VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji wa Mahakama ya Rufani,hakuwahi kuiangusha Serikali kwenye maamuzi yake. Tangu akiwa Mahakama Kuu,Jaji Juma aliilinda kwa nguvu zake zote Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Analipa fadhila kwa rafikiye Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Kiuweledi, Jaji Prof.Juma ni msomi washeria aliyebobea. Ana uwezo mkubwa sana. Lakini,maisha yanampokonya matumizi sahihi ya weledi wake. Ndivyo mambo yanavyotakiwa kuwa?!Akiwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jaji Prof.Juma aliwahi 'kumsave' Wakili Msomi Ridhiwani Kikwete ambaye 'alidisco'. Alimsimamia kidete hadi akabaki nakumaliza masomo yake mwaka 2005 na kutunukiwa Shahada ya Kwanza ya Sheria.
Jaji Prof. Juma alianza kulipwa alichokifanya kwa Ridhiwani mwaka 2007 pale alipoteuliwa kweye Tume ya Kuchunguza Mauaji ya wafanyabiashara watatu maeneo ya Sinza. Tume hiyo iliyoundwa na Rais iliongozwana Jaji Kipenka Musa. Baadaye, Jaji Prof. Juma aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mwaka 2008. Akiwa hapo,Shauri la uchaguzi kati ya Makongoro Mahanga na Fred Mpendazoe likaletwa mbele yake. Kila mtu anafahamu kilichotokea. Kwa kukumbuka tu,Mahanga aliibuka mshindi na CCM 'ikapeta'.
Mwishoni mwa mwaka jana,Jaji Prof.Juma alipandishwa cheo na kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Hapo ndipo lilipomkuta Shauri lililotolewa uamuzi jana:Shauri la Aeshi Hilary dhidi ya Norbert Yamsebo. Mlitegemea matokeo tofauti? Ingawa shauri la Yamsebo lilisikilizwa na jopo la Majaji watatu: Jaji Edward Rutakangwa, Jaji Stephen Bwana na Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma, bado Jaji Juma alikuwa na nafasi yake kubwa katika shauri hilo.
Tasnia ya sheria inafanana na ya jeshi. 'Mdogo' hutumwa na kutumikia zaidi. 'Seniority' ndio kila kitu. Kwa 'ukubwa' katika jopo hilo, Jaji Rutakangwa anaanza,halafu Jaji Bwana na tena Jaji Prof. Juma. Hivyo basi, kazi kubwa ilifanywa na Jaji Prof. Juma. Mwenye kuamini na aamini. Majaji wawili waliobaki wao 'wali-vet' kilichoandaliwa na Jaji Prof. Juma.
Sina mashaka na uwezo wa Jaji Prof. Juma. Nina mashaka na mahusiano yake na mkuu wa Serikali na chama. Kwa mahusiano hayo, CHADEMA waweza kufurukuta mbele ya Jaji huyu? Sidhani. CHADEMA watakuwa wanapiga mwereka mbele yake kila shauri. Labda aamue kutumia weledi wake ipasavyo.
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dares Salaam(sasa Dodoma)