Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma katika Utendaji

Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji wa Mahakama ya Rufani,hakuwahi kuiangusha Serikali kwenye maamuzi yake. Tangu akiwa Mahakama Kuu,Jaji Juma aliilinda kwa nguvu zake zote Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Analipa fadhila kwa rafikiye Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Kiuweledi, Jaji Prof.Juma ni msomi washeria aliyebobea. Ana uwezo mkubwa sana. Lakini,maisha yanampokonya matumizi sahihi ya weledi wake. Ndivyo mambo yanavyotakiwa kuwa?!Akiwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jaji Prof.Juma aliwahi 'kumsave' Wakili Msomi Ridhiwani Kikwete ambaye 'alidisco'. Alimsimamia kidete hadi akabaki nakumaliza masomo yake mwaka 2005 na kutunukiwa Shahada ya Kwanza ya Sheria.

Jaji Prof. Juma alianza kulipwa alichokifanya kwa Ridhiwani mwaka 2007 pale alipoteuliwa kweye Tume ya Kuchunguza Mauaji ya wafanyabiashara watatu maeneo ya Sinza. Tume hiyo iliyoundwa na Rais iliongozwana Jaji Kipenka Musa. Baadaye, Jaji Prof. Juma aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mwaka 2008. Akiwa hapo,Shauri la uchaguzi kati ya Makongoro Mahanga na Fred Mpendazoe likaletwa mbele yake. Kila mtu anafahamu kilichotokea. Kwa kukumbuka tu,Mahanga aliibuka mshindi na CCM 'ikapeta'.

Mwishoni mwa mwaka jana,Jaji Prof.Juma alipandishwa cheo na kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Hapo ndipo lilipomkuta Shauri lililotolewa uamuzi jana:Shauri la Aeshi Hilary dhidi ya Norbert Yamsebo. Mlitegemea matokeo tofauti? Ingawa shauri la Yamsebo lilisikilizwa na jopo la Majaji watatu: Jaji Edward Rutakangwa, Jaji Stephen Bwana na Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma, bado Jaji Juma alikuwa na nafasi yake kubwa katika shauri hilo.

Tasnia ya sheria inafanana na ya jeshi. 'Mdogo' hutumwa na kutumikia zaidi. 'Seniority' ndio kila kitu. Kwa 'ukubwa' katika jopo hilo, Jaji Rutakangwa anaanza,halafu Jaji Bwana na tena Jaji Prof. Juma. Hivyo basi, kazi kubwa ilifanywa na Jaji Prof. Juma. Mwenye kuamini na aamini. Majaji wawili waliobaki wao 'wali-vet' kilichoandaliwa na Jaji Prof. Juma.

Sina mashaka na uwezo wa Jaji Prof. Juma. Nina mashaka na mahusiano yake na mkuu wa Serikali na chama. Kwa mahusiano hayo, CHADEMA waweza kufurukuta mbele ya Jaji huyu? Sidhani. CHADEMA watakuwa wanapiga mwereka mbele yake kila shauri. Labda aamue kutumia weledi wake ipasavyo.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dares Salaam(sasa Dodoma)

We umeamua kumtisha Godbless Lema bila sababu.
 
sio kweli, majaji wanapo kaa full benchi kwenye uamuzi kama mmoja hajaridhia anaunwezo wa kukataa bila wenzake kumlazimisha( decending judge) kesi nyingi za Lord Denning alikuwa asipo ridhia na maamuzi ya wenzake anakataa. hakuna seniority pale. wacha kupotosha umma. unless kama interest zako zimeguswa na hukumu zake.
Huyo jamaa keshaminywa na Prof., mzee wa kunyoosha rula.
 
Kwani jaji mzuri ni yule anayeiangusha serikali?

Ama kweli wengine vichwa vyenu mnatumia kufugia nywele!
Hapo ndo kituko kilichopo, afu hawajui kuwa kesi haiamuliwi mitaani.
Inaamuliwa mahakamani kwa sheria na ushahidi.
Kuna watu walishashindwa kesi nyingi za wazi kabisa kwa makosa yao wenyewe kwenye kanuni za mahakama.
 
sio kweli, majaji wanapo kaa full benchi kwenye uamuzi kama mmoja hajaridhia anaunwezo wa kukataa bila wenzake kumlazimisha( decending judge) kesi nyingi za Lord Denning alikuwa asipo ridhia na maamuzi ya wenzake anakataa. hakuna seniority pale. wacha kupotosha umma. unless kama interest zako zimeguswa na hukumu zake.
Mkuu..umeharib kipande cha mwisho tuu..
Umempa logic nzuri as basic kwake
 
Kwa sisi tuliopitia mikono ya Dr. Juma tunaufahamu uadilifu wake fika!. Kwa waliopita UD wanajua kuna technical disco na ku disco kwa ukilaza!.

Hata mimi pia nilisoma UD na nilidisco wakati Dr. Juma akiwa dean!. Kiukweli wale watakaomshutumu kwa lolote, wanajichumia dhambi bure!. Ni sawa na Prof. Shivji au Fimbo awe Jaji halafu atoe rulling ya haki in favour of serikali useme analipa fadhila!.

Kwa sababu tumepoliticise kila kitu, uamuzi wowote in favour of Chadema then huo ndio uamuzi wa haki!. Uamuzi wowote in favour of CCM ni upendeleo!.

Pasco.
Mkuu Pasco! Naomba unifafanulie tofauti kati ya "technical disco na kudisco kwa ukilaza"? Pili tukubaliane kuwa "controversial rulings" za jaji ye yote zinaleta mashaka juu ya weledi wake. Tatu "any judge like Caesar's wife, should be beyond suspicion"
Mara nyingi hua ninazikubali sana report za bwana Tupa tupa, mzee wa Lumumba, mara baada ya kusoma hii comment yako nimeridhika pasipo shaka kwamba huyu jaji anatumika (kama ni kweli ndiye aliyehukum kesi ya Mpendazoe na Makongoro). Kama sikosei, kwenye ile hotuba ya Kikwete ya baraza la Idd mwaka juzi pale Dodoma nilisikia hili jina la huyu jaji kupitia kinywa cha Kikwete, I am starting to join the dots here! Anyway, hata hivyo CDM mwendo mdundo, 2015 sio mbali!
 
Jaji mzuri niyule anaehukumu kwahaki kisheria hatakàma ukishinda kesi zote haijalishi. Mahakama zatanzania haziko huru tunahitaji Uhuru ili tuiamin
 
tupatupa mzee wa kupindisha pindisha na kunogesha maneno yake ili kunogesha riwaya zake.......na kwakufanya hivyo amefanikiwa kuwakamata mamia ya nyumbu hapa jf!.
 
Mkuu Pasco! Naomba unifafanulie tofauti kati ya "technical disco na kudisco kwa ukilaza"? Pili tukubaliane kuwa "controversial rulings" za jaji ye yote zinaleta mashaka juu ya weledi wake. Tatu "any judge like Caesar's wife, should be beyond suspicion"
Mkuu asante kwa swali hili, kwa sababu mimi mwenyewe ni muhanga wa kula DISCO nilipokuwa UDSM na Prof. Ibrahim Juma akiwa Dean, alinitendea haki na nikaendelea.

1.Academic disco ni mwanafunzi anayeshindwa kufikia GPA ya 1.8, kwa sababu zozote zile iwe ni ukilaza au hakukamilisha course work.
A student shall be discontinued from studies at the University if he/
she attains an overall GPA of less
than 1.8. A student shall be discontinued from studies if, after sitting for supplementary
examinations, he/she obtains a GPA of less than 2.0
2. Technical Disco ni pale mwanafunzi anapozuiwa kufanya EU kwa sababu zozote. hivyo anakuwa discontinued. Huyu anayepewa disco kwa kuzuiwa sio lazima awe kilaza na kwenye matokeo panawekwa dash,

A candidate
must attend a minimum of 75% of the lectures and seminars (where offered) to be eligible
to sit for the end of semester written examination in the course otherwise the Dean retains the power
to bar any candidate’s access to examination if he/she is not sa
tisfied that the candidate qualifies to sit
for the examination as required by regulations, either by reason of poor attendance in lectures and
seminars or poor performance in coursework. A student who is so barred:
A candidate who, under these regulations is not permitted to do a written examination in any course
may be recommended for discontinuation or required to repeat a year as the case may be.

Mimi disco langu lilikuwa hili la pili. Nili appeal na nikashinda, na amini usiamini Ma-lectures nao ni human beings na sometimes kunatokea ma bifu tuu ya kitaa, unakomeshewa darasani.

My case was very special case, nimefanya mtihani, nimepata B+ kwenye karatasi ya mtihani, lakini kwenye matokeo ikawekwa E. Nikaanzia kwa mwalimu wa somo, akasema ulipata B sasa kama imeandikwa ni E then huyo atakuwa ni exterrnal examiner. Nikaenda kwa dean (Dr. Juma) akaangalia marking ya external akakuta alipitisha ile ile B+, hivyo hiyo E imetoka kwa mwalimu wa somo, ambaye ndiye yule niliyemuona mwanzo.

Dr. Juma akamuuliza mwalimu wa somo, kwa nini ameweka E, mwalimu akamjibu,huyu mwanafunzi (mimi), ananifahamu vizuri, na hakuwahi kuniona nikihudhuria lecture zake, hivyo sikuattend minimum ya 75% hivyo amenifutia matokeo iwe asa if sikufanya na sikuattend course.

Hapo ndipo Dr. Juma akatenda haki, kuwa mwanafunzi aliyeshindwa kufikia hiyo 75% ya mahudhurio, alipaswa kuzuiwa kufanya EU na sio kufanya na kufutiwa matokeo!. Pili mwalimu wa somo alipaswa kumletea mahudhurio dean kuthibitisha sikuhudhuria lecture zake, na ni dean ndiye anayezuia mwanafunzi kufanya EU na sio mwalimu wa somo. Appeal ikapita, B+ ikatambuliwa, disco lilaondolewa!.

Hivyo Prof Juma ni mtu wa haki bin haki!.

Paskali
 
Tatizo tutatibu dalili za maradhi badala ya maradhi yenyewe.

Kutoaminiana hadi kufikia vyombo vya sheria kutiliwa shaka ni hatua ya kusikitisha.

Hata hivyo kuna sehemu mbili za kujadili

1. Vyombo vya sheria:
Kumekuwepo na mtazamo usiopendeza juu yake

Hili linachangiwa kwa sehemu na vyombo vya sheria ''kupoteza'' nguvu kama mhimili

Matukio yanayoendelea hasa ya siasa yanatia shaka hata pasipohitaji shaka

Kwa maneno mengine, trust na vyombo vya kutoa sheria ipo tofauti na matarajio

2. Hatuwezi kupata suluhu ya jambo hili hadi tutakapobadili mfumo

Jaji mkuu anapaswa kupitia katika 'vetting' nyingine

Nchi za wenzetu mtu akiwa Jaji, kwanza hawezi kuondolewa, pili anawajibika maeneo mengine si kwa eneo moja

Kwa mtazamo huo hakuna mhimili 'uliozama' zaidi chini, na yote inakuwa huru

Tuangalie hili la Jaji wa sasa. Wadhifa wake anakaimu Ujaji mkuu hadi uteuzi kamili

Hii si nafasi ya kukaimu, si kuwa inamkwaza mhusika, inajenga mashaka bila ulazima.

Jaji kwa kukaimu anakuwa na conflict of interest.
Kulinda masilahi ya taasisi lakini kama binadamu naye ana matarajio binafsi

Likitokea jambo maamuzi ya Jaji yataweza kuunganishwa na 'ukaimu'

Kwavile mfumo wetu ni mbovu, unatoa fursa tu ya mteuzi kuamua lini afanye hivyo

Hivi Jaji Othman aliamka tu na kutoa taarifa au kulikuwa na taarifa siku nyingi?

Kwanini nafasi ya Ujaji mtu akaimu?

Kwa umuhimu wake katika nchi na utawala hili linatokeaje?
Mkuu Nguruvi3, naelewa concern yako kwenye system ambayo ni rotten, then its normal watu kudhani kila mteuliwa pia ni a rotten stock, lakini kiukweli hata katika tenga la samaki, sio lazima mmoja akioza, wote waoze, samaki mmoja wa jana, aliyewekwa tenga moja na samaki wa leo, then ikatokea huyo mmoja wa jana akaoza, ukalitupa tenga lote kwa kuamini wote wameoza, utakuwa hajawatendea haki samaki wale wa leo kwa sababu watakuwa hawajaoza!.

Paskali
 
tupatupa mzee wa kupindisha pindisha na kunogesha maneno yake ili kunogesha riwaya zake.......na kwakufanya hivyo amefanikiwa kuwakamata mamia ya nyumbu hapa jf!.
Soma angalau tarehe ya uzi huu Mkuu. Mengine hujaelewa chochote

Mzee Tupatupa
 
Pia alikuwa mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria Tanzania,Law Reform Commission of Tanzania,

Ni mweledi sana japo ni conservative judge,pia radical and a bit shy.

Ni kizazi bora kabisa cha chuo kikuu cha Dar es salaam kitivo cha sheria,itachukua miaka kupata kizazi kingine taking into account ccm wamekuwa wakiwashawishi waache taaluma na kuwatumikia
 
Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji wa Mahakama ya Rufani,hakuwahi kuiangusha Serikali kwenye maamuzi yake. Tangu akiwa Mahakama Kuu,Jaji Juma aliilinda kwa nguvu zake zote Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Analipa fadhila kwa rafikiye Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Kiuweledi, Jaji Prof.Juma ni msomi washeria aliyebobea. Ana uwezo mkubwa sana. Lakini,maisha yanampokonya matumizi sahihi ya weledi wake. Ndivyo mambo yanavyotakiwa kuwa?!Akiwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jaji Prof.Juma aliwahi 'kumsave' Wakili Msomi Ridhiwani Kikwete ambaye 'alidisco'. Alimsimamia kidete hadi akabaki nakumaliza masomo yake mwaka 2005 na kutunukiwa Shahada ya Kwanza ya Sheria.

Jaji Prof. Juma alianza kulipwa alichokifanya kwa Ridhiwani mwaka 2007 pale alipoteuliwa kweye Tume ya Kuchunguza Mauaji ya wafanyabiashara watatu maeneo ya Sinza. Tume hiyo iliyoundwa na Rais iliongozwana Jaji Kipenka Musa. Baadaye, Jaji Prof. Juma aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mwaka 2008. Akiwa hapo,Shauri la uchaguzi kati ya Makongoro Mahanga na Fred Mpendazoe likaletwa mbele yake. Kila mtu anafahamu kilichotokea. Kwa kukumbuka tu,Mahanga aliibuka mshindi na CCM 'ikapeta'.

Mwishoni mwa mwaka jana,Jaji Prof.Juma alipandishwa cheo na kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Hapo ndipo lilipomkuta Shauri lililotolewa uamuzi jana:Shauri la Aeshi Hilary dhidi ya Norbert Yamsebo. Mlitegemea matokeo tofauti? Ingawa shauri la Yamsebo lilisikilizwa na jopo la Majaji watatu: Jaji Edward Rutakangwa, Jaji Stephen Bwana na Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma, bado Jaji Juma alikuwa na nafasi yake kubwa katika shauri hilo.

Tasnia ya sheria inafanana na ya jeshi. 'Mdogo' hutumwa na kutumikia zaidi. 'Seniority' ndio kila kitu. Kwa 'ukubwa' katika jopo hilo, Jaji Rutakangwa anaanza,halafu Jaji Bwana na tena Jaji Prof. Juma. Hivyo basi, kazi kubwa ilifanywa na Jaji Prof. Juma. Mwenye kuamini na aamini. Majaji wawili waliobaki wao 'wali-vet' kilichoandaliwa na Jaji Prof. Juma.

