Jaji Mutungi: Vyama 18 vya Siasa vimeomba usajili, 6 tumevipatia usajili wa Muda. Vikipita vyote tutakuwa na vyama 39

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,137
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Mutungi amesema Ofisi yake imepokea maombi ya vyama vipya 18.

Kati ya hivyo vyama 6 vimeshakidhi vigezo na kupewa Usajili wa Muda/awali.

Mutungi amesema endapo vyama vyote 18 vitafanikiwa kupata Usajili Nchi Yetu itakuwa na vyama vya Siasa 39.

Source: Mwananchi
 
Huwa nasikia....'Weka Nyama'....'Utamu kolea'.

Sasa ndio naelewa huwa wanamaanisha nini!

Manake naziona hizi taarifa kana nchuzi za kachumbari tu. Nyama hamna wala nini....kha....Ukiona hivi, ni Lala salama.
 
Kuna vyama mfu Kama Ford, UMD, Demokrasia Makini, UPDP nk hivi vinangojea mikutano na semina za TCD au kutumiwa kutukana Chadema tuu.
Aache kujaza vyama vya briefcase kama vya Congo wakati wa Mobutu
 
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Mutungi amesema Ofisi yake imepokea maombi ya vyama vipya 18.

Kati ya hivyo vyama 6 vimeshakidhi vigezo na kupewa Usajili wa Muda/awali.

Mutungi amesema endapo vyama vyote 18 vitafanikiwa kupata Usajili Nchi Yetu itakuwa na vyama vya Siasa 39.

Source: Mwananchi
 
Vyama 39 ndio maana hatusogei popote, hiyo yote ni faida kwa CCM, mambo yakiwa magumu hawawezi kukosa hata vyama kumi na tano hapo viwapiga tafu pale watakapokwama.
 
Back
Top Bottom