Jaji Warioba ni Muongo au Msahaulifu?

Jaji Warioba ni Muongo au Msahaulifu?

Mwanadiwani soma vizuri ulichoandika na maneno ya MH.Warioba alafu upime kuwa umeandike nini kama si kujidharirisha.
 
MwanaDiwani usizunguuuke sana otherwise waonyeshe wazee wajingawajinga wenzako kwamba umepost kitu baadae ukachukue buku 7 yako.
Suala ni moja, kura za NDIYOO zisipotimia zitaTImilizwa.
 
Last edited by a moderator:
hii inaonyesha kiasi gani ccm wanamkubali Mzee Warioba
 
Ndugu,
Mimi siyo mbinafsi katika masuala ya kitaifa. Ninaangalia masuala mapana ya kitaifa kwa sababu Katiba haiwezi kumridhisha kila mwananchi katika .

Katiba Inayopendekezwa imeziangatia masuala mapana ya kitaifa kwa maana hiyo, maoni yangu yamezingatiwa.

Ninachosubiri kwa sasa ni kupiga Kura yangu ya Maoni.
Tanzania ndani ya miaka 50 ya kujitawala chini ya ccm na katiba ya 1977 imeendelea kuwa masikini huku ikitegemea wahisani kwa kiwango kikubwa.tupe sababu za msingi zilizo sababisha Tanzania na watanzania Kuwa masikini na kisha utueleze ni kwa jinsi gani katiba pendekezwa ilivyotoa majibu ya maswala hayo
 
Baada ya kugundua hoja zake hazina mashiko kwa watu wenye fikra pevu kwa sababu zimeangukia katika convenience sampling badala ya random sampling,

Kwa hiyo unamaanisha kuwa maoni mbadala yaliyokusanywa na Samweli Sitta Dodoma (ambayo labda ndiyo yaliyopendekeza serikali mbili) yalipatikana kwa random sampling?

Hivi ungeweza kutumia random sampling kukusanya maoni ya katiba mpya?

Kama mlitaka hiyoo naamini mngeitisha kwanza kura ya maoni kuhusu suala hilo kabla ya mchakato wa katiba mpya, hapo angalau tungeweza kusema kitaalam. Lakini mlikataa, halafu baadaye mkaanza kudai eti alitakiwa akusanye maoni ya katiba kwa kutumia random sampling technique. Wewe ungeweza na kwa akili yako ninavyoitathmini? Lakini labda iungeweza kwa kutumia nguvu za giza kama zile zilizowahi kuwagombanisha mwenyekiti wa BMK na mwandishi wetu wa katiba, au zile zilizomwezesha marehemu kupiga kura na wajumbe kama sita hivi kuhama makazi overnight.
 
Mwanadiwani tena! Nikiona post yako huwa natarajia propaganda za CCM. Huna tofauti na IDs zile zingine za propaganda za vyama vingine.
Wanasiasa wa Tanzania mlio mbele wengi wenu mmeshaishiwa.

Mwisho tu utuambie hiyo asilimia 20 kwa nini waliiondoa?
Kama tume ya katiba ilileta maoni ya wananchi kwa nini zilifutwa? kama hayakuwa maoni ya wananchi bunge lilipata wapi ubavu wa kuweka 80% ya maoni yasiyo ya wananchi ktk katiba yake pendekezwa?

mnaifanya siasa iwe ni worthless post kwa uselessness of your arguments
Ndugu,
Rasimu ya Katiba ilikuwa ni waraka tu ambao Tume ya Jaji Warioba ilipendekeza.

Ninatumaini unafahamu maana ya neno MAPENDEKEZO.

Kazi ya Bunge Maalum ilikuwa ni kutunga Katiba kama Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 inavyobainisha.

Hapo kwenye RED. Bunge Maalum halikuweka 80% ya maoni yasiyo ya wananchi.

