamuzi ya mahakama yanaweza kupingwa kwa maandamano basi tumejenga msingi hatari tuendako. Lakini anapungukiwa:
i. Hasemi tufanye nini hao walioandaa mikataba mibovu ambayo ndio msingi wa Tozo ya ICC na hatimaye mahakama yetu.
2. ICC na hata mahakama haitaji kinagaubaga Dowans ni nani hasa. Warioba hajatuambia nani hasa analipwa. Au yu tayari tulipe kampuni hewa?
3. ICC yenyewe imeona utata kwenye role ya Rostam Aziz. Tulipe bila kusolve hi puzzlee.
Warioba una nafasi changia kuokoa taifa. Tunaangamia.
 
Daktari.

heshima kwako. kwanza nikupe uhakika kwamba mimi na familia yangu ni wanachama hai wa chama chako na tutaipinga ccm mpaka kufa.

huyo babu siku hizi kashikwa masikio. anapewa high table kila palipo na hafla inayohusu wakubwa. anatumika sana hasa pale Mlimani. Lakini mwambieni mzee mwenzenu...it's too late.

sisi tunamshangaa mtu mzima kutukashifu vijana ati tumekosa uzalendo, uzalendo kwa nani?
 
Waziri mkuu wa kwanza duniani kunywa gongo pombe haramu kisheria huku akiwa anatumikia cheo cha waziri mkuu, utuambie mahakama gani inafanyika kwenye chumba cha hoteli tena kimyakimya, chumba chenyewe wamelipiwa na dowans mmoja wa wahusika wa kesi, halafu utegemee maamuzi yao waliyotoa yatende haki. Huyu ni mmoja wa vilaza walio bebwa na Nyerere.
 
Utawala wa Sheria ndiyo unataka hivyo. Je, pingamizi lililowekwa na wanaharakati lilifanikiwa mahakamani?

mhhhhhhhh! wengine tuko nyuma sana, yaani ni kama tunakuwa watu wa matukio tu, baada ya hapo tunakuwa wagumu kufuatilia mambo.

Yaani muda wote tunataka kushtuliwa kwa mambo ya nyuma tu!
 
Unaoneka kiasi gani unapishana na sheria suala la sheria ni taaluma sio porojo za vijiweni kama unavyotaka kuleta..

Wanaharakati ndio wanaweza kuingilia hukumu ya mahakama?

Wanaharakati ni kina nani na wamelisaidia nini taifa letu zaidi ya kujipatia pesa kupitia NGO zao..zinduka wewe

Ritz you should have read my post between the lines, otherwise i can not tell the difference between you and the one i tried to reach.
 
mhhhhhhhh! wengine tuko nyuma sana, yaani ni kama tunakuwa watu wa matukio tu, baada ya hapo tunakuwa wagumu kufuatilia mambo.

Yaani muda wote tunataka kushtuliwa kwa mambo ya nyuma tu!

Sijakusoma.
 
wana JF
Namwelewa sana Jaji Warioba. Kwa misingi na macho ya kisheria ni dhahiri ameegemea kulinda heshima na hadhi ya mhimili mahakama. Nahisi anahofu pia kujenga Precedence kuwa iwapo maamuzi ya mahakama yanaweza kupingwa kwa maandamano basi tumejenga msingi hatari tuendako. Lakini anapungukiwa:
i. Hasemi tufanye nini hao walioandaa mikataba mibovu ambayo ndio msingi wa Tozo ya ICC na hatimaye mahakama yetu.
2. ICC na hata mahakama haitaji kinagaubaga Dowans ni nani hasa. Warioba hajatuambia nani hasa analipwa. Au yu tayari tulipe kampuni hewa?
3. ICC yenyewe imeona utata kwenye role ya Rostam Aziz. Tulipe bila kusolve hi puzzlee.
Warioba una nafasi changia kuokoa taifa. Tunaangamia.
Dr.W. Slaa.

Pole na majukumu ya ujenzi wa taifa..kama mtanzania nakuuliza swali utuweke wazi humu jamvini..

Tutajie wewe Dowans ni nani nimepata kukusoma kwenye magazeti ukisema kauli tofauti kuhusu Dowans,

Kwanza ulisema mmiliki wa Dowans ni JK..

Baadae ukasema mmiliki ni Rostam..

Dowans ilivyouzwa umekaa kimya, ujasema chochote, Jaji Warioba kashindwa kumtaja mmiliki wa Dowans,

Tuambie wewe nani mmiliki wa Dowans ni nani?
 
Mkuu kama tulitumia umeme uliyo zalishwa na mitambo hiyo ni wajibu wetu kulipa, na sioni popote Jaji Warioba alipokosea kutoa matamshi hayo, cha muhimu hapa ni TANESCO na DOWANS wakae chini wahafikiane jinsi ya kulipana na sisi tusiwe matapeli kwa kutoa visingizio vya kutowalipa wakati walikuwa wanazalisha umeme wa uhakika na mitambo yao haikuwa na walakini wowote kiufundi - watu wa kulaumiwa katika sakata zima hili na wale walioandika mkataba ya ajabu kwa kukosa kusoma small prints za mikataba hiyo, tatizo liko kwetu sisi watanzania siyo mfanya biashara.

Hivi kweli TANZANIA hii hakuna weledi wa kutafuta bei alisi ya mitambo hiyo kutoka viwandani, gharama za usafirishaji kwa ndege mitambo yenyewe kuja Tanzania na handling charges zote, capacity charge za kweli zisizo za kutunga; wakajumlisha yote hayo,alafu wakam-confront mfanya biashara aliye leta mitambo hiyo nchini na facts and figures hizo hili waweze kuhafikiana kwenye muhafaka wa kulipana bila kuzidiana ujanja wala mizengwe. Mimi swala hili huwa naliona ni dogo sana kulimaliza, lakini watu wengine wanaliona kama ni mtaji wa kujinadi kisiasa na kuwasema sema vibaya wengine especially JK.

Mkuu unachemka! Hawa dowans na Richmond walijua kabisa kuwa walikuwa wanashirikiana na watendaji wetu mafisadi kuwahujumu watanzania kwa kujipatia malipo zaidi ya uhalisia. Kama tutakubaliana na mafisadi wetu kushirikiana na wafanyabiashara kuhujumu uchumi wetu kwa kujitengenezea malipo yaLiyozidi viwango halisi basi tutakwisha.

Sisi kama wananchi hatupashwi kulipa deni hilo maana hatukutumia umeme kipindi kile mkataba umevunjwa maana hele inayodaiwa ni ile hasara waliyoipata kwa kuvunja mkataba.

Wao wadaiane na mafisadi wenzao ndo walipe hizo pesa lakini si kodi ya wanatzania. Kuna mikataba mingapi ambayo tunauhakika hata kesho akiingia Raisi mwadilifu ataivunja pasipo kujali consequence zake? Mkataba kama ya IPTL na songas ni mifano tu. Hata wale walioko kwenye ICC wanahukumu kisheria lakini wangeangalia pia haki za binadmu wangeihurumia hii nchi namna inavyonyonywa kwa kupitia mafisadi wake yenyewe.

Mkuu achana na sheria haitakaa imtendee haki binadamu masikini maana sheria siku zote huwanufaisha wenye pesa. Cha msingi ni kuangalia haki za binadamu na ndiyo maana tume ya haki za binadamu inalichukuwa Jambo hili ni hujuma dhiki ya haki za bidamu watanzania masikini wanaoteseka huku watu wachache wanaingia mikataba ya kuwaumiza wananchi masikini. Hili jambo si kuliangalia kisheria maana sheria haitaweza kwenda mbali na kuangalia Kama mkataba ulikuwa kandamizi Bali inaishia kuangalia ilimradi pande mbili ziliridhia mashariti.

Sisi wananchi tunayo haki ya kuukataa huu mkataba ambao serikali iliingia kwa niaba yetu pasipo kutushirikisha au kuangalia masilahi yetu. Kwa kuwa waliingia mkataba huu ili wafaidike wao basi ni sharti pia wawajibike katika hili na sikuwatwika wananchi mzigo usiokuwa wao.
 
Dr.W. Slaa.

Pole na majukumu ya ujenzi wa taifa..kama mtanzania nakuuliza swali utuweke wazi humu jamvini..

Tutajie wewe Dowans ni nani nimepata kukusoma kwenye magazeti ukisema kauli tofauti kuhusu Dowans,

Kwanza ulisema mmiliki wa Dowans ni JK..

Baadae ukasema mmiliki ni Rostam..

Dowans ilivyouzwa umekaa kimya, ujasema chochote, Jaji Warioba kashindwa kumtaja mmiliki wa Dowans,

Tuambie wewe nani mmiliki wa Dowans ni nani?

Ritz
nashauri utafute kama hujapata Tuzo ya ICC naamini inajieleza kuhusiana na maswali yako. Sina tabia ya kutoa kauli pale ambapo nimeisha kutolea kauli.
 
Ndugu zangu; sidhani kama kuna mtu yeyote anayepinga DOWANS kulipwa kwa kuwa tu anapinga! Sheria imewekwa na ni lazima iheshimiwe na ifuatwe na kila mtu. Sidhani kama wanaharakati, wananchi, na wadau wengine wanapinga kwa kuwa tu wameamua kupinga au wana chuki (wivu wa kike) na DOWANS.

Hoja kuu katika sakata hili ni: WALIOCHANGIA KUINGIZA TAIFA KATIKA MKATABA HUO WA AJABU WALIPE DENI NA WAWAJIBISHWE. Tatizo kuu la nchi yetu ni watendaji wanofanya madudu kutowajibika au wajibishwa. Jaji Warioba sio kwamba hajui yote haya ila naamini ameongea aliyoyaongea kwa malengo maalumu.
 
Hata UBAGUZI WA RANGI Afrika Kusini nao ulikua unatambuliwa na sheria rasmi.

Kwa hiyo si kila jambo linalotambulika kisheria linamaanisha linatoa HAKI,... We jiulize maswali machache tu haya:

Mahakama yenyewe ni iliyohukumu ni ipi: ICC

Je liliwahi fikishwa kwenye Mahakama zetu za ndani kwanza: Hapana

Je ICC ina majaji iliyowaajiri: Ndiyo

Je Jaji wa kesi ya DOWANS alikuwa mwajiriwa wa ICC: Hapana

Je alifanya kazi ya kuhukumu kwa niaba ya ICC: Ndiyo

Jiulize ICC walimpa mkataba wa kumlipa kiasi gani kwa kesi hii: UTAJAZA lakini haiwezi kuzidi USD 300,000(Kama "Consultation" Fees)

Kesi ilikua inasikilizwa wapi: MOVENPICK HOTEL

Kesi yenyewe ilikua ya madai ya kiasi gani: USD 64,000,000( 64 Million US Dollars)

Kulikua na Polisi au Askari wowote wa Mahakama: HAPANA

Wahusika wakuu wa kesi: DOWANS(Kampuni Binafsi) Vs TANESCO( Shirika la UMMA- a.k.a HALINA MWENYEWE)

Huyu "jaji" alipatikanaje : UTAJAZA Mwenyewe

SASA KWA MAZINGIRA HAYO JUU HEBU OTEA "JAJI" ATATOA HUKUMU GANI.

Then unashauri watanzania tukakodishe bendi na matarumbeta kusherehekea hukumu hiii iliyotolewa katika mazingira
ya kishenzi kama haya.

YOU NEED YOUR HEAD EXAMINED BY A PSYCHIATRIST ASAP!!![/QUOTE

Ungesoma mkataba wa Dowans na Tanesco na jinsi ICC inavyoendeshwa kabla ya kuandika ulichoandika! Tanesco walikubalina na dowans katika mkataba waliosaini kuwa kama kutakuwa na matatizo katika mkataba basi wapelekana ICC, Tanesco ilikuwa na uharaka gani wa kuvunja mkataba ambao ulishatekelezwa kwa asilimia themanini? Tumia akili yako acha kutumia za wanasiasa!!
 
Hapa napenda tena kuongeza neno la ziada kwamba Serikali ya Tanzania na vyombo vyake vya kiutendaji imepoteza umakini wake na ndicho kinachosababisha mabilioni hayo yote (nisiyotaka kutamka) yalipwe. Serikali ya Danganyika haina budi kulipa fedha hizo maana iliingia mkataba kijinga-jinga ama kwa rushwa waliyopokea wahusika waliosaini mikataba hiyo. Ndiyo maana nakubaliana na Mhe. Jaji Warioba kwamba Dowans awe yupo ama hayupo, awe fisadi asiwe fisadi walipwe halafu mafisadi wakamatwe mara moja wapelekwe Mahakamani na ikiishathibitika wameiba waende magereza NA KUFILISIWA. Hapo ndio nitaamini wanaopiga kelele kwenye majukwa ya siasa wako serious otherwise it craaaaaaaaap! And this nonesense of politicizing "ufisadi" should end immediately. Wanasiasa wasituzuge hapa kwa ujanja ujanja wa kutafuta umaarufu. Kama kweli wana uchungu na Watanzania wafungue kesi Mahakamani wakishinda hawa watuhumiwa wa ufisadi wanazo pesa zitalipwa kwani Mahakama itawaamuru walipe hizo pesa kama ambavyo imeamuru Dowans ilipwe. Unafiki hautatufikisha mahali popote. Siwaamini wanasiasa wapiga kelele bila vitendo. Wafanye haraka kuwafungulia mafisadi kesi Mahakamani!

Wanansiasa wenyewe hawana jipya! Kila siku dowans dowans, twiga wanatoroshwa wao na dowans, madini yanaibiwa wao na dowans! Grrrrrrrrr!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom