Jaji Warioba: Sioni kwanini tusiwalipe DOWANS pesa zao....

Dr.W. Slaa.

Pole na majukumu ya ujenzi wa taifa..kama mtanzania nakuuliza swali utuweke wazi humu jamvini..



Kwanza ulisema mmiliki wa Dowans ni JK..

Baadae ukasema mmiliki ni Rostam..



index.jpg

IMG_5035.JPG

bado una swali?
 
Mkuu ebu soma habari yote hapo chini na useme warioba amekosea wapi!1. Mkataba muingie nyie2. mkataba mvunje nyie3. mkubali kwenda mahakamani4. mahakama iamue5. mkatae kulipa deniTHINK...The whole saga doesnt make sense at all!sheria na siasa ni vitu viwili tofauti,deni litalipwa tu!
Warioba: Simuoni kiongozi anayepambana na ufisadi Send to a friend
Friday, 04 November 2011 21:55
0diggsdiggAWALAUMU WATU WANAOPINGA MALIPO YA DOWANS, ATAKA MAHAKAMA ZIHESHIMIWERaymond KaminyogeWAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema haoni nia ya dhati kwa viongozi wa ngazi za juu wa serikalini kupambana na ufisadi badala yake, suala hilo limekuwa likizungumzwa kisiasa.“Viongozi wa ngazi za juu wanazungumzia mafisadi lakini hawawachukulii hatua za kisheria, huu ni upungufu mkubwa katika utawala wetu,” alisema Jaji Warioba Dar es Salaam jana alipokuwa akizindua Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Chama cha Majaji Wastaafu Tanzania (Tarja).Warioba ambaye aliwahi kuongoza Tume ya Kero ya Rushwa wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu ya Benjamin Mkapa alisema viongozi wa Serikali wanashindwa kutofautisha masuala ya kisiasa na ya kisheria: “Sheria ni kuchukua hatua siyo kuhutubia kwenye majukwaa. Nawaasa majaji wenzangu wastaafu tujitahidi kutoa ushauri kwa viongozi na wananchi kuhusu umuhimu wa kufuata sheria,” alisema.Kauli ya Jaji Warioba imekuja kipindi ambacho jamii ya Watanzania imegawanyika kuhusu vita dhidi ya ufisadi kutokana na watuhumiwa kutofikishwa katika vyombo vya sheria kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kukosekana kwa ushahidi dhidi ya tuhuma zinazowakabili.Dowans walipweKatika hotuba yake, Jaji Warioba pia alizungumzia suala la malipo ya Kampuni ya Dowans akisema Serikali inawajibika kutekeleza amri ya Mahakama kwa kuilipa kampuni hiyo ya Costa Rica na kwamba kufanya hivyo ni kuzingatia utawala bora na wa sheria lakini akataka mafisadi waliohusika wachukuliwe hatua.Kauli hiyo ya kwanza ya Jaji Warioba kuhusu sakata hilo la Dowans imekuja kipindi ambacho Watanzania wengi wakiwamo wanaharakati wanapinga malipo hayo ya Sh110 bilioni kwa Dowans kiasi cha kutaka kuandamana kuyapinga.Wakati wanaharakati hao wakiwamo wanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wakipinga malipo hayo, jana Jaji Warioba alitofautiana nao akisema jambo hilo si la kisiasa bali kisheria.Jaji Warioba aliwashangaa baadhi ya viongozi wanaosimama hadharani na kupinga hukumu hiyo ya Mahakama.Ingawa hakuwataja kwa majina, lakini viongozi wa kisiasa ambao wamekuwa wakipinga malipo hayo kwa nguvu zote ni pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe.“Nashangaa viongozi wa nchi inayofuata utawala bora na wa sheria wanapinga hukumu iliyotolewa na Mahakama isitekelezwe, tunaonyesha mfano gani kwa jamii tunayoiongoza? Leo tunaikataa hukumu ya kesi ya Dowans, kesho haijulikani tutaikataa kesi gani, hii itatufanya tuwe na jamii ya watu wasiofuata sheria.”Warioba ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), alitoa mfano mwingine wa kesi ya uhaini katika utawala wa Awamu ya Kwanza ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere akisema katika kesi hiyo, wananchi walilalamikia adhabu iliyotolewa na Mahakama kuwa ilikuwa ndogo mno.