Jaji Warioba ni Muongo au Msahaulifu?

Jaji Warioba ni Muongo au Msahaulifu?

... Pasco tatizo hao kiriku ccm hawana adabu kwa wakubwa zao, huwezi kumuita warioba muongo
jaji anajua nini anafanya na kwa madhumuni gani

kwanza hayo maoni ambayo tume ys warioba wamekuwa wakiyazungumzi ni maoni ya wananchi
 
Last edited by a moderator:
"Ukihesabu ibara kwa ibara..." unajua kwa nini hicho kichwa kimeanza kwa kusema hilo?
 
MwanaDiwani

Hamna kitu umeeleza hapo zaidi ya kujitahidi kufanya kitu kinaitwa MCHEZO WA UBONGO! Ok! labda tukuulize nikwanini kifungu kilichotaka viongozi wawajibishwe mmekitoa!!??
Ndugu,
Hakuna mchezo wa ubongo niliyofanya. Nimeeleza kama zilivyo hoja za Jaji Warioba katika uwanja wa siasa.

Kuhusiana na kifungu cha Wabunge kuwajibishwa, Tume ya Uandishi wakati ikiwasilisha Katiba Inayopendekezwa kwenye Bunge Maalum ilitoa ufafanuzi na kusema,
Haki ya wapiga kura kumwajibisha Mbunge

Mheshimiwa Mwenyekiti,
Ibara hii inahusu haki ya wapiga kura kumwajibisha Mbunge. Kamati moja imependekeza Ibara hii ibaki kama ilivyo kwenye Rasimu ya Tume. Kamati saba zimependekeza Ibara hii ifutwe, na Kamati Nne zimependekeza marekebisho madogo ikiwemo kuwepo kwa haki ya wapiga kura kumwajibisha mbunge ambaye ameshindwa kuwasilisha au kutetea kero za wapiga kura wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti,
Kamati ya Uandishi baada ya kutafakari maoni hayo inapendekeza ibara hii ifutwe kwa kuwa, haki inayopendekezwa inaweza kutumika vibaya ikiwemo kumwekea vikwazo vya kiutendaji Mbunge aliyeko madarakani. Aidha, wapiga kura wanayo haki ya kumwajibisha kwa kutompigia kura Mbunge katika kipindi cha miaka mitano endapo wananchi wataona Mbunge anayewawakilisha hafai, wanaweza kumwajibisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti,
kwa kuzingatia mapendekezo hayo Kamati ya Uandishi inapendekeza Ibara hii ifutwe.
Either way, kama utakubaliana au kutokubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uandishi, majibu utayaweka kwenye sanduku la Kura ya Maoni!
 
Ndugu,
Hakuna mchezo wa ubongo niliyofanya. Nimeeleza kama zilivyo hoja za Jaji Warioba katika uwanja wa siasa.

Kuhusiana na kifungu cha Wabunge kuwajibishwa, Tume ya Uandishi wakati ikiwasilisha Katiba Inayopendekezwa kwenye Bunge Maalum ilitoa ufafanuzi na kusema,

Either way, kama utakubaliana au kutokubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uandishi, majibu utayaweka kwenye sanduku la Kura ya Maoni!

Nimesoma maelezo yako hapo juu! kwa uwerevu wangu nimegundua kunakitu mnakipigania nacho ni "KUBAKI" madarakani.
 
Jaji warioba sio muongo na sio msahaulifu,wewe Mwanadiwani ndo hujaelewa au unapotosha.
Mzee warioba anaposema katiba ya 6 imechukua 81% anamaanisha MAUDHUI ya ibara.
Mzee warioba anaposema katiba ya 6 imechukua 20% anamaanisha CONTENTS kama zilivyo kutoka kwenye rasimu.

NB:Ile 81% ya maudhui pia imebadilishwa na kubakiza 20% tu ndiyo imeachwa tena kwenye vipengele ambavyo havina madhara kwa wanasiasa.sasa hapo uongo na usahaulifu wa mzee warioba ni upi?cc;MwanaDiwani
 
Back
Top Bottom