Sina mashaka na uwezo wa Jaji Prof. Juma. Nina mashaka na mahusiano yake na mkuu wa Serikali na chama. Kwa mahusiano hayo, CHADEMA waweza kufurukuta mbele ya Jaji huyu? Sidhani. CHADEMA watakuwa wanapiga mwereka mbele yake kila shauri. Labda aamue kutumia weledi wake ipasavyo.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dares Salaam(sasa Dodoma)

Uzuri wa JF ni bonge la back up
 
sio kweli, majaji wanapo kaa full benchi kwenye uamuzi kama mmoja hajaridhia anaunwezo wa kukataa bila wenzake kumlazimisha( decending judge) kesi nyingi za Lord Denning alikuwa asipo ridhia na maamuzi ya wenzake anakataa. hakuna seniority pale. wacha kupotosha umma. unless kama interest zako zimeguswa na hukumu zake

Is it "DISSENTING" or ' DECENDING"? nadhani the former is correct!!! Hawa ndio wanasheria wa VODA FASTA!!
 
Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji wa Mahakama ya Rufani,hakuwahi kuiangusha Serikali kwenye maamuzi yake. Tangu akiwa Mahakama Kuu,Jaji Juma aliilinda kwa nguvu zake zote Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Analipa fadhila kwa rafikiye Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Kiuweledi, Jaji Prof.Juma ni msomi washeria aliyebobea. Ana uwezo mkubwa sana. Lakini,maisha yanampokonya matumizi sahihi ya weledi wake. Ndivyo mambo yanavyotakiwa kuwa?!Akiwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jaji Prof.Juma aliwahi 'kumsave' Wakili Msomi Ridhiwani Kikwete ambaye 'alidisco'. Alimsimamia kidete hadi akabaki nakumaliza masomo yake mwaka 2005 na kutunukiwa Shahada ya Kwanza ya Sheria.

Jaji Prof. Juma alianza kulipwa alichokifanya kwa Ridhiwani mwaka 2007 pale alipoteuliwa kweye Tume ya Kuchunguza Mauaji ya wafanyabiashara watatu maeneo ya Sinza. Tume hiyo iliyoundwa na Rais iliongozwana Jaji Kipenka Musa. Baadaye, Jaji Prof. Juma aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mwaka 2008. Akiwa hapo,Shauri la uchaguzi kati ya Makongoro Mahanga na Fred Mpendazoe likaletwa mbele yake. Kila mtu anafahamu kilichotokea. Kwa kukumbuka tu,Mahanga aliibuka mshindi na CCM 'ikapeta'.

Mwishoni mwa mwaka jana,Jaji Prof.Juma alipandishwa cheo na kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Hapo ndipo lilipomkuta Shauri lililotolewa uamuzi jana:Shauri la Aeshi Hilary dhidi ya Norbert Yamsebo. Mlitegemea matokeo tofauti? Ingawa shauri la Yamsebo lilisikilizwa na jopo la Majaji watatu: Jaji Edward Rutakangwa, Jaji Stephen Bwana na Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma, bado Jaji Juma alikuwa na nafasi yake kubwa katika shauri hilo.

Tasnia ya sheria inafanana na ya jeshi. 'Mdogo' hutumwa na kutumikia zaidi. 'Seniority' ndio kila kitu. Kwa 'ukubwa' katika jopo hilo, Jaji Rutakangwa anaanza,halafu Jaji Bwana na tena Jaji Prof. Juma. Hivyo basi, kazi kubwa ilifanywa na Jaji Prof. Juma. Mwenye kuamini na aamini. Majaji wawili waliobaki wao 'wali-vet' kilichoandaliwa na Jaji Prof. Juma.

Sina mashaka na uwezo wa Jaji Prof. Juma. Nina mashaka na mahusiano yake na mkuu wa Serikali na chama. Kwa mahusiano hayo, CHADEMA waweza kufurukuta mbele ya Jaji huyu? Sidhani. CHADEMA watakuwa wanapiga mwereka mbele yake kila shauri. Labda aamue kutumia weledi wake ipasavyo.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dares Salaam(sasa Dodoma)

Mungu aliye hai akulinde sana we Mzee.
 
Back
Top Bottom