JAJI MKUU atua Arusha kwa Lema

nimepatwa na wasi wasi.........
...ondoa wasi wasi...kwa maoni haya matumaini yako...

Nina imani sana na Jaji Massati ni jaji asiyeyumbishwa ( mgombea binafsi) pia Chande, hawa ni majembe 90%, wana wa Arusha anzeni kushangilia ushindi, ila M4C itayumba...dah!

Mhe.Jaji Kimario alikuwa mmoja wa majaji watatu walioamua rufaa yangu pia. Hili ni jopo lisiloyumbishwa. Huwa linapenda kufanya kazi kwa standard ya kuweka Case study nzuri kwa ajili ya mifano siku zijazo.. Nawaamini.
 

.
Massati wa Zombe? Hapa tusubiri uchaguzi mpya au labda wataona aibu kuibemunda haki maana mkuu wa mhimili yupo. Maombi kwa Mungu wa HAKI ni muhimu.
.
 

Wakimrejesha Rahaaaa wakimtema kote Rahaaa sana Maana Kipenga Kikilia Arusha CCM hawatokiiiiiii...hata siku moja...
 
Hao Majaji hawakufika hapo kwa bahati mbaya na wala hawapiti humu ili kutathmini ni wangapi wanamkubali na wangapi hawamkubali, bali wanatenda kazi zao kwa taratibu, sheria na kanuni.

Na kimsingi hiyo rufaa iko wazi huyo kijana kushinda ni sawa na Ngamia kupita kwenye tundu la sindano and after all we need no Mbunge kwa sasa....... Mkoa umetulia na kazi zinaendelea vibaya mno.........
 
Mkuu, jikumbushe Mh. Lissu alipotamka suala la uwezo wa majaji Bungeni alionekana kama mwendawazimu kabisa lakini wale wanaoelewa kidogo kidogo mpaka sasa wameshamuelewa na naamini wataendelea kuelewa zaidi!

Mh. Chande akivulunda atakuwa amechafua historia yake pia maana wanasheria wanaoelewa vizuri watatoa mchanganuo!
Tukumbuke kuwa pale Iringa askari imewatumia weeks mbili lakini walikosa jinsi na ikabdi wamfikishwe mwenzao mahakamani (japo bado kuna utata na uhalisia wa mtu/jina).

Kwa hali hiyo sio ajabu na Chande kuamua kukaa upande wa Ukweli na haki na kutoa ufafanuzi sahihi kwa kuikosoa hukumu ya awali.
Acha tusubiri

 

On top of that, hata wakili wa Majangili CCM ni Kakaake na Lissu, so naye hatakuwepo kuwatetea Magamba from the first Day, Kimomogoro atatuwakilisha fresh mpaka hapo Baadae Jembe Lissu (Tundu) atakapo m join
 
ndicho kimekuleta hapa jamvini!!!!?" &**()?xx##
 
Nikweli tusubiri hatma itakuaje mna Nchi hii si unajua mara sheria inapindishwa na wakuu wa nchi hawaoni aibu wao watachukulia poa tuu.
 
Independent Thinker Dr Ngongo,
Naomba maoni yako kwenye kadhia hii.
 
Last edited by a moderator:
chadema hoye

Mkuu hiyo kauli haipo kabisa kwenye msamiati wa Chadema tena inatia kichefu chefu kusikia hilo limsemo. Peoples Power is the voice of God and in God we Trust.
 
Independent Thinker Dr Ngongo,
Naomba maoni yako kwenye kadhia hii.

Mkuu wangu Ritz nadhani utakubalina na mimi kwamba wanaoshinda kesi yoyote iwe ya jinai au civil case mara nyingine utakuta wanashinda kwasababu ya uhodari wa mawakili wanaowawakilisha na si kwamba wana haki sana.

Katika kesi ya Bwana Lema na wanachama wa CCM yapo mambo kadhaa ambayo kama yangezingatiwa Lema asingechomoka hata kidogo lakini kwa mshangao wa wengi wanaCCM walimfungulia kesi either walishindwa kujipanga au hawakupewa ushirikiano wa kutosha na muathirika mkuu Dr Batilda na uongozi wa CCM mkoa wa Arusha.

Kwa maoni yangu Dr Batilda angetakiwa binafsi amshitaki Lema.Hilo halikufanyika badala yake wakajitokeza wanachama wa CCM ambao walidai matusi ya Bwana Lema yaliwaathiri na kupelekea mgombea wao Dr Batilda kushindwa.Mengine tuwaachie majaji wenyewe wana akili na ujuzi wa kupembua chuya na mchele.