“Hata Serikali ilikiri kuwa kweli adhabu hiyo iliyotolewa kwa wahaini ilikuwa ndogo, lakini haikuchukua hatua ya kuikataa adhabu hiyo, iliheshimu uamuzi wa Mahakama,” alisema Warioba.Alizishangaza pia taasisi zinazojihusisha na masuala ya haki za binadamu kupinga malipo hayo kwa kampuni ya Dowans.Mahakama Kuu ya Tanzania iliisajili Tuzo ya Dowans iliyopewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara ( ICC) ya kutaka kulipwa Sh94 bilioni na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).Baada ya kupitia tuzo hiyo iliyokuwa imesajiliwa na Dowans katika Mahakama hiyo, ilitoa uamuzi wa kutaka kampuni hiyo iliyorithi mkataba wa kifisadi wa Richmond ilipwe Sh110bilioni ikiwamo riba kwani hukumu ya ICC iliyotolewa Novemba, mwaka jana imezingatia masharti ya kisheria ya mkataba kati ya pande mbili.Hata hivyo, hatua hiyo imekuwa ikipingwa vikali na kina Sitta na Dk Mwakyembe ambao wamepata nguvu ya wanaharakati ambao sasa wanaandaa maandamano makubwa nchi nzima.Uhuru wa mahakamaAkizungumzia Mahakama, Jaji Warioba alisema chombo hicho kitakuwa huru kikipata uhuru wa kuwa na bajeti wanayoweza kujipangia wenyewe nini cha kufanya.Alisema utaratibu wa sasa wa kuomba fedha Hazina katika kila shughuli zinazotakiwa kufanywa na chombo hicho unakwamisha uhuru wake.“Bunge liko huru kwa sababu wana bajeti yao ambayo wao wenyewe wanaigawanya kutekeleza majukumu yao, katika Katiba Mpya hilo lipewe kipaumbele,” alisema.Kuhusu Katiba Mpya, Waziri Mkuu huyo mstaafu alisema maoni ya wananchi katika uandaji wake ni ya muhimu kwa sababu wao ndiyo wenye uwezo wa kueleza ni Tanzania ya aina gani wanayoitaka.“Lakini ukiwahoji viongozi hasa wa kisiasa kuhusu Katiba, wao watakueleza madaraka makubwa ya Rais au Tume ya uchaguzi iwe huru mambo ambayo hayawezi kumaliza matatizo ya wananchi,” alisema.Rais wa Tarja, Jaji Robert Mihayo alisema ingawa nchi inafuata misingi ya utawala bora na wa sheria, vitendo vinavyofanyika vinakiuka misingi hiyo.Kuhusu mpango huo wa miaka mitano, Jaji Mihayo alisema utakifanya chama hicho kuwa mwelekeo mzuri wa kiutendaji. “Chama kitakuwa na ratiba ya shughuli za kufanya katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2011 hadi 20015.”Alisema hiyo itawafanya hata wafadhili wenye nia ya kukisaidia kufahamu shughuli zake ambazo alisema ni pamoja na utoaji wa ushauri na mafunzo kwa mahakimu na majaji nchini ili kuimarisha utawala bora na wa sheria.“Unajua Hakimu akifanya kosa wakati akitekeleza majukumu yake kama vile kupokea rushwa inakuwa aibu yetu kwa sababu naye anaweza siku moja kuwa jaji ndiyo maana inabidi kuwa karibu nao,” alisema Jaji Mihayo.Mpango mkakati huo umefadhiliwa na Mfuko wa Asasi za Kiraia na Taasisi ya 2000 Agenda Participation.
Mkuu tatizo lilianzia mbali huko nyuma ambapo serikali ikiwa inamtafuta mmiliki ili imshtaki hakujitokeza, sasa baada ya maneuvering wanaonekana kuja kudai pesa!
 
wana JF
Namwelewa sana Jaji Warioba. Kwa misingi na macho ya kisheria ni dhahiri ameegemea kulinda heshima na hadhi ya mhimili mahakama. Nahisi anahofu pia kujenga Precedence kuwa iwapo maamuzi ya mahakama yanaweza kupingwa kwa maandamano basi tumejenga msingi hatari tuendako. Lakini anapungukiwa:
i. Hasemi tufanye nini hao walioandaa mikataba mibovu ambayo ndio msingi wa Tozo ya ICC na hatimaye mahakama yetu.
2. ICC na hata mahakama haitaji kinagaubaga Dowans ni nani hasa. Warioba hajatuambia nani hasa analipwa. Au yu tayari tulipe kampuni hewa?
3. ICC yenyewe imeona utata kwenye role ya Rostam Aziz. Tulipe bila kusolve hi puzzlee.
Warioba una nafasi changia kuokoa taifa. Tunaangamia.

The president that was never be! salaam!

Naona unamtwisha mzigo Warioba bila sababu yeyote

1. AMESEMA kuwa wote walioandaa mikataba mibovu wachukuliwe hatua!

"Katika hotuba yake, Jaji Warioba pia alizungumzia suala la malipo ya Kampuni ya Dowans akisema Serikali inawajibika kutekeleza amri ya Mahakama kwa kuilipa kampuni hiyo ya Costa Rica na kwamba kufanya hivyo ni kuzingatia utawala bora na wa sheria lakini akataka mafisadi waliohusika wachukuliwe hatua"-warioba

2. Dr Slaa tafadhali usiingie kwenye mkumbo wala usiwapeleke watu kwenye hoja nyepesi...please

Nani aliwapeleka TANESCO huko ICC?
Mahakamani TANESCO walikuwa wanaendesha kesi na hewa? kivuli?
Ile kila mwezi TANESCO walikuwa wanawalipa Dowans how?

Leo hii unataka warioba ataje wamiliki au walipwa Tuzo ya dowans...nonsense!


Nyie mliosema mktaba mvunjwe , mlitakiwa kusema how we can overcome all barriers of laws..leo hii mnatapatapa tu na mnatuletea umaskini

Slaa maswali yako haya hayakuweki kwenye level yako hata kidogo, sit down think again!

NARUDIA TENA kukujulisha ujinga wangu au upumbavu wangu mimi na wewe...ni huu

1. Mkataba tumeingia sisi wenyewe
2. mkataba tukauvunja sisi wenyewe
3. tukapelekwa mahakamani tukaenda tukakubali wenyewe
4. Hukumu imekuja tunaikataa wenyewe!

Lazima kuna tatizo kwenye ubongo wako na wangu let me solve the puzzle

1. Mkataba tumeingia sisi wenyewe (how na ilikuwaje tukaweka mkataba, kulikuwa na haja?)

2. mkataba tukauvunja sisi wenyewe ( kama point 1 ni invalid basi hakuna kuuvunja mkataba, kuuvunja mkataba ni alama ya kuwepo mkataba, na kuuvunja kwake lazima sheria na condition za mkataba zingeangaliwa ili kukwepa HUKUMU..hili halikufanywa)

3. tukapelekwa mahakamani tukaenda tukakubali wenyewe (unapoenda mahakamani unategemea nini? unapoitwa kwenye kesi unatarajia nini?, hatukutakiwa kwenda mahakamani in the first place kama mkataba haukuwa sahihi)

4. Hukumu imekuja tunaikataa wenyewe! (Kuamka na kuona hukumu haifai wakati yote hapo juu tulikuwa tunayaangalia na kuhusika kikamilifu ni ujinga aidha wa kukosa uzalendo, kutokujali taifa hili na wote na SLAA huko hapa)..tueleze mbali ya kutaka mkataba uvunjwe na ulivunjwa ulifanya nini kuzuia tusilipe wakati kesi inaendelea? au haukujua kuna kesi makahamani)

Haya maswali hapo juu siyo rahisi, yanatufanya sisi kama watanzania tuonekane watu wa ajabu ajabu na kukurupuka kwa kila kitu

Warioba is right!!! otherwise abolish judiciary system!
 
Huyu Mzee atakuwa Amenunulia na Mafisadi Yaani hata MPAMBANAJI SITTA Hajamuona
 
Akiongea katika mkutano wa kufungua mpango mkakati wa TARJA, Jaji Warioba ameongea maneno yanayokanganya na kutilia shaka uweledi wake pale alipo sema haoini shida na sababu za kwanini tusiwalipe DOWANS pesa zao. Akaendelea kusema kama mahakama ambacho ndio chombo cha kutafsiri sheria kimeamua hivyo nani anayepasa kupinga?

Maoni Yangu
Huyu Mzee anaanza kupoteza weledi na anajishushia heshima yake mbele ya watanzania.

Mie nakubaliana nawe. Kama hana la maana la kusema ni bora akae kimya tu kuliko kuropoka. Huwezi kumlipa mtu ambaye alitumia uwongo ili kuhakikisha anapata mkataba toka kwako. Hawa Dowans alias Richmond waliidanganya Serikali kwamba wana utaalamu wa kufua umeme kitu ambacho hakikuwa kweli na pia HQ zao zilikuwa Houston, Texas kumbe ni kampuni iliyokuwemo katika briefcase ya fisadi Rostam
 
Akiongea katika mkutano wa kufungua mpango mkakati wa TARJA, Jaji Warioba ameongea maneno yanayokanganya na kutilia shaka uweledi wake pale alipo sema haoini shida na sababu za kwanini tusiwalipe DOWANS pesa zao. Akaendelea kusema kama mahakama ambacho ndio chombo cha kutafsiri sheria kimeamua hivyo nani anayepasa kupinga?

Maoni Yangu
Huyu Mzee anaanza kupoteza weledi na anajishushia heshima yake mbele ya watanzania.
Watanzania mnapiga kura kama vipofu, halafu mnalalama kama vichaa! Ni vema muendelee kuteseka hadi hapo mtakapopata mang'amuzi na kuondoa ushabiki wa Yanga na Simba katika siasa! Amani na utulivu! Tulieni ili mliwe vizuri kwa kuwa mliyataka wenyewe!
 
Akiongea katika mkutano wa kufungua mpango mkakati wa TARJA, Jaji Warioba ameongea maneno yanayokanganya na kutilia shaka uweledi wake pale alipo sema haoini shida na sababu za kwanini tusiwalipe DOWANS pesa zao. Akaendelea kusema kama mahakama ambacho ndio chombo cha kutafsiri sheria kimeamua hivyo nani anayepasa kupinga?

Maoni Yangu
Huyu Mzee anaanza kupoteza weledi na anajishushia heshima yake mbele ya watanzania.


Mkuu ccm uozo mtupu wanajaza matumbo yao hawatukumbuki wachovu ukiona kiongozi wa ccm anakemea ufisadi ujuwe anajianda kuiba sehemu au katoka kuiba sehem
 
Nimejitahidi mara zote kutotaka kuingia katika mkumbo ambao hauko sahihi. Mara zote tunalilia mkondo wa sheria ufanye kazi. Mkondo huo ukifanya kazi kwa kutoa maamuzi tusiyoyataka tunataka tusiutumie. Huu u ndumilakuwili kweli sitaki uwe sehemu ya mimi. Kwa sababu suala tayari lipo kisheria tuiachie sheria hata kama imekuwa shubiri kwetu. Tusiendelee kupigia kelele tulipoangukia, tushughulike na kilichotuangusha!
DOWANS walipwe tena haraka tusizidishe deni ambalo TUTALILIPA TU hata tukipayuka vipi.
Kuna mmoja alikuja na uchambuzi kuwa ile hukumu ya ICC haipo, ni ujanja wa wachache. Kama tunavithibitisho kweli vya hili...tuchukue hatua za kisheria kupambana...sio kelele na maandamano....hayatusaidii. Wote mnaopinga isilipwe wakati mahakama imetutaka tulipe mnahoja gani hasa? Mtujuze tusiojua na iwe katika mintarafu ya kisheria, please!
principle ya kwanza ya sheria ni kwamba kilicho haramu hakiwezi kutoa kilicho halali, na wenzetu wa nchi zisizoshabikia ubadhirifu nk wana pinga saana kuwepo kwa shell company na watu au ma-director kutumia njia za panya kuficha id zao, hapo ndipo tatizo la kwanza linapoanzia.
 
hapa mzee anatumia mbinu ya ccm ya siku zote kuwa na makundi matatu, moja la wezi, la pili la kati kati na la tatu wanaojifanya ni wenye niddhamu au kufuata sheria ili kuwa ghilibu wananchi kwa kupoza mambo, wakati wa mzee ruhusa walimtumia saana mrema, wakati wa mkapa walimtumia kingunge ngombale mwiru, lakini mwisho wa siku hadithi ni ile ile wizi wizi wizi, na sasa ni ujambazi na hakuna hatua zifaazo kutatua hilo tatizo
 
akiongea katika mkutano wa kufungua mpango mkakati wa tarja, jaji warioba ameongea maneno yanayokanganya na kutilia shaka uweledi wake pale alipo sema haoini shida na sababu za kwanini tusiwalipe dowans pesa zao. Akaendelea kusema kama mahakama ambacho ndio chombo cha kutafsiri sheria kimeamua hivyo nani anayepasa kupinga?

maoni yangu
huyu mzee anaanza kupoteza weledi na anajishushia heshima yake mbele ya watanzania.
sina hakika kama maana ya weredi iko sawa kwako< mind you weredi si uccm wala ucdm, na kwahili nafikiri wewe unatatizo la kiimani kwa maana imani uliyonayo inakupeleka kasi.
 
principle ya kwanza ya sheria ni kwamba kilicho haramu hakiwezi kutoa kilicho halali, na wenzetu wa nchi zisizoshabikia ubadhirifu nk wana pinga saana kuwepo kwa shell company na watu au ma-director kutumia njia za panya kuficha id zao, hapo ndipo tatizo la kwanza linapoanzia.

lakini kumbuka kutokujua sheria ktk maana ya kuandaa mikataba ya hovyo hovyo kwa upande mmoja (wataalam wetu) haiwezi kuwa sehemu ya kuonewa huruma kwa upande mwingine. Pili mahakama si wehu kutoa hukumu ile kuweni waelewa, na hapo tu ndipo dhana ya utawala wa sheria utakapofuatwa.
 
mkuu ccm uozo mtupu wanajaza matumbo yao hawatukumbuki wachovu ukiona kiongozi wa ccm anakemea ufisadi ujuwe anajianda kuiba sehemu au katoka kuiba sehem

haishangazi kwa sasa kuja na mawazo kama haya kwani hata tumeshuhudia waumini na wachungaji wao wakipelekana puta kwani tatizo ni imani kushuka baina yetu inayochangiwa na ubinafisi na roho ya wivu
 
si mlikua mnamshabikia sitta na Mwakyembe!!! lazima tulipe. wametuingiza mkenge sasa wamekaa kimya amebaki kubisha kupitia kipindi cha ITV DAKIKA 45, kama kweli sitta mwanaume aende mahakamani
 
the president that was never be! Salaam!

Naona unamtwisha mzigo warioba bila sababu yeyote

1. Amesema kuwa wote walioandaa mikataba mibovu wachukuliwe hatua!

"katika hotuba yake, jaji warioba pia alizungumzia suala la malipo ya kampuni ya dowans akisema serikali inawajibika kutekeleza amri ya mahakama kwa kuilipa kampuni hiyo ya costa rica na kwamba kufanya hivyo ni kuzingatia utawala bora na wa sheria lakini akataka mafisadi waliohusika wachukuliwe hatua"-warioba

2. Dr slaa tafadhali usiingie kwenye mkumbo wala usiwapeleke watu kwenye hoja nyepesi...please

nani aliwapeleka tanesco huko icc?
Mahakamani tanesco walikuwa wanaendesha kesi na hewa? Kivuli?
Ile kila mwezi tanesco walikuwa wanawalipa dowans how?

Leo hii unataka warioba ataje wamiliki au walipwa tuzo ya dowans...nonsense!


nyie mliosema mktaba mvunjwe , mlitakiwa kusema how we can overcome all barriers of laws..leo hii mnatapatapa tu na mnatuletea umaskini

slaa maswali yako haya hayakuweki kwenye level yako hata kidogo, sit down think again!

Narudia tena kukujulisha ujinga wangu au upumbavu wangu mimi na wewe...ni huu

1. Mkataba tumeingia sisi wenyewe
2. Mkataba tukauvunja sisi wenyewe
3. Tukapelekwa mahakamani tukaenda tukakubali wenyewe
4. Hukumu imekuja tunaikataa wenyewe!

lazima kuna tatizo kwenye ubongo wako na wangu let me solve the puzzle

1. Mkataba tumeingia sisi wenyewe (how na ilikuwaje tukaweka mkataba, kulikuwa na haja?)

2. Mkataba tukauvunja sisi wenyewe ( kama point 1 ni invalid basi hakuna kuuvunja mkataba, kuuvunja mkataba ni alama ya kuwepo mkataba, na kuuvunja kwake lazima sheria na condition za mkataba zingeangaliwa ili kukwepa hukumu..hili halikufanywa)

3. Tukapelekwa mahakamani tukaenda tukakubali wenyewe (unapoenda mahakamani unategemea nini? Unapoitwa kwenye kesi unatarajia nini?, hatukutakiwa kwenda mahakamani in the first place kama mkataba haukuwa sahihi)

4. Hukumu imekuja tunaikataa wenyewe! (kuamka na kuona hukumu haifai wakati yote hapo juu tulikuwa tunayaangalia na kuhusika kikamilifu ni ujinga aidha wa kukosa uzalendo, kutokujali taifa hili na wote na slaa huko hapa)..tueleze mbali ya kutaka mkataba uvunjwe na ulivunjwa ulifanya nini kuzuia tusilipe wakati kesi inaendelea? Au haukujua kuna kesi makahamani)

haya maswali hapo juu siyo rahisi, yanatufanya sisi kama watanzania tuonekane watu wa ajabu ajabu na kukurupuka kwa kila kitu

warioba is right!!! Otherwise abolish judiciary system!

tatizo ndugu yangu si kana kwamba dr. Slaa hayo ulosema hajui bali kanywa sumu anatakiwa atapishwe kwa kumkorogea mavi ya ngombe mabichi
 
Mimi binafsi nadhani ni TBC ambao wameikatisha hotuba yake iseme vile, vinginevyo haiingii akilini kwa mtu kama warioba kutamba yale kama ndio mtazamo wako; ninahisi kuna mkono wa mtu aliyeipanga ile clip ikae vile na kutuchanganya wengi; Judge Warioba is very sobber with what is going on, tatizo TBC hawakuweka clip yote tuelewe alikuwa anasema nini hasa.
 
Nyie watu kisheria dowans wana haki ya kulipwa na deni likikaa ndivyo linavyozidi ukubwa. Kijamii Dowans hawatakiwi kulipwa. La msingi walipwe Dowans ili tusije kuuza rasilimali zetu tukalia zaidi halafu sie tuwakamate wale wote waliohusika including akina Rostam na Lowassa, Rex Attorney kama kuna ushahidi.

Vyenginevyo deni linaongezeka siku hadi siku. Kuna jamaa amenidokeza kuwa deni sasa linafikia Bilioni 130 toka Bilioni 94. Endeleeni kubishana mwisho wa siku serikali itashindwa kumlipa huyo dowans na kuishia kuuza mbuga ya taifa ndio mtajua kwanini wengine sie tunasema walipwe waishie zao sie tumalizane na akina Rostam, Lowassa na wengineo.

Tulishasema hilo tangu ilipotolewa hukumu na ICC maandamano hayana faida kwani mtu yeyote zaidi ya mtaji wa kisiasa tu.
 
Inshu ya Dowans tulishajichanganya tokea awali kwenye kusign mikataba na kuhuisha milki ya mikataba, kwa sasa vile jambo lenyewe limeendeshwa kisheria/kimahakama hakuna tunachoweza kufanya kuzuia malipo, tunaangalia tulipoangukia badala ya wapi tulijikwaa!
Kwa sababu walijichanganya na si tulijichanganya kwa makusudi ndio maana hatutalipa
 
jamaniee...mzee wa watu yuko sahihi kabisa,na jambo lipo wazi.sisi tujilaumu kwa kuwakilishwa na wanasheria uchwara lakin deni la watu halikwepeki.
 
jamaniee...mzee wa watu yuko sahihi kabisa,na jambo lipo wazi.sisi tujilaumu kwa kuwakilishwa na wanasheria uchwara lakin deni la watu halikwepeki.

Naweza kubisha kwamba siwanasheria uchwara,kwamba ni dili,lakini pia nakubaliana na wewe kwasababu hata katika sekta nyingine wasomi wetu wamefeili ajabu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom