Kwa kumbukumbu zangu tanzania bara ina mikoa 20. Zanzibar mikoa 5.
Sikumshangaa sana maana ni vigumu kuijua mikoa na wilaya zinazoundwa kama zawadi kwa wanasiasa! Ni juzi tu umeundwa mkoa wenye wilaya mbili! Nani ataweza kukumbuka vitu kama hivyo?
Nadhani ni rahisi kuchanganya, hasa kunapotokea uongezaji wa mikoa na wilaya kila siku.Nimeshangaa nimemsikia jaji mkuu mstaafu Agustino Ramadhani BBC anasema 'Tanzania ina mikoa 22 sijui 23' My take: sikufurahia kwa mkubwa huyu kushindwa kuweka kichwani mambo ya msingi kama hili; uzee nao tatizo tunahitaji hata tume kuzingatia kuwa na vijana zaidi kuliko wazee
mikoa ianyojilikana ni 26, hiyo ambayo hata mipaka haijawekwa wala haiko katika ramani rasmi ya Tanzania sio mikoa bado
Nimeshangaa nimemsikia jaji mkuu mstaafu Agustino Ramadhani BBC anasema 'Tanzania ina mikoa 22 sijui 23' My take: sikufurahia kwa mkubwa huyu kushindwa kuweka kichwani mambo ya msingi kama hili; uzee nao tatizo tunahitaji hata tume kuzingatia kuwa na vijana zaidi kuliko wazee
Wrong..hakuna Njoluma ila upo mkoa wa Njombe na hakuna Mpanda ila mkoa wa Katavi. You see...usishangae Mtu kukosea haya mambo siku hizi...Nimeuliza tu wala msinitemee cheche, angalau ukijua ilikuwa 25 kabla kuongezewa mmoja na baadaye Simiyu,Geita,Njoluma na Mpanda. Lakini kusema 22 sijui 23 lazima nishangae!
Kwani wewe mwenyewe unajua ipo mikoa mingapi?
Kama unajua tutajie hapa bila ku-consult vyanzo vingine vya habari
JK mwenyewe ukimkurupusha kwa swali umuulize kuna mikoa mingapi ... mwenyewe hajui!