Jaji Warioba: Sioni kwanini tusiwalipe DOWANS pesa zao.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Warioba: Sioni kwanini tusiwalipe DOWANS pesa zao....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Nov 5, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Akiongea katika mkutano wa kufungua mpango mkakati wa TARJA, Jaji Warioba ameongea maneno yanayokanganya na kutilia shaka uweledi wake pale alipo sema haoini shida na sababu za kwanini tusiwalipe DOWANS pesa zao. Akaendelea kusema kama mahakama ambacho ndio chombo cha kutafsiri sheria kimeamua hivyo nani anayepasa kupinga?

  Maoni Yangu
  Huyu Mzee anaanza kupoteza weledi na anajishushia heshima yake mbele ya watanzania.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Gongo + kuzeeka vibaya
   
 3. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Utawala wa Sheria ndiyo unataka hivyo. Je, pingamizi lililowekwa na wanaharakati lilifanikiwa mahakamani?
   
 4. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu kama tulitumia umeme uliyo zalishwa na mitambo hiyo ni wajibu wetu kulipa, na sioni popote Jaji Warioba alipokosea kutoa matamshi hayo, cha muhimu hapa ni TANESCO na DOWANS wakae chini wahafikiane jinsi ya kulipana na sisi tusiwe matapeli kwa kutoa visingizio vya kutowalipa wakati walikuwa wanazalisha umeme wa uhakika na mitambo yao haikuwa na walakini wowote kiufundi - watu wa kulaumiwa katika sakata zima hili na wale walioandika mkataba ya ajabu kwa kukosa kusoma small prints za mikataba hiyo, tatizo liko kwetu sisi watanzania siyo mfanya biashara.

  Hivi kweli TANZANIA hii hakuna weledi wa kutafuta bei alisi ya mitambo hiyo kutoka viwandani, gharama za usafirishaji kwa ndege mitambo yenyewe kuja Tanzania na handling charges zote, capacity charge za kweli zisizo za kutunga; wakajumlisha yote hayo,alafu wakam-confront mfanya biashara aliye leta mitambo hiyo nchini na facts and figures hizo hili waweze kuhafikiana kwenye muhafaka wa kulipana bila kuzidiana ujanja wala mizengwe. Mimi swala hili huwa naliona ni dogo sana kulimaliza, lakini watu wengine wanaliona kama ni mtaji wa kujinadi kisiasa na kuwasema sema vibaya wengine especially JK.
   
 5. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Ulitaka apinge kishabiki kama chadema wanavyofanya?.
   
 6. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Nimejitahidi mara zote kutotaka kuingia katika mkumbo ambao hauko sahihi. Mara zote tunalilia mkondo wa sheria ufanye kazi. Mkondo huo ukifanya kazi kwa kutoa maamuzi tusiyoyataka tunataka tusiutumie.

  Huu u ndumilakuwili kweli sitaki uwe sehemu ya mimi. Kwa sababu suala tayari lipo kisheria tuiachie sheria hata kama imekuwa shubiri kwetu. Tusiendelee kupigia kelele tulipoangukia, tushughulike na kilichotuangusha!

  DOWANS walipwe tena haraka tusizidishe deni ambalo TUTALILIPA TU hata tukipayuka vipi. Kuna mmoja alikuja na uchambuzi kuwa ile hukumu ya ICC haipo, ni ujanja wa wachache. Kama tunavithibitisho kweli vya hili...tuchukue hatua za kisheria kupambana...

  Sio kelele na maandamano....hayatusaidii. Wote mnaopinga isilipwe wakati mahakama imetutaka tulipe mnahoja gani hasa? Mtujuze tusiojua na iwe katika mintarafu ya kisheria, please!
   
 7. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,288
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Yeye alijilipa kupitia Mwananchi Gold hivyo haoni tatizo kwanini na hao wengine wasilipwe.
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Nov 5, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wewe ndo huna akili..makosa wafanye viongozi wen then mahakama iamue mnaanza kupinga..lipeni hizo hela ili nkome kuchagua viongozi kwa kutazama sura zao mwanana...lakini kichwani hawana kitu
   
 9. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Kisheria kitendo cha kutumia umeme waq Dowans kwa miezi ishirini na moja na kuulipia inaonyesha kuwa ratify huo mkataba, ni kiherehere gani kilichowanya muuvunje ukiwa umebaki miezi mitatu ni nini? Lazima dowans walipwe wether u like it or not! Na wote walioingia huo mkataba, waliotushauri tuuvunje lazima wawajibike.
   
 10. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #10
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  "Neno kuwajibika" wameliondoa kwenye msamiati wameweka "funika kikombe mwanaharamu apite"
   
 11. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #11
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jaji warioba, kaongea haya maneno sio kwa ushabiki kaongea kwa kejeli kwa serikali iliopo madarakani.