Kila kilichowekwa kwenye Katiba Inayopendekezwa ni maoni ya wananchi kama yalivyoainishwa kwenye Takwimu za Ukusanyaji wa Maoni ya Wananchi na pia kwenye Taarifa ya maoni ya wananchi.

Kwa maelezo zaidi tembelea thread hii,
Kama hijapata information zaidi, unaweza kutembelea hapa,
 
Ndugu,
Mimi siyo mbinafsi katika masuala ya kitaifa. Ninaangalia masuala mapana ya kitaifa kwa sababu Katiba haiwezi kumridhisha kila mwananchi katika .

Katiba Inayopendekezwa imeziangatia masuala mapana ya kitaifa kwa maana hiyo, maoni yangu yamezingatiwa.

Ninachosubiri kwa sasa ni kupiga Kura yangu ya Maoni.

Kama wewe si mbinafsi basi dunia hii hakuna mbinafsi. Wewe kwa faida unazopata ndani ya chama tawala uko radhi kila siku kukipigia debe hata kama watu wanaongelea mambo ambayo yako wazi kama wizi/ufisadi na uchafu mwingine. Kama ni kutokuwa mbinafsi ndani ya chama, hapo siwezi kukubishia, lakini usiseme kuhusu taifa kwa ujumla. Kwa maslahi ya taifa wewe ni mbinafsi tena asiye na kipimo. Ningekwambia ujipime mwenyewe lakini najua utatumia kipimo kilichopungua, kwa hiyo ngoja nkuache tu kama ulivyo. Siku moja utapata malipo kwa kazi yako...na kwa kuwa umesema wewe si mbinafsi, naamini yatakuwa malipo mema muheshimiwa sanaaaaaa!
 
Mkuu Super man, asante, kumbe kuna kipengele cha ?!, elimu ya uraia kuhusu kura ya maoni, itakusaidia sana!.

Pasco

pasco soma vizuri sheria ya mabadiliko ya katiba then utaona kama50% haikufikiwa nini kinafanyika
 
Nimeufuatilia sana thread yako hii,

Mpaka sasa zijakutana na hoja mbadala yoyote kutoka kwa UKAWA au wapiga debe wa UKAWA zaidi ya kuhororoja na kubwabwaja.

Huyo 'mchumba' wako FaizaFoxy yeye hazijatimia nahisi. Hiyo mada kichwa chake kinavyoonyesha wewe unadhani alikaa kitako ajibu nini wakati amesema hawana hoja. Nazidi kuthibitisha kuwa ninyi watu kuna namna wanawafanya hadi mnapoteza any slightest sense of reasoning. Ni kama mmeambiwa "the more you post, the more your wallet will fatten" Period.

MwanaDiwani unaleta post ndeeefu zenye mambo yasiyo na maana, sasa najua ni kwa nini. Siku zilizopita niliwahi kukuuliza wewe na wenzako maswali machache ya msingi, mlipotea hadi leo sijapata majibu. Leo mnalazimisha watu waongee vile mnavyotaka...tutakabana tu taratibu tutaelewana.
 
Last edited by a moderator:
Rudisheni maoni ya wananchi kwenye katiba pendekezwa, ondoweni maoni ya chenge na sita kwenye katiba pendekezwa, mkifanya hivyo narudi ccm
Ndugu,
Kuwa mwanaCCM na kutokuwa mwanaCCM ni uamuzi wako ndani ya fikra na mapenzi yako.

Katiba Inayopendekezwa siyo ya CCM, ndiyo maana unawaona UKAWA na wapiga debe wa UKAWA wanahangaika kwenye midahalo, makongamano na mikutano ya hadhara wakiwahamasisha WANANCHI WOTE na siyo wanaCCM ili wapige kura ya HAPANA.

Mtu au Mwanasiasa anayesema Katiba Inayopendekezwa niya CCM wakati huo huo anawaomba wananchi wote wakaipigie kura ya HAPANA ni kuwadharau wananchi kwa kuwafanya ni wajinga.

