JAJI wa MAHANGA hakuwa na jinsi...

Ni kama zilivyo dhaifu na za kishamba zile za Kupinga ubunge wa
Igunga.Too low hata mimi kama ni hakimu nazitupilia mbali.

Kamanda vipi mbona siku hizi umekuwa mtu wa kupondea sana, nini kimetokea hapo kati? Ila ukweli mmoja ni kwamba moto wa Chadema unawawakia na mnalitambua hilo, sema tu ubishi wenu kuonyesha kwamba hamkubali lakini moyoni mnasononeka.
 
Historia ya CDM wengi hawaijui, Ilizaliwa ikawa yatima, chokoraa na mwisho ombaomba...imeishi maisha ya mtaani ikitafakari ugumu wa maisha, ikayatambua na KUFANYA MAAMUZI MAZITO ya kuondoka mtaani na kuionesha jamii ubaya wa huko jalalani, sasa inaishi mjini na kutafuta ukombozi wa kuwatoa wengine huko kwenye lindi la umasikini...Kwanini wakatae kuja? Je huo uchafu na hizo harufu hawazioni? Umakini wa CDM unatokana na matatizo wanayoyapata "WENYENCHI" ambao siku zote wanatambulishwa kwa jina la "NDUGU WANANCHI" pindi wanapoombwa kupiga kura.
 
kwa mwenendo wa kesi ulivyo kuwa, pamoja na ushahidi na shangaa huyu makongoro kushinda,yani katika kesi ambazo zilikuwa zinaonekana wazi kabisa CDM kushinda ni hii,kwani hata mtoto mdogo angejua tu hukumu inakuaje.
Kwa hukumu nadhani tumeona jinsi ukweli unavyo pindishwa na mahakama zetu zisizo huru.
Hii inanifanya nipate wasiwasi kwenye kesi ya jimbo la ubungo,kwani naona kama kuna kampango fulan hiv,na ndio njia wanataka kuitumia kuuwa CDM,lakin naamini mapambano hayatokoma kabisa ndio yanazidi kupamba moto!

huyu ndugu anayejiita dume la chura sidhani kama anaelewa kinachoendelea nchini,leo hii mtu mwe utimamu wa akili sidhani kama anaweza kuropoka kama anvyo fanya dume la chura. hawezi kutaja hoja ata moja ambayo yeye dume la chura ana iona haina mashiko. hili ni jukwaa la kutoa mawazo yenye maana siyo kuropoka kama dume la chura.
Dume la chura na kushauri urudi kule fb tafadhali,nahisi utasababisha ban kwa watu.
 
Mbona Chadema ikishinda huwa hamtuletei wasifu wa jaji? au mnataka kila siku mshinde nyie?
Mbona Chadema ikishinda huwa hamtuletei wasifu wa jaji? au mnataka kila siku mshinde nyie?
Mimi sidhani ni suala la nani kashinda. Umesikia Shinyanga wa CCM kashinda na hakuna kelele, umesikia sumbawanga cdm kashinda hakuna kelele; hoja ni kwamba kwa namna tulivyokuwa tunasikia yaliyokuwa yanaendelea mahakamani na ushahidi uliokuwa ukitolewa, tuliamini kuwa Mahanga atashindwa. Utakumbuka kuwa hata kabla kesi haijafunguliwa, taarifa mbalimbali za vyombo vya habari zikiwa na uthibitisho wa video na picha zilionyesha wazi uchakachuaji wa matokeo. Vituo kadhaa havikujmuishwa kwenye matokeo, masanduku yaipatikana yakiwa tupu, mihuri ilikamatwa mahali pasipohusika nk. Hukumu kwenda kinyume na ushahidi uliotolewa ndiyo kinafanya watu wawe na mashaka.
Hata kesi ya Lema kule Arusha, haina ubishi kuwa Lema alitumia lugha kali katika kampeni (ingawa hii ilitumiwa na wengine pia), na kwa kuwa hakimu alijikita katika sababu hiyo, akaamua kutengua ubunge wake; kilichopingwa zaidi ni kumzuia Lema kutogombea tena, kwani kosa alilofanya halimo katika yale yaliyotajwa kumfanya asigombee tena.
Kwa hiyo si kweli kuwa kila cdm inaposhindwa basi lazima watu waone haki haikutendeka, inategemea na hukumu ilivyojieleza na kesi ilivyoendeshwa.
Kwa hili la Mahanga wengi tuna hamu ya kujua namna jaji alivyotupilia mbali ushahidi uliotolewa. Tupeni hukumu tujisomee wenyewe - sheria ya uchaguzi tunayo.
 
Jf sasa inaanza kupoteza mwelekeo. Ni kweli Rais amepewa mamlaka ya kikatiba kuteua majaji. Lakini uhuru wa majaji umewekwa wazi katika katiba hiyo hiyo. Tujaribu kusoma katiba. Kuna malolongo mrefu kabla ya kutengua uteuzi huo na umewekwa kwa ajili ya kulinda hadhi ya mahakama na uhuru wa majaji katika utendaji wao wa kazi. Hawaingiliwi kwa urahisi kama inavyodaiwa kwenye jamvi hili. Tujaribu kufanya utafiti kabla la kupotosha wengine.
 
Mpendazoe walimkamia sana kwa sababu ya kumshupalia mkapa na ufisadi kwenye bunge lililopita na sasa huu ni wakati wa malipizi....................
huo ndiyo ukweli wenyewe na wataendelea kumuhujumu kila hatua kama walivyofanya kwa Lema kule Arusha. lakini yote haya yana mwisho,haki siku zote itashinda!
 
Jina lake halisi ni Siaga Ongoro Masaburi, ni ndugu wa damu na Didas Masaburi-meya wa jiji la dar.

Jina la Makongoro Mahanga ni kama ilivyo kwa Dr. Hamisi Kigwangalla-bila shaka you know "woraimin"!!

Familia yao haiko Bunda, walihamia wilayani serengeti kijiji kinachoitwa bwitengi, na ndipo makongoro alipopatia upenyo wa kuona mwanga wa shule baada ya kufanya ukigwangalla!!
nimeipenda hiyo ya 'ukigwangalla'...inabidi tuiingize kwenye kamusi yetu ya kitaa kama ile ya ramadhani ally 'kihiyo'...!
 
hivi kwanini asikate rufaa? labda haki itatendeka mbeleni, huwezi jua

I agree, lakini pia awe tayari kwa lolote. Hatakama ameonewa/chezewa kamchezo , watu hao hao wanaweza wakawa wajanja, mahakama ya rufaa pia inamapandikizi/waoga wachache. That being said, kama kesi ikiamuliwa na majaji watatu, wawili wanaweza kuwa mapandikizi na wakaweka mmoja imara/asiyeyumbishwa. Sasa wale wawili wakishakubaliana kumpitisha Mahanga ,huyo jaji mmoja ata awe vipi ratio itakuwa 2-1 = matokeo yale yale. Nimeliona hili kwenye ile kesi ya kuweka mgombea binafsi , na ile inayohusu fedha alizotoa Ghadafi etc. However everything is worth trying kama Mpendazoe anaamini ameonewa haki itapatikana tu ; it is a matter of time.
 
Inasikitisha kama mtu anakamatwa na maboksi ya kura live then anashinda kesi ila kila kitu kina mwisho wake,mahakama haiko huru huo ndio mjandala,na sio mahakama ni mfumo wote wa uongozi kuanzia kwa kw JK na watu wake
 
Amka wewe!

Ushahidi wa kukamatwa na masanduku ya kura ni dhaifu?
Wacha woga utaishia kusindikiza mafisadi
 
Ni bora kuisoma kuliko kusema bila kuisoma....Kesi ya Mpendazoe imeharibiwa na wakili wake. Hakuonesha ni vipi Mahanga alikamatwa na maboksi, hakukuwa na taarifa ya polisi. Gazeti halikutaja jina wala chama. Vielelzo kama video na picha havikuwakilishwa mahakamani. Jamani Jaji atabeba mbeleko vipi hapo. Tuwe makini.
 
Ndo maana anaitwa Prof. Kafanya mengi makubwa na ya maana, someni hukumu acheni blabla jamani. Anafaa hata kupendekezwa Mahakama ya kimataifa.
 
Back
Top Bottom