Unaweza ukamchukia/kumdharau mtu lakini do not CHALLENGE his integrity kama huna facts. Hujamtendea haki Prof. Ibrahim Juma kwa hili bandiko lako (Full disclosure: Prof. Ibrahim Juma ni mwalimu wangu na mtu ninaye mheshimu sana). Naweza kuwa sifahamu sana utendaji wake ndani ya Mahakama, lakini humtendei haki ukisema ni msomi wa Ovyo. He is an accomplished scholar. And no scholar I know in the judiciary can match his scholarship. None.
For your info:
Academically: Judge Ibrahim Juma ana:
1. Bachelor of Laws, University of DSM.
2. LLM, University of DSM
3. LLM Ghent University, Belgium (specialty: Law of the Sea)
4. Masters of Laws (International Human Rights Law), Raoul Wallenberg University, Lund, Sweden.(One of the very best Human Rights institutions in Europe).
5. PhD, Ghent University Belgium (specialty: Law of the Sea).
Google hivyo Vyuo (na Thesis zake zipo online)
Prof. Juma ni mbobezi kwenye sheria za Bahari (he is an expert in the law of the sea-PhD na LLM yake alibobea humo).
Alivyorudi UD, ni katika wasomi wachache ambao walikuwa na utaalam wa sheria za bahari (mwingine kwa Tanzania ni Prof. Mahalu na Prof. Nasila Rembe-Huyu aliishia huko kusini mwa Africa na of course wapo wengine wachache-lakini yeye ndo alikuwa mtaalamu mbobezi).
Prof. Juma ameandika sana, I mean ana maandiko kwenye journals nyingi za kimataifa. Amefanya compilation ya Index of cases za Criminal Law (yeyote aliyepita Faculty ya sheria mlimani aliitumia), ame-publish vitabu kwenye Human Rights, Law of The sea, refugee law, international law, environmental law etc-jaribu hata ku-google) utapata kazi zake nyingi online. Ame-edit vitabu kama vinne na Professor Chris Maina Peter nk.
NAWEZA KUSEMA KWA DHATI KABISA Profesa wa UDSM anayeweza kumzidi publications Prof. Ibrahim Juma (na weledi labda) ni Prof. Chris Maina Peter na Issa Shivji (amestaafu) (hawa wako kwenye dunia yao-again kwa aliyepita UD ananielewa). No body else. I repeat no body else. Hata Prof. Kabudi, kwangu mimi hafiki hata nusu ya Prof. Ibrahim Juma (ingawa na yeye ni mtaalamu in his own right).
Prof. Juma ni katika walimu wachache sana pale UDSM waliokuwa very thoughtful, fair in their dealings with students, straight forward with unimpeachable integrity.
Siwezi kuongelea kipindi ambacho ame-join judiciary 2008 onwards. Lakini as a matter of fact, kwangu mimi Prof. Juma anastahili hata kuwa Judge International Tribunal for the Law of the Sea (Hamburg) au International Court of Justice (The Hague). Kwamba alimsaidia Ridhiwani Kikwete asi disco-it is just garbage and not even worth a discussion. By the way ninavyomfahamu Prof. Juma, hata kama angekuwa na hiyo nafasi asingeweza. He simply cant.
Narudia kusema, jamani hata kama tunachukia mtu Fulani tujitahidi kuwa fair in our assessment. Maana mimi ninavyomfahamu Prof. Juma, kusoma bandiko la ndugu yangu Lusungo naona ni chuki zimemjaa kabisa au humjui Huyu bwana (excuse my language).
Again, Prof. Juma anaweza kuwa na mapungufu yake kama binadamu mwingine yeyote. lakini tuwe waangalifu. Kama hatuna information za kutosha tusidharau watu kwa chuki zetu au kwa kuambiwa.
Masanja