Kama ni Katiba ya CCM, kwa nini uwaombe wananchi wote wakaipigie kura ya HAPANA badala ya kuwaomba wanaCCM pekee.
 
MwanaDiwani usizunguuuke sana otherwise waonyeshe wazee wajingawajinga wenzako kwamba umepost kitu baadae ukachukue buku 7 yako.
Suala ni moja, kura za NDIYOO zisipotimia zitaTImilizwa.
Ndugu storage

Nimejibu hoja kama hii katika bandiko la #11

Pitia ili upate majibu yangu.
 
Tanzania ndani ya miaka 50 ya kujitawala chini ya ccm na katiba ya 1977 imeendelea kuwa masikini huku ikitegemea wahisani kwa kiwango kikubwa.tupe sababu za msingi zilizo sababisha Tanzania na watanzania Kuwa masikini na kisha utueleze ni kwa jinsi gani katiba pendekezwa ilivyotoa majibu ya maswala hayo
Ndugu,
Umeisoma Katiba Inayopendekezwa ambayo imebeba Sura 19 zenye Ibara 296?
 
Nimeufuatilia sana thread yako hii,

Mpaka sasa zijakutana na hoja mbadala yoyote kutoka kwa UKAWA au wapiga debe wa UKAWA zaidi ya kuhororoja na kubwabwaja.

mtu mwenye ukoma hawezi ku-sense chochote kwenye kiungo kilicho athirika hata umfanyeje.
that's exactly what CCM is suffering from - mental and intellectual leprosy!
 
Ndugu yangu Pasco.

Heading yangu imeuliza swali kama utakuwa umeisoma vizuri.

Mzee Warioba hajasema kwenye Maudhui ni 20%.

Pasco acha kumuwekea maneno mdomoni Mzee wetu!

Kura za Maoni zitatosha na kamwe haziwezi kutosheshwa kwa sababu hakuna sheria ya kutoshesha Kura za Maoni, ndiyo maana UKAWA na wapiga debe wa UKAWA wako kwenye midahalo, makongamano na mikutano ya hadhara wakiwatongoza wananchi ili waipigie kura ya HAPANA Katiba Inayopendekezwa.
MwanaDiwani Contrast hiyo

Mkuu Mwana Diwani, kwani kusheshwa sio sheria ni mbinu tuu, uliwahi kuona popote sheria ya kupiga kura za "siriwazi?!",
kuna sheria yoyote inayoruhusu kupiga kura nje ya kituo cha kupigia kura?!, yote haya hakuna sheria, ila ili kutimiza malengo kusudiwa, tangu ndani ya BMK, kura hazikutosha!, zilitosheshwa!, kwa vile kule ndio ilikuwa ngumu, na zilipotosheshwa, zikatosheleza na kutosha!, kwenye kura ya maoni ni simple zaidi, ndio maana mimi nimewashauri jamaa zangu, wasipoteze muda kufanya kampeni ya kura za hapana, kwa sababu zisipo tosha zitatosheshwa!.

Wengi wanataka kuitumia Zanzibar kama kingamaji kuzuia kura zisitoshe, kwa kuhamasisha kura nyingi za hapana!, bahati mbaya hawajui, hilo kingamaji limewekwa kwenye mteremko!, maji yakija kwa wingi, yatalipanda, na kasi ya maji ikizidi, hadi hilo kingamaji nalo litasombwa na maji, kwa sababu, utaratibu wa "kutoshesha!", huko Zanzibar, ndiko ulikoanzia siku nyingi!, siku zote "sharubu" huwa zinashinda, ila zinatosheshwa, na kutangwazwa mshindwa!.

Katiba imeishapita, kinachofanyika ni taratibu tuu za kuhalalisha, kwa faida ya hawa wajaza mabakuli yetu, tunaowatembezea!, lakini kwa sisi Watanzania!, katiba ni "ndiyo!".

Pasco.
 