Kwakuwa Dr Batilda hakumshitaki Bwana Lema ilitarajiwa na wengi angekuwa shahidi muhimu hasa ikizingatiwa aliyedhalilisha ni yeye na si wanachama wa CCM au chama cha mapinduzi.Kwa mshangao wa wengi Dr Batilda hakujitokeza mahakamani.

Ilitarajiwa wakili wa wanachama wa CCM wangewasilisha ushahidi wa video kwakuwa ulikuwepo lakini nao pia hakutumika mahakamani !.

Hukumu haikuwa na case law pia jaji alikosea kumkataza Bwana Lema asigombee kwasababu hapakuwa na mashitaka ya rushwa ambayo yanakipengele cha kumzuia anayepatikana na hatia kutogombea.Niko tayari kusahihishwa Mheshimiwa Steven Wasira aliwahi kuzuiliwa kugombea katika kesi aliyofunguliwa na Mhe Jaji Warioba.

Ninaamini Bwana Lema atashinda si kwasababu hakumkashifu Dr Batilda bali ni ubovu wa mawakili wa wanachama wa CCM kwa kutoiandaa kesi vyema na ubovu wa jaji aliyewapa ushindi.Ifahamike wazi ni kweli yapo baadhi ya maneno yaliyotamkwa na Bwana Lema hasa sakata la Redio Safina kama yangewasilishwa vizuri mahakamani Lema asingekuwa na jeuri ya kukata rufaa.
 
Last edited by a moderator:
Haki itatendeka,hii sio kesi ya kwanza ya mbunge kuvuliwa ubunge, kama mahakama zinapendelea basi wabungu wa CCM wasinge enguliwa. Tatizo lenu gwandaz mnafikiri kila mbunge wenu ni malaika.
 

Mkuu wangu Ngongo,
Nimekusoma kwa miwani ya 3D nakubaliana na wewe Chadema wakijipanga vizuri kwenye jopo lao la wanasheria wanaweza kumrudisha Lema bungeni. Bahati nzuri Tundu Lissu yupo na kwa mujibu wa kauli yake majaji wengi wa Tanzania ni vodafasta anakwenda kupambana nao kwenye uwanja wa sheria yetu macho matokeo yoyote ya mahakama hatuna budi kuyakubali.
 
Last edited by a moderator:
Vipi kuhusu Tundu Lisu kufiwa na baba yake? Ataweza kweli kuwepo kwenye shauri hiyo siku?
Hata Mbowe alisema akifa yeye waweke mwili wake pembeni na makamanda waendelee mbele na Jeshi la ukombozi...Naamini jembe Lisu lazima ahudhurie hukumu...
 
Arusha ilikuwa shwari baada ya huyu mwehu kupigwa chini,sala zetu zote ni kuhakikisha hoja zake zote zinatupiliwa mbali ili amani ya bwana iendelee kudumu.. Ameeeeeeeeen!!!
...huyo bwana wako ameshidwa na sasa amemtuma mke wake(CUF)...
 
Arusha ilikuwa shwari baada ya huyu mwehu kupigwa chini,sala zetu zote ni kuhakikisha hoja zake zote zinatupiliwa mbali ili amani ya bwana iendelee kudumu.. Ameeeeeeeeen!!!
Amani ya Bwana SHETANI inataka watu wakiibiwa waseme hewala baba!! wakiporwa rasilimali; hewalla baba! wakishiba wao wengine wakifa njaa waseme hewalla bwana!! amani inayotakiwa na CCMABWEPANDE ni AMANI YA SHETANI. Karibu kamanda LEMA utuondolee huu ushetani!!
 

Kwa kunisaidia mbumbumbu kama mimi, labda ungeaniambia watu wa Arusha kabla ya Lema kuwa Mbunge baada ya saa 10 jioni walikuwa wanafananya nini? natanguliza shukrani zangu kwako.
 
Nyongeza, na kwa wale ambao ni wageni hapa JF au ambao hawamfahamu huyu Member mwenzetu Ngongo huyu jamaa hampendi hata chembe Lema na haitokaa aje kumpenda. mwenye akili zake timamu anajuwa ni nini nimeongea na Ngongo ni mkweli kiasi gani kutoka moyoni mwake licha ya kwamba hampendi hata chembe Lema.
Ngongo hongera sana kwa hili kwamba nimepata kitu kutoka kwako na nitakutumia pm ni kwa nini unamchukia Lema huenda una sababu za msingi sana. viwavi wadandia hoja hawawezi kukuelewa ila naelekea kukuelewa.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…