  Makosa yamefanywa mwanzo huko bungeni masuala ya kitaalamu unachanganya kisiasa.
  Yote haya wanasiasa ndiyo wametufikisha hapa Warioba kapiga dongo
   
 12. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #12
  Nov 5, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sasa mzee Warioba anamakosa gani?Yeye amesema ukweli na ndio ukweli wenyewe hata kama unauma!Si tulijichanganya wenyewe toka mwanzo?
   
 13. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #13
  Nov 5, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Kwanza anaheshima gani mbele ya Watanzania
   
 14. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #14
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Literature and his references are very narrow enough to say YES to everything!! Huyu babu anatakiwa aachane na masuala ya kitaifa!! wapo wazee wengi tu wanaodhani bado tuko karne ya 19!! Let the people crack their head and come out with strong arguments za kutosha. The only problem is "who is ready to sucrifice his time, life and money for this wonderful animal DOWANS"?
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Nov 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huyu mzee anaanza kuchosha watu sasa, kila kukicha yuko kwenye vyombo vya habari. Alikuwa wapi wakati hii mikataba inasukwa in the first place. Sawa na kusimamisha basi kwa nyuma.
   
 16. c

  cyberspace JF-Expert Member

  #16
  Nov 5, 2011
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 660
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35

  Kiswahili mkuu:- alisi - halisi
  Wahafikiane- waafikiane
   
 17. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #17
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Mkuu ebu soma habari yote hapo chini na useme warioba amekosea wapi!

  1. Mkataba muingie nyie
  2. mkataba mvunje nyie
  3. mkubali kwenda mahakamani
  4. mahakama iamue
  5. mkatae kulipa deni

  THINK...The whole saga doesnt make sense at all!

  sheria na siasa ni vitu viwili tofauti,deni litalipwa tu!
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Warioba: Simuoni kiongozi anayepambana na ufisadi [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Friday, 04 November 2011 21:55 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  AWALAUMU WATU WANAOPINGA MALIPO YA DOWANS, ATAKA MAHAKAMA ZIHESHIMIWE
  Raymond Kaminyoge
  WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema haoni nia ya dhati kwa viongozi wa ngazi za juu wa serikalini kupambana na ufisadi badala yake, suala hilo limekuwa likizungumzwa kisiasa.“Viongozi wa ngazi za juu wanazungumzia mafisadi lakini hawawachukulii hatua za kisheria, huu ni upungufu mkubwa katika utawala wetu,” alisema Jaji Warioba Dar es Salaam jana alipokuwa akizindua Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Chama cha Majaji Wastaafu Tanzania (Tarja).

  Warioba ambaye aliwahi kuongoza Tume ya Kero ya Rushwa wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu ya Benjamin Mkapa alisema viongozi wa Serikali wanashindwa kutofautisha masuala ya kisiasa na ya kisheria: “Sheria ni kuchukua hatua siyo kuhutubia kwenye majukwaa. Nawaasa majaji wenzangu wastaafu tujitahidi kutoa ushauri kwa viongozi na wananchi kuhusu umuhimu wa kufuata sheria,” alisema.
  Kauli ya Jaji Warioba imekuja kipindi ambacho jamii ya Watanzania imegawanyika kuhusu vita dhidi ya ufisadi kutokana na watuhumiwa kutofikishwa katika vyombo vya sheria kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kukosekana kwa ushahidi dhidi ya tuhuma zinazowakabili.

  Dowans walipwe
  Katika hotuba yake, Jaji Warioba pia alizungumzia suala la malipo ya Kampuni ya Dowans akisema Serikali inawajibika kutekeleza amri ya Mahakama kwa kuilipa kampuni hiyo ya Costa Rica na kwamba kufanya hivyo ni kuzingatia utawala bora na wa sheria lakini akataka mafisadi waliohusika wachukuliwe hatua.

  Kauli hiyo ya kwanza ya Jaji Warioba kuhusu sakata hilo la Dowans imekuja kipindi ambacho Watanzania wengi wakiwamo wanaharakati wanapinga malipo hayo ya Sh110 bilioni kwa Dowans kiasi cha kutaka kuandamana kuyapinga.
  Wakati wanaharakati hao wakiwamo wanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wakipinga malipo hayo, jana Jaji Warioba alitofautiana nao akisema jambo hilo si la kisiasa bali kisheria.

  Jaji Warioba aliwashangaa baadhi ya viongozi wanaosimama hadharani na kupinga hukumu hiyo ya Mahakama.

  Ingawa hakuwataja kwa majina, lakini viongozi wa kisiasa ambao wamekuwa wakipinga malipo hayo kwa nguvu zote ni pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe.
  “Nashangaa viongozi wa nchi inayofuata utawala bora na wa sheria wanapinga hukumu iliyotolewa na Mahakama isitekelezwe, tunaonyesha mfano gani kwa jamii tunayoiongoza? Leo tunaikataa hukumu ya kesi ya Dowans, kesho haijulikani tutaikataa kesi gani, hii itatufanya tuwe na jamii ya watu wasiofuata sheria.”