Last edited by a moderator:
Bahati mbaya propoganda za namna wakati mwingine zinapotosha na kudanganya. Unaweza kuwa na mada iliyoandikwa maneno elf na ya pili iliyoandikwa maneno 998 yale yale not maneno mawili yakabadilishwa not kuongezwa mengine manne. Mada hii haiwezi kuwa sawa na ile ya awali na pengine hata maana yake ikabadilika kabisa...
 
Kwanza kabla yakusoma andiko lako tu, Katiba yakuandikwa na Chenge fisadi haiwezi hata siku moja ikawakilisha mawazo yawananchi. Chenge hapo amewakilisha genge la mafisadi papa nyuma yake and what do you expect? Fisi apewe jukumu lakuandika katiba ya kuwaongoza mbuzi? Give me a break author! Eti 80% yamawazo yawananchi yamewakilishwa, in what context? Nyambafu kabisa
 
mtu mwenye ukoma hawezi ku-sense chochote kwenye kiungo kilicho athirika hata umfanyeje.
that's exactly what CCM is suffering from - mental and intellectual leprosy!
Ndugu,

Hata mtu asiyefahamu kama hafahamu, hawezi kufahamu kama hafahamu.

Inawezekana UKAWA ni mmoja wa watu katika kundi ninalolisema!.

CCM kwenye siasa za Tanzania inapimwa kwenye sanduku la kura.

Kwa mara ya mwisho ilipimwa kwenye chaguzi za madiwani 27 na chaguzi za ubunge katika Jimbo la Kalenga na Chalinze.

Kuna vyama fulani baada ya kutumia helikopta 3 kwenye kampeni, vilijikuta vikiambulia madiwani 3 katika ya madiwani 27. CCM ilipata madiwani 24.

Kwenye uchaguzi katika jimbo la Kalenga, walitumia helikopta 1 kuambulia 20% ya kura zilizopigwa wakati CCM wakipata 79% ya kura.

Kwenye Jimbo la Chalinze waliamua kutumia magari na kuambulia 10.5% ya kura, wakati CCM ilipata 86.6%.

Hiyo ndiyo ''mental and intellectual leprosy'' ya CCM kwa mtazamo wako.
 
sio kweli kwamba ukipiga kura ya hapana unataka katiba ya zamani hapo ni kwamba kura ya hapana itafanya raisi haitishe bmk warudie kazi upya ili kuondoa hizo kasoro labda ipigiwe kura ya hapana tena ndo tutarudi kwenye katiba ya zamani! so acha upotoshaji!

Achana na huyo mchumia tumbo,njaa imempofusha akili hapo alipo anawaza makombo toka kwa lowasa tu!
 
Ndugu,

Hata mtu asiyefahamu kama hafahamu, hawezi kufahamu kama hafahamu.

Inawezekana UKAWA ni mmoja wa watu katika kundi ninalolisema!.

CCM kwenye siasa za Tanzania inapimwa kwenye sanduku la kura.

Kwa mara ya mwisho ilipimwa kwenye chaguzi za madiwani 27 na chaguzi za ubunge katika Jimbo la Kalenga na Chalinze.

Kuna vyama fulani baada ya kutumia helikopta 3 kwenye kampeni, vilijikuta vikiambulia madiwani 3 katika ya madiwani 27. CCM ilipata madiwani 24.

Kwenye uchaguzi katika jimbo la Kalenga, walitumia helikopta 1 kuambulia 20% ya kura zilizopigwa wakati CCM wakipata 79% ya kura.

Kwenye Jimbo la Chalinze waliamua kutumia magari na kuambulia 10.5% ya kura, wakati CCM ilipata 86.6%.

Hiyo ndiyo ''mental and intellectual leprosy'' ya CCM kwa mtazamo wako.

Tumia akili kufikiri,haiwezekani uchaguzi wenye watu 16,000 walioandikishwa kwenye daftari uamuliwe na watu 2000!Yaani mshindi achaguliwe na hao 2000 then mtu timamu ajisifu
 
Back
Top Bottom