Mwanadiwani na spins zako!
nimeuliza je Rasimu ya tume ni legal na legitimate?
1. kama ndio kwa nini mmefuta maoni ya wananchi?
2. kama hapana kwa nini mmetumia 80% ya document ambayo haina uhalali kuleta katiba pendekezwa? je ina derive legality na legitimacy toka wapi?
hujajibu umepiga njia za sungura tu zinazoelekea nowhere
Ndugu Stefano Mtangoo,
Hakuna spins katika mada yangu!.
Tume ya Jaji Warioba ilikusanya maoni kama Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 inavyobainisha. Kazi ya kuchambua maoni ya wananchi na kuyaweka kwenye waraka unaoitwa Rasimu ya Katiba ilifanyika kulingana na utashi wao ndani ya msingi wa sheria. Kwa msingi huo, Ndiyo maana sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeweka nguzo za kisheria katika msingi wa checks and balance ili kuhakikisha kile ambacho Tume ya Jaji Warioba haikukiweka au ilikiweka isivyo, basi kifanyiwe marekebisho, kifutwe au kiwekwe kingine kilichoko ndani ya maoni ya wananchi.
Checks and balance imeanzia kwenye Mabaraza ya Katiba, Bunge Maalum na wananchi wenye uwezo kisheria wa kupiga kura ya maoni.
Ikumbukwe kuwa, Tume ya Jaji Warioba ilipokea jumla ya maoni 772,211 kwa njia ya mdomo na maandishi kutoka kwa wananchi wapatao 351,664. Ielewe kuwa, siyo maoni yote ya wananchi yaliwekwa kwenye Rasimu ya Jaji Warioba.
Sheria iliweka msingi wa Checks and balance kwa maana ya kuwepo kwa Bunge Maalum ambalo litaipitia Rasimu ya Katiba A.K.A Waraka ili kufanya marekebisho kadri linavyoona inafaa. Ndiyo maana Bunge la Katiba liliamua kuongeza na kupunguza baadhi ya Sura au Ibara kadri lilivyoona inafaa.
Kwa sasa Checks and balance imebaki kwa wananchi kupitia Kura ya Maoni ambapo kama watadhani Katiba Inayopendekezwa imeingiza yale yenye manufaa kwa maisha yao, basi wataamua kuipigia Kura ya NDIYO. Kama watadhani kuna mapungufu, basi wataipigia Kura ya HAPANA.
Kitu cha muhimu lazima tuelewe kuwa, Katiba haiweza kuweka kila kitu anachokipenda mtu mmoja mmoja katika Taifa.
Uamuzi uko kwa wananchi ambao kila mwanachi ana kura moja katika sanduku la kura ya maoni.