  Warioba ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), alitoa mfano mwingine wa kesi ya uhaini katika utawala wa Awamu ya Kwanza ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere akisema katika kesi hiyo, wananchi walilalamikia adhabu iliyotolewa na Mahakama kuwa ilikuwa ndogo mno.

  “Hata Serikali ilikiri kuwa kweli adhabu hiyo iliyotolewa kwa wahaini ilikuwa ndogo, lakini haikuchukua hatua ya kuikataa adhabu hiyo, iliheshimu uamuzi wa Mahakama,” alisema Warioba.

  Alizishangaza pia taasisi zinazojihusisha na masuala ya haki za binadamu kupinga malipo hayo kwa kampuni ya Dowans.Mahakama Kuu ya Tanzania iliisajili Tuzo ya Dowans iliyopewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara ( ICC) ya kutaka kulipwa Sh94 bilioni na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

  Baada ya kupitia tuzo hiyo iliyokuwa imesajiliwa na Dowans katika Mahakama hiyo, ilitoa uamuzi wa kutaka kampuni hiyo iliyorithi mkataba wa kifisadi wa Richmond ilipwe Sh110bilioni ikiwamo riba kwani hukumu ya ICC iliyotolewa Novemba, mwaka jana imezingatia masharti ya kisheria ya mkataba kati ya pande mbili.
  Hata hivyo, hatua hiyo imekuwa ikipingwa vikali na kina Sitta na Dk Mwakyembe ambao wamepata nguvu ya wanaharakati ambao sasa wanaandaa maandamano makubwa nchi nzima.

  Uhuru wa mahakama
  Akizungumzia Mahakama, Jaji Warioba alisema chombo hicho kitakuwa huru kikipata uhuru wa kuwa na bajeti wanayoweza kujipangia wenyewe nini cha kufanya.Alisema utaratibu wa sasa wa kuomba fedha Hazina katika kila shughuli zinazotakiwa kufanywa na chombo hicho unakwamisha uhuru wake.

  “Bunge liko huru kwa sababu wana bajeti yao ambayo wao wenyewe wanaigawanya kutekeleza majukumu yao, katika Katiba Mpya hilo lipewe kipaumbele,” alisema.

  Kuhusu Katiba Mpya, Waziri Mkuu huyo mstaafu alisema maoni ya wananchi katika uandaji wake ni ya muhimu kwa sababu wao ndiyo wenye uwezo wa kueleza ni Tanzania ya aina gani wanayoitaka.

  “Lakini ukiwahoji viongozi hasa wa kisiasa kuhusu Katiba, wao watakueleza madaraka makubwa ya Rais au Tume ya uchaguzi iwe huru mambo ambayo hayawezi kumaliza matatizo ya wananchi,” alisema.
  Rais wa Tarja, Jaji Robert Mihayo alisema ingawa nchi inafuata misingi ya utawala bora na wa sheria, vitendo vinavyofanyika vinakiuka misingi hiyo.

  Kuhusu mpango huo wa miaka mitano, Jaji Mihayo alisema utakifanya chama hicho kuwa mwelekeo mzuri wa kiutendaji. “Chama kitakuwa na ratiba ya shughuli za kufanya katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2011 hadi 20015.”
  Alisema hiyo itawafanya hata wafadhili wenye nia ya kukisaidia kufahamu shughuli zake ambazo alisema ni pamoja na utoaji wa ushauri na mafunzo kwa mahakimu na majaji nchini ili kuimarisha utawala bora na wa sheria.

  “Unajua Hakimu akifanya kosa wakati akitekeleza majukumu yake kama vile kupokea rushwa inakuwa aibu yetu kwa sababu naye anaweza siku moja kuwa jaji ndiyo maana inabidi kuwa karibu nao,” alisema Jaji Mihayo.Mpango mkakati huo umefadhiliwa na Mfuko wa Asasi za Kiraia na Taasisi ya 2000 Agenda Participation.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 18. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #18
  Nov 5, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Inshu ya Dowans tulishajichanganya tokea awali kwenye kusign mikataba na kuhuisha milki ya mikataba, kwa sasa vile jambo lenyewe limeendeshwa kisheria/kimahakama hakuna tunachoweza kufanya kuzuia malipo, tunaangalia tulipoangukia badala ya wapi tulijikwaa!
   
 19. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,771
  Trophy Points: 280
  Hizi gongo zinazotengenezwa kwa mayai viza zinaathiri sana mfumo wa kufikiri.
   
 20. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #20
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jf ina members wengi sana, wenye mawazo ya kila aina!

  LONG LIVE Jf!
   
Loading...