Jaji Mkuu atangazia mashahidi kiama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Mkuu atangazia mashahidi kiama

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Sep 24, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Ni kwenye kesi za uchaguzi  [​IMG]
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani  Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani, amewataka majaji na mahakimu nchini kuwahukumu kwa mujibu wa sheria watu wanaokiri mbele ya mahakama kwamba walipokea rushwa kutoka kwa wagombea katika uchaguzi.
  Jaji Ramadhani alitoa wito huo jana jijini Dar es Salaam, wakati akifungua warsha kuhusu sheria ya uchaguzi kwa mahakimu wakazi wafawidhi nchini, inayofanyika jijini hapa.

  Alisema haiingii akilini kwa jaji au hakimu anayesikiliza shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi, kumuacha huru shahidi anayekiri kupokea rushwa kutoka kwa mgombea.
  “Sheria inasema wazi kuwa mtoa rushwa na mpokea rushwa ni sehemu ya kosa, kwa hiyo wote wanastahili adhabu, iweje wewe umuache mtu aliyekiri kupokea rushwa akaenda zake,” alihoji.

  Jaji Ramadhani alisema sheria ya uchaguzi inawaruhusu majaji na mahakimu kutoa adhabu mbalimbali, ikiwemo ya kuwafungia watuhumiwa wanaotiwa hatiani kutogombea.
  Alisema kwa vile watoa rushwa wanazuiwa kugombea, itafaa zaidi ikiwa mashahidi wanaopatikana na hatia ya kupokea rushwa katika kesi za uchaguzi, wakazuiwa kupiga kura kwa muda maalum.

  “Tusipoyafumbia macho makosa haya, watu wengi hawatakubali kupokea rushwa au kutumiwa na wagombea kuja mahakamani kukiri kupokea hongo kwa faida ya kumnufaisha mlalamikaji,” alisema.
  Alisema kuna mazingira yanayoonyesha kuwa baadhi ya mashahidi katika kesi za uchaguzi, licha ya kuapa kwa kutumia misahafu, lakini wanashiriki kuidanganya mahakama.

  Jaji Ramadhani alisema mafunzo ya sheria ya uchaguzi kwa majaji na mahakimu ni azma aliyokuwa nayo tangu akiwa katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
  Alisema azma hiyo ilitokana na ukweli kwamba hakuna chuo kinachotoa mafunzo ya sheria ya uchaguzi kwa majaji na mahakimu.
  Pia alisema maamuzi mbalimbali yaliowahi kufikiwa na mahakama katika kesi hizo, hayakuzingatia taratibu za uchaguzi.

  Alisema kuwa maamuzi hayo kwa kiasi kikubwa yalifikiwa kutokana na majaji na mahakimu kutoifahamu vizuri sheria ya uchaguzi.
  Maamuzi hayo aliyoyazungumzia Jaji Ramadhani yalihusu hukumu iliyowahi kufikiwa na Mahakama Kuu, kutengua ushindi wa mmojawapo wa wagombea ambao hata hivyo hakumtaja kwa jina.

  Alisema hukumu ya kubatilisha ushindi wa mgombea huyo, ilitolewa kwa sababu ya kukuta baadhi ya kufuli na sili za masanduku ya kupigia kura, zikiwa zimechezewa.
  Uamuzi mwingine ni ule uliofanywa na Mahakama Kuu wa kutengua sharti la kuweka Sh. milioni tano, kama dhamana ya mtu kuruhusiwa kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge.
  Aliwataka mahakimu wanaoshiriki kwenye warsha hiyo, kujifunza kwa umakini kwa kuwa watashughulikia malalamiko na rufaa za uchaguzi zitakazowasilishwa mahakamani.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Tufuatilie kesi ya Mwakalebela labda italeta change
  Ila kauli ya JAJI mkuu ni pigo kwa TAKOKURU kwa jinsi wanavyopika kesi za rushwa zisizo na mashiko. Haiwezekani mtu apokee rushwa ndipo akatoe ripoti. toa ripoti kwanza upewe hela za moto za kutimiza lengo kisha waachie takukuru wafanye kazi ndipo utakuwa shahidi mzuri. Haiingii akilini kusema kwamba jamaa juzi alinihonga thumuni nikachukua naomba ashtakiwe. NOOOO WAY
   
 3. M

  Mwanantala Senior Member

  #3
  Sep 25, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hili likitekelezwa kwa vitendo litapunguza kubambikiana kesi.
   
 4. M

  Mutu JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mhhhhhhhhh
   
